Hivi siasa za chuki zitaisha lini?

Hivi siasa za chuki zitaisha lini?

S.N.Jilala

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
540
Reaction score
507
Ukifuatilia kimatendo, huwezi kuona sera wala itikadi yoyote ambayo inaendeshwa kwa sasa kati ya vyama viwili yaani CCM na CHADEMA. CCM ili kufanikisha mambo yao ambayo wanataka yawe mara nyingi wakiibuka ni kuwashambulia CHADEMA kwa maneno mengi ya kebehi na vioja vingi sana. Na CHADEMA nao wakiibuka wanawashambulia CCM kwa maneno mengi, kebehi na vioja pia.

Kitu ambacho kwa sasa ni ngumu au nadra sana kukiona ni hiki cha kueneza sera na itikadi ya vyama hivi viwili. Havipambanishi sera wala itikadi tena. Kwa sasa sioni kabisa kama kuna siasa inafanyika zaidi ya chuki tu. Ni vyema tuache chuki sote na tujikite kwenye siasa iliyo bora. Tukubaliane kutofautiana kama sera na itikadi zetu zilivyo tofauti katika katiba ya vyama vyote.

Kwa bahati nzuri au mbaya sana, CCM wana sehemu ya kujificha kama wakiona wamezidiwa na upande wa CHADEMA.

OMBI LANGU KUU.

Suluhisho ya yote hapo juu.

Tunahitaji katiba mpya ambayo itavifanya vyama vyote vya siasa kufanya siasa iliyo nzuri. Kilio changu Mimi ni kwamba, uendeshaji wa maswala ya kisiasa unatakiwa iwekwe vyema kabisa kwenye katiba ili kuwafanya Watanzania kushiriki vyema katika maswala yote ya kisiasa hasa yanayohusu maisha yao na si haya yanayoendelea kwa sasa. Na lazima maoni ya wananchi yazingatiwe na si maoni ya wachache na kujifanya kuwa ni maoni ya wengi. Tulianza vizuri kwenye Tume ya Warioba lakini siasa za chuki zikatupoteza kwenye msitari.
 
sijui umekosea jukwaa au mimi ndo siyajui
 
Back
Top Bottom