Hivi Rais hatoi Nishani tena?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Nakumbuka kuliwahi kuwepo na nishani za Uhuru, Nishani ya Utumishi wa Muda Mrefu, Nishani ya Utumishi Uliotukuka, Nishani ya Vita ya Kagera, Nishani ya Kilimanjaro (the highest civilian medal) n.k

Nishani hizi zilikuwa zinatolewa kwa wanajeshi na watumishi wa umma na hata wananchi wa kawaida. Ilikuwepo (sijui kama bado ipo) na Nishani ya Shaaban Robert ambayo ilikuwa inatukuza lugha ya Kiswahili.

Kwa miaka hii michache sikumbuki kama nishani hizi zimetolewa kwa wananchi wa kawaida ukiondoa zile ambazo zinatolewa Jeshini, Polisi, Magereza n.k ambazo nyingi zinakuja kutokana na utumishi au utendaji fulani wa kijeshi.

Ni raia gani wasiowanajeshi ambao wamepata kutunukiwa nishani na Rais Kikwete - ukiondoa zile za "vita" ya Comoro?
 
Naskia umewaamuru Chadema waombe radhi?

Are you sirias?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom