Ngalikivembu
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,959
- 874
Ninajua kuwa mapumziko yoyote ya kitaifa nchini Tanzania yapo kisheria. Hata wakati nasoma somo la uraia tulisomeshwa kuwa kuna Sherehe za kidini zinazo tambulika kisheria ambazo lazima tupumzike. Hakuna kwenda kazini kwa wafanyakazi Wote wa serikali na wa Sekta binafsi.
Pia mashule nayo yanaenda mapumziko kama kawaida. Haihitaji kuuliza kwa Mwalimu mkuu au mkuu wa shule kujua wanafunzi waje au wasije shule. Sherehe kama Mapinduzi, Muungano, Uhuru, Nane nane, Nyerere day, Karume Day ni mapumziko ya moja kwa moja. Hizi ni za upande wa kiserikali.
Sherehe kama mwaka mpya, ijumaa kuu, jumapili ya pasaka, jumatatu ya pasaka, Maulid, Idd El Fitr, Krismas, Boxing Day ni mapumziko kwa upande wa kidini.
Katika siku za hivi karibuni nimeona mambo yanaenda tofauti. Wanafunzi hivi sasa wanaenda kama kawaida shuleni. Ukiuliza kulikoni wanafunzi wanasema tumeambiwa twende na mwanafunzi asiye enda anapewa adhabu. Hili likoje? Walimu wamepewa mamlaka ya kuamua hili?
Nimeshuhudia mwaka huu. Ijumaa kuu wanafunzi walienda shule. Muungano pia nimeona wanafunzi wameamriwa kwenda kukaa darasani kama kawaida. Kuna mabadiliko yoyote huko mashuleni yametokea tofauti na enzi zetu?
Wenye kuelewa zaidi naomba waje.