Hivi sisi tukoje?

Walifanya sahihi kuonyesha ili iwe fundisho kwa watu wengine wanao ishi kiujanja ujanja mjini.
 
Walifanya sahihi kuonyesha ili iwe fundisho kwa watu wengine wanao ishi kiujanja ujanja mjini.
hapa sikubaliani na wewe kwa sababu wote wanaopigwa/kuchomwa moto mpaka kuuwawa si vibaka...kuna mwanafunzi wa chuo alishawahi kupigwa mpaka akauwawa eti kwa sababu alipita karibu na nguo zilizoanikwa na mtu mmoja akapiga kelele za mwizi...ingekuwa ni mimi nipo kwenye mamlaka husika ningeiangalia vizuri ile footage na wote walioakuwa wanamwagia mafuta/kumpiga/kumuwekea majani ili moto ukolee wote wangekutana na mvua kali ya sheria...!
 
Itv wako saihihi kabisa ,ila lazimama watoe tadhari kwamba picha hii sio nzuri kwani inatisha au haifai kwa watoto, wewe unaesema haikuwa saihi ngoja nikupe ethic nyingine anayo unatakiwa kufanya muandishi.kama kuna mtoto mdogo barabarani na kuna gari lina kuja kumgonga yule mtoto ki ethics za uwandishi unatakiwa upige picha lile tukio na sio kumuokoa huyo mtoto.kupiga picha kwako kutatoa fundisho kwa watu wengine .kama utaweza kupiga picha na kumuokoa ni jambo zuri ila lakwanzan ni kupiga picha :Thats News
 
Ni sahihi kwa kuwa hatuna askari nchi hii
waliopo ndo wanaowatuma.
kwa anaebisha ngoja yamkute utakuwa wa kwanza!!😛oa

Mkuu, huu ni uvunjifu wa sheria zetu wenyewe, sasa wabunge wakijiongezea posho kimyakimya msilaumu kuwa hawakufuata taratibu na sheria za nchi.

Hakuna sheria ndogo au kubwa, sheria ni sheria tu.

Turudi kwenye mada, hawa ITV walitakiwa basi watoe tahadhari kuhusu picha watakazo onesha kuhusu tukio hilo la kijana kuchomwa moto mpaka kifo.
 

Hivi ITV ni bure? Asee tangu haya madish ya kichina yaanze kuleta chenga chenga mi nalipia ITV bana nina kama nusu mwaka sasa! Bure yao kwenye antena au dish gani mkuu
 
Picha ile haikuwa nzuri kuionyesha. Siku ile Mkulu anadondoka pale Jangwani hawakutuonyesha. Waliikatiza. Ya vibaka wanayakomalia!
 
@mende0, hapo juu nilikuwa nakujibu ile msg yako uliosema ukikuta kibaka anapigwa na wewe utashiriki kumsulubu...!
 

Mkuu kuchukua sheria mikononi ni kosa, lazima tufuate sheria zetu.

Hii haina tofauti na wakurugenzi wa halmashauri wanaokula hela za miradi, ni makosa.
 

Wakienda wapi wanaperform: TBC ama Clouds? Kwa maoni yangu ITV ndio chombo ambacho kipo relatively free ukilinganisha na vingine vya hapa nchini na kwa msingi huo watangazaji wake wana nafasi ya kuperform vyema zaidi wakiwa hapo hapo ITV.
 

Napata ufahamu hapa wewe hujawahi ibiwa kitu na hujakumbana na machungu ya kuibiwa wewe.
 
Kama unaona soo kuangalia si bora ufuatilie news za radio? Tv kuonesha ndo usahihi wenyewe. Sikubaliani na wewe hata kidogo.
 
MAY THE FORCE BE WITH YOU ALL !!!!!!!!!!!!!

Kama kuonyeshwa kibaka aliebondwa na kuchomwa ni injustice, mbona tumesha ona watu waki katwa vichwa, walio jivisha mabom na hata askari wa Israel wakiuwa baba na mtoto wake mdogo asiye na hatia?

Tunadai maendeleo. Yanapo kuja tuna yalaani. Tunadai uhuru wa habari, tunapopewa, tuna laani. Nini kitaturidhisha an kutufurahia?

TV ni yako. Iko nyumbani kwako. Ukiona kuna habari au documentary huipendi au haifai, simle. ZIMA. Waache wenzako waone.

Zungumzia kuhusu kitakacho kutoa kwenye uamskin lakini sio kuwapangia wengine nini waangalie.
 
Hivi ITV ni bure? Asee tangu haya madish ya kichina yaanze kuleta chenga chenga mi nalipia ITV bana nina kama nusu mwaka sasa! Bure yao kwenye antena au dish gani mkuu
Haya yanaweza kuwa na mantiki maana mimi natumia dish mediacom nina kama wiki tatu hivi ITV siipati kabisa licha ya fundi kuhangaika bila mafanikio.
 
Napata ufahamu hapa wewe hujawahi ibiwa kitu na hujakumbana na machungu ya kuibiwa wewe.
Hapana mkuu, nimeshaibiwa mara nyingi sana lakini kwa kweli sina ujasiri na wala haiingii akilini mwangu kumpiga ,kumwagia mafuta na kuua binadamu mwenzangu hata kama ni kibaka. Wewe ukisikia siku ndugu yako wa karibu amefanyiwa hivyo hata kama kweli ni kibaka ndiyo utajua nina maanisha nini. Wewe unayeshiriki kumuua kibaka huoni unafanya kosa kubwa kushinda alilofanya kibaka mwenyewe na unastahili adhabu kubwa kupita hata atakayepata kibaka kama angepatikana na hatia? Nakushauri ukikuta kibaka anachomwa ufanye kama wale wasamalia wema waliokuwa wanayatoa yale majani yalikuwa yanamuwakia moto.
 
wanatakiwa watoe warning juu ya images kama hizo-then waonyeshe mzigo mzima kama ulivyo bila ku-edit kitu
 
A person is torched to death in broad daylight and some people think that is okay. SMH!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…