Vocal Fremitus
JF-Expert Member
- Oct 20, 2016
- 1,191
- 6,011
Kwanza niweke wazi mimi bado sijaoa. Nipo kwenye early 30s na sina mpango wa kuoa kwa sasa. Na hata ikitokea naoa sitaki mchango wa mtu.
Kuna jambo limenikuta. Yani nina classmates na washkaji zangu kama sita hivi wote wapo mbioni kuoa mwaka huu na mwanzo wa mwaka ujao. Wote wanataka michango. Na wote michango yao ni zaidi ya 50k kila mmoja.
Kuna hawa wawili tulishapotezana huu mwaka wa sita tangu tumalize chuo na hatujawahi kuonana tangu kipindi hiko. Lakini wamepambana mpaka wakapata mawasiliano yangu. Wote wameniunga katika magroup yao ya whatsapp ya kuchangisha michango. Mmoja ameset kabisa kiwango mchango ni 100k kwa single, na 130k kwa couple.
Nikijitazama niko mbali nao kijografia na uwezekano wa kushiriki katika harusi zao ni mdogo sana. Lakini kwangu wamekua kama kero. Leo asubuhi nimekuta missed call nane na sms za kuombwa michango yao ya harusi. Kwakweli nakwazika sana.
Ndoa sio jambo la dharura. Sio busara kusumbua watu wakuchangie.