Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,162
Tumeshuhudia teuzi za Rais Magufuli zikiwa ni za moto kweli kweli, na kwa wengine wamekuwa hawadumu kwenye teuzi hizo zaidi ya miezi 6 tokea wateuliwe!
Swali kubwa linaloulizwa na watanzania hivi sasa, je Rais yuko fair katika utumbiuaji wake?
Hebu tuchukulie mifano ifuatayo:-
Tumeshuhudia watanzania wengi wakimlalamikia Mkuu wa Mikoa wa Dar, Paul Makonda, kuwa anatumia jina la bandia na cheti chake ni cha kufoji na jina lake halisi ni Daudi Bashite
Lakini tumeona Mkuu wa nchi akijibu tuhuma hizo kuwa yeye hajali mtu kama ametumia vyeti vya kufoji, anachojali yeye ni uchapaji kazi na kwa kuwa Paul Makonda anamchapia kazi, na anamkamatia wauza madawa ya kulevya, akamhimiza chapa kazi dogo!
Mfano wa pili ni wa Mkuu mikoa wa Arusha, Mrisho Gambo, ambaye alinukuliwa akiwahamasisha Umoja wa Kina mama wa Mkoa wa Arusha, ikibidi wawafanyie fujo wapinzani, kwa kuwa jimbo la Arusha mjini ni lazima lirudi CCM!
Mfano mwingine ni wa Mkuu mpya wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti, ambapo Mbunge Joshua Nassari alionyesha ushahidi wa dhahiri wa namna alivyokuwa akigawa rushwa kwa madiwani wa Chadema, ili wajiunge na CCM
Mfano mwingine ni jinsi yule kijana Akwilina alivyouawa kwenye maandamano ya Chadema, ambapo tulimsikia Kamanda Maalum wa Polisi wa Dar, Athumani Mambosasa, akikiri kuwa mmoja wa askari wake ndiye aliyehusika na mauaji hayo na kuwa askari wake 6 wapo ndani kwa uchunguzi zaidi
Lakini tulishangaa baada ya siku chache DPP akijitokeza na kutuambia kuwa faili hilo wamelifunga baada ya kutombaini mtu aliyemuua mwanafunzi Akwilina!
Unajua kwenye familia mnapokuwa na mzazi ambaye anaonyesha upendeleo wa dhahiri kwa mmoja wa watoto wake, hao watoto wanatokea kumdharau mzazi huyo!
Je hiyo ndiyo hali iliyolikumba Taifa kwa hivi sasa??