Hivi nini kilimpata Rais Samia akatoka Kenya na barakoa?

Kama wewe huwezi dhurika na corona baada ya chanjo lakini unaweza ambukiza ambao hawana chanjo je unatakiwa uvae au usivae barakoa? Hiyo chanjo unajua inavyofanya kazi au umesikia kwa yule Gwajiboy mwana gang mwenzio!
Ukichanjwa unapataje maana huwezi kuambukizwa wala kuambukiza
 
Ok tuseme ni kweli, wewe kataa kuchanjwa uone kama kuna mtu atakufata na bakora kukulazimisha uchanjwe.
Sichanjwi na barakoa sivai ili asilishe taifa, kwa taarifa za kuzitoa kwa aliyeathirika
 
Yaani unataka aapishwe leo kesho aonyeshe kwenda kinyume na mtangulizi wake, unajua forces za power wewe?

Yaani hujateua mtu wako hata mmoja kwenye key position unataka uende against mtangulizi wako?

Transition to power huwa inaenda slow, ukitaka kuonyesha uko against na mtangulizi wako kwa vitu vya msingi harakaraka unakuwa unamobilize force za kukukwamisha mapema kabisa
We jamaa bwana yaani kuvaa barakoa kuna uhusiano gani na transformation of powers?? Kwan ai alienda baada ya kuteua baraza la mawaziri? Tayark alikuwa na serikali tiifu kwake. Kwanini hakutangaza uwepo wa korona mbona alianza.kuvaa barakoa hata kabla ya kupokea taaeifa ya kamati yake?
 
Mada ya maana Ila mnajadili kipumbavu sana. JK wnaingiaje humu wapuuzi sana. Jikitrni kwenye mada anayepinga aweke sababu na anayemsapoti aweke sababu Ila mkianza kutaja wasiohudika ni ujinga mnapogeza maana ya thread inaanza kuonekana ipo politically oriented.

Mwacheni JK apumzike kama anaenjoy mwacheni pia sukumagang
Tupo watu tofauti sana kimtazamo
 
Yaani mtu ana ushahidi usio na chembe ya shaka kuwa Vice President wake alipata Korona nusu imuue halafu unataka akae na kuamini kuwa Tanzania hakuna Korona?

Mama hana ubishi usio na maana kama Jiwe, Jiwe aliamua kututoa Kafara, alijali kufunika aibu ya misimamo yake iliyotugharimu sana kwenye wimbi la pili at the expense ya maisha ya watu.

Huenda Kenyatta alimpa mama Mkanda Mzima wa Jiwe alivyokwenda Kenya kimyakimya kutafuta matibabu ya Korona. Mama akaona kuwa hii kitu ni real siyo ya kufanyia mchezo

Humu kwenye JF ni sisi tulimwambia ajilinde
Kwa jinsi ulivyomuelezea Rais umemshusha hadhi yani kwamba hakuwa hakijua umuhimu wa kuvaa barakoa wala kujua ukweli wa kuhusu corona hadi pale alipoenda Kenya? basi tuna rais wa hovyo haijapata kutokea.
 
Rais hapangiwi, kaamua kuvaa barakoa basi anavaa, kama wewe hutaki kuvaa hujalazimishwa uvae
 
Kuna nchi flan ilitawaliwa kidikteta, wananchi wakalalamika chinichini maana hakukuwa na mtu aliyethubutu kunyanyua kinywa chake, bahati mbaya yule bwana akafa, mtu mwingine akatawala , huyu mtawala wa pili akawa anamkosoa saana mwendazake kwamba alinyanyasa saana raia.

Mwandishi mmoja akaandika kinote bila kuandika jina lake kikamfikia rais kikisema " mbona hkuyasema haya wakati mwenyewe akiwepo??"

Rais akakisoma kile kinote kwa sauti, kila mtu akawa kimya kisha akauliza "nani aliyeandika hiki kinote??"

Kila mtu akawa kimyaaa hata yule aliyekiandika hakunyoksha mkono.

Rais akaulisa swali lie lile mara kadhaa bila mtu kujitokeza.

Kisha akawaambia kama kuna mtu ameandika hiki kinote na yupo hapa anashindwa kujitaja mlitaka mimi misemaje haya mbele ya mwendazake??

hope umenielewa
Walikuwa wanaogopa wataharibu ulaji wao ndio maana huwezi kuona hata mmoja kujiondoa kwa kutofautiana mawazo na mkubwa wake kama wenzetu wanavyofanya.
 
Rais hapangiwi, kaamua kuvaa barakoa basi anavaa, kama wewe hutaki kuvaa hujalazimishwa uvae
Mimi sipo kwenye kumpigia wala kupinga kuvaa barakoa, nimezungumzia jinsi ambavyo wewe ulivyomuelezea huyo Rais ndio nimesema kama ulivyoeleza ndio kweli basi huyo atakuwa rais wa hovyo yani kipindi chote hiki alikuwa hajui ukweli wa corona hadi alipoenda huko Kenya yani hata humu Jf walikuwa wanajua ila yeye hajui sasa huyo si ni rais wa hovyo?
 
Rais hapangiwi, kaamua kuvaa barakoa basi anavaa, kama wewe hutaki kuvaa hujalazimishwa uvae
Avae yeye asilazimishe na watendaji wake wavae maana wao ndio taswira ya taifa wanataka kuiambia dunia nini wakati ilishashangaa hatukuanguka kama wao?

India ni mabingwa wa dawa hata viongozi wetu wanatibiwa huko, wanatengeneza vaccines zao na bado wanapigika vilivyo mbona hizo barakoa na dawa haziwakingi?
 
Walikuwa wanaogopa wataharibu ulaji wao ndio maana huwezi kuona hata mmoja kujiondoa kwa kutofautiana mawazo na mkubwa wake kama wenzetu wanavyofanya.
hawa jamaa ni vinyonga kabisa wanacheza na rangi ya pori.
 
Mimi sipo kwenye kumpigia wala kupinga kuvaa barakoa, nimezungumzia jinsi ambavyo wewe ulivyomuelezea huyo Rais ndio nimesema kama ulivyoeleza ndio kweli basi huyo atakuwa rais wa hovyo yani kipindi chote hiki alikuwa hajui ukweli wa corona hadi alipoenda huko Kenya yani hata humu Jf walikuwa wanajua ila yeye hajui sasa huyo si ni rais wa hovyo?
Thats is exactly my point
 
Maza alienda Uganda akatuaga uwanjani bila barakoa, alipofika kule alivaa coz ni sheria za UG kutokana na kupigwa kiasi na CORONA.

Alirudi bila BARAKOA maisha yakaendelea. Then akaenda Kenya Kwa Kenyatta akavaa barakoa maana wale jamaa walinyooshwa na wanaendelea kunyooshwa vilivyo na hii pandemic.

Sasa baada ya kurudi yaani akili imembadilika kabisa kaja na mitazamo tofauti na alichokiamini kabla na baada ya JPM kuondoka.

Kaanza kusisitiza uwepo wa CORONA wakati sisi raia tunasonga mbele kibingwa, tunabanana kama kawa kwenye vyombo vya usafiri, kumbi za starehe na nyumba za ibada.

Mara ile Tume yake ikaja na mapendekezo kwamba tutambue "uwepo wa covid" nikashangaa hii Tume imefanya kazi kwa weledi au ndio kumfurahisha aliyeiteua??

Hapa mama kingia disco la CHADEMA saa11 asubuhi wakati DJ anapiga ngoma za.kumalizia huku vijana wake wameanza kukusanya spika na nyaya.

Sasa nabaki najiuliza hizi chanjo za nini wakati sisi tupo poa tu yaani tunasonga kibabe mbele ya covid.

Hii MIBARAKOA WACHA WAVAE WANASIASA NA FAMILIA ZAO ILI KUWAFURAHISHA WANAOTAKA TUWE NA KORONA NA MTASHANGAA

"THE SO CALLED NEXT CORONA WAVE HILL HIT REAL HARD " bacause of this so vaccines

Hizo chanjo wajichanje wenyewe na hao walioenda kuzileta.

Watz kwa hili acha nisimame na " mwendazake"

Nimemaliza!!View attachment 1792943
Aliona makaburi mengi sana yakamtisha
 
Ndugu yangu hii nchi ina platform ya kusemea haya mambo kwa niaba ya wananchi. Bungeni! Wabunge wapo tena wengine hadi kiwango cha PhD kwanini msiwapush waseme haya hadharani kwa niaba ya wananchi? Hakuna sababu ya kulalamika nyuma ya keyboard ilhali tunawakilishi. Kama unaona hili jambo ni tishio kwa Taifa mfikishie Mbunge wako malalamiko yako. Hapa unachofanya ni personal attack kwa mama Salimia Suluhu bila sababu. Yeye kuvaa barakoa wewe inakuumiza nini?
Wameisha katazwa kudemka, na walifuatwa hapo hapo Bungeni na Nduguyo na Muongo umewasikia
 
Maza alienda Uganda akatuaga uwanjani bila barakoa, alipofika kule alivaa coz ni sheria za UG kutokana na kupigwa kiasi na CORONA.

Alirudi bila BARAKOA maisha yakaendelea. Then akaenda Kenya Kwa Kenyatta akavaa barakoa maana wale jamaa walinyooshwa na wanaendelea kunyooshwa vilivyo na hii pandemic.

Sasa baada ya kurudi yaani akili imembadilika kabisa kaja na mitazamo tofauti na alichokiamini kabla na baada ya JPM kuondoka.

Kaanza kusisitiza uwepo wa CORONA wakati sisi raia tunasonga mbele kibingwa, tunabanana kama kawa kwenye vyombo vya usafiri, kumbi za starehe na nyumba za ibada.

Mara ile Tume yake ikaja na mapendekezo kwamba tutambue "uwepo wa covid" nikashangaa hii Tume imefanya kazi kwa weledi au ndio kumfurahisha aliyeiteua??

Hapa mama kingia disco la CHADEMA saa11 asubuhi wakati DJ anapiga ngoma za.kumalizia huku vijana wake wameanza kukusanya spika na nyaya.

Sasa nabaki najiuliza hizi chanjo za nini wakati sisi tupo poa tu yaani tunasonga kibabe mbele ya covid.

Hii MIBARAKOA WACHA WAVAE WANASIASA NA FAMILIA ZAO ILI KUWAFURAHISHA WANAOTAKA TUWE NA KORONA NA MTASHANGAA

"THE SO CALLED NEXT CORONA WAVE HILL HIT REAL HARD " bacause of this so vaccines

Hizo chanjo wajichanje wenyewe na hao walioenda kuzileta.

Watz kwa hili acha nisimame na " mwendazake"

Nimemaliza!!View attachment 1792943
Tuache upuuzi wa kudharau sayansi
 
Avae yeye asilazimishe na watendaji wake wavae maana wao ndio taswira ya taifa wanataka kuiambia dunia nini wakati ilishashangaa hatukuanguka kama wao?

India ni mabingwa wa dawa hata viongozi wetu wanatibiwa huko, wanatengeneza vaccines zao na bado wanapigika vilivyo mbona hizo barakoa na dawa haziwakingi?
Watendaji wake kama hawataki kuvaa wasivae huko majumbani kwao, lakini wakiwepo mahali yeye yupo lazima wavae ili wasije wakampa rais wetu Korona.

Magufuli alijifanya mbabe kutovaa barakoa Korona ikamuondoa
 
Back
Top Bottom