Haki za wafanyakazi siku hizi hazipo kabisa.Nakumbuka nilipoanza kazi nilisaini mkatataba na serikali ambao hata hivyo ulivunjwa bila mimi mwenyewe kushirikishwa.Leo mfanyakazi hana haki yeyote.Nakumbuka niliahidiwa kupata matibabu bure Grade I,badala yake imeingizwa bima ya afya bila kushirikishwa.Tuli ahidiwa pia malipo ya nauli tukienda likizo,leo malipo hayo wanapewa wafanyakazi wachache tu,wengine ni kama kitu ambacho ni zawadi,si kitu mfanyakazi anachostahili.Hata ukipewa inabidi aende kwanza akirudi eti ndio adai.Kwa mshahara upi hasa unao muwezesha mfanyakazi kwenda halafu akirudi adai kama sio fisadi.Wengine kufuatana na ngazi tuliahiwa umeme na maji bure,lakini leo inabidi tujilipie umeme wenyewe.Haki hii hii iliondolewa kinyemela na bila maelezo yeyote.Kila mfanyakazi aliahidiwa nyongeza ya mshahara kila mwezi,lakini bila maelezo na kinyemela kabisa haki hii pia ikaondolewa.Leo serikali inatoa mshahara wa mfanyakazi wakati inapopenda.Mara tarehe 22,mara 23 n.k.Leo hii ninapoandika thread hii ni tarehe 30,na wafanyakazi hawajui watapata mshahara wao tarehe ngapi.Kama serikali imefulia watuambie wazi.Kama mimi mfanyakazi wa ngazi ya juu naona ni matatizo,jee mfanyakazi wa ngazi ya chini hali yao ikoje.
La msingi zaidi ni mipango ya kazi na malipo ya kila mwezi.Kwa ujumla mabadiliko ni makubwa mno.Kama mtafiti pesa ya kufanyia kazi na vifaa haikuwa tatizo kabisa.Leo inabidi kubangaiza kutafuta pesa za kufanyia kazi.Mpango wa serikali ni kutegemea zaidi wafadhili ambao hata hivyo wana malengo tofauti kabisa na ya kwetu.Nia yao kwa hakika ni kutukwamisha kabisa.
Kwa ujula matatizo ya wafanyakazi wa serikali ni makubwa sana na kama serikali haikufanya mipango ya makusudi kabisa ya kuyarekebisha tunakokwenda ni kubaya.