Hili ni swali fikirishi. Tumeshuhudia mara kadhaa Vyombo vya Dola (TCRA, SERIKALI) vikitoa adhabu ya kuvifungia kutoa huduma vyombo vya habari pale vinapokiuka taratibu hata pengine sheria. Tumeshuhudia hivyo kwa gazeti la Mwananchi, gazeti la Tanzania Daima na hivi majuzi kituo cha TV cha Wasafi.
Swali la kujiuliza ni mamlaka zinapofanya hivyo zinamlenga nani na na anaumia katika kutoa hiyo adhabu. Kanuni moja ya msingi ni kuwa adhabu itolewe na kumwathiri aliyetenda kosa. Chombo cha habari kinapofungiwa kutoa huduma anayeathirika siyo mmiliki wa chombo pekee.
Wafanyikazi, familia zao watoa matangazo na wapata huduma mbalimbali. Hao wote wanaadhibiwa kwa kosa ambalo hawakuhusika moja kwa moja. Napendekeza mamlaka zibuni adhabu zitakazomuathiri mtenda kosa bila kuwagusa wasio na hatia.
Nawakilisha.