Hivi serikali imefilisika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi serikali imefilisika?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by demokrasia, Dec 2, 2011.

 1. d

  demokrasia Member

  #1
  Dec 2, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari zenu wana JF? Hivi hii tabia ya serikali kuchelewesha mishahara ya watumishi wa umma inasababishwa na nini? Leo ni tarehe 2 lakini kila nikienda kwenye akaunti sikuti chochote. Au serikali yetu ndio inafilisika? Lakini mbona serikali imeweza kuwaongezea wabunge posho za vikao kwa asilimia 150% kutoka sh. 70,000/= hadi sh. 200,000/= kwa kila kikao? Kwa nini inashindwa kuwalipa watumishi wa Umma mishahara yao kwa muda unaotakiwa? Hivi serikali ni kwa nini inafanya maamuzi kisiasa badala ya kufanya maamuzi kwa kuzingatia utaalamu? Hii nchi mambo hayaendi vizuri kwa sababu serikali inaingiza siasa kwenye kila jambo. Wananchi tunateseka sana na hii Serikali. Maisha ni magumu sana. Hii miaka minne iliyobaki, kwa kweli cha moto tutakiona.
   
 2. H

  HAKI bin AMANI Senior Member

  #2
  Dec 2, 2011
  Joined: Sep 5, 2011
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali legelege huwekwa mfukoni na wenye fedha. Sasa hivi inawabembeleza mafisadi na matajiri wanaokwepa kulipa kodi wawakwamue ili kuweza kulipa mishahara. Si wewe tu ambaye hujalipwa mshahara kwani ni baadhi ya wizara tu zile zinazoitwa nyeti ndiyo wamelipwa wengine bado. Haijalishi kama upo kwenye jiji lenye ikulu ya Rais au Nakapanya au Nanguruwe. NSSF wamestuka kukopwa kila mwezi lakini madeni hayalipwi. Usanii mtupu wa serikali ya JEIKEI. WaTz tulivyofunikwa na blanketi zito liitwalo AMANI, mpaka tutakapozinduka, itakuwa kushney. Lakini naisifu serikali kwa kuwa na msimamo wa kutotangaza kufilisika kupisha aibu, ingawa hilo siyo jawabu lake kwani wahenga walisema mficha uchi hazai.
   
Loading...