Hivi ni ugumu wa maish au?

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WIMBI la wanaojinyonga wenyewe linazidi kuongezeka siku hadi siku sababu ambayo wananchi wanashindwa kuelewa linatokana na chanzo gani kutokana na watu kuamua kukatiza uhai wao wenyewe
Mbali na kujiondoa uhai watu wameonekana kubadilika mioyo yao na utu umeisha kutokana na watu kushindwa kuaminiana kufanyiana mambo ya kinyama hali ambayo inatishia maisha kwenye jamii

Inawezekana ugumu wa maisha unachingia auu? Mana siku hizi ukitembea barabarani kukuta mtu anaongea peke yake imekuwa ni kawaida na idadi hiyo inazidi kuongezeka kila kukicha.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, David Miseme, ametoa taarifa jana kuwa, mkazi wa Mbagala, Abdallah Mohamed (25), amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya manila aliyokuwa ameitundika kwenye dari chumbani kwake.

Amesema tukio hilo lilitokea juzi saa 12 jioni huko Mbagala anakoishi.

Amesema sababu ya kujinyonga haikupatikana mara moja uchunguzi unafanyika.

Matukio haya yamekithiri sana kila kukicha makamanda wanatoa taarifa kuhusiana na watu kujiua wenyewe kwa kutumia vitu mbalimbali vikiwemo sumu na vinginevyo vinanyoua
 
Ni kweli Mzee Kilimasera, watu wanajinyonga sana, wanauana sana, sababu kubwa nafikiri ni ugumu wa maisha. japo kuwa kwa kujinyonga siyo suruhisho pia, maana uendako hukujui pia. dawa ni kukomaa nao tu hadi kieleweke:second::second:
 
Husniyo na Sweetlady, avatar zenu mmezitupa wapi!!
 
Tusiwe na majibu mepesi kwa maswali magumu. Tusisingizie ugumu wa maisha. Kwani ni wakati gani maisha yaliwahi kuwa rahisi kwa mwanadamu. Swala ni kwamba watu wengi wamemuasi Mungu siku hizi,na hayo ni mojawapo ya matokeo ya kuwa mbali na Mungu.
 
Back
Top Bottom