Hivi ni sahihi kudaiwa hela ya kutolea kwenye simu pale unapotuma pesa kama msaada ?

Kifaru86

JF-Expert Member
Apr 22, 2017
1,734
3,810
Jamani Nina rafiki yangu alinitafuta siku mbili tatu hizi alikuwa na shida kama elfu 30 alikuwa na matatizo kidogo ya kifamilia nimsaidie elfu 30.

Basi kwa vile mshikaji namfahamu nilienda m-pesa nikamtumia kama elfu 30 kama ilivyo ili na Mimi kwenye simu nibakie hata hela ya emergency kama elfu tatu vile.

Baada ya kutuma nilimpigia kama text ameiona akaniambia ndio kaionaa lakini akaniambia mbona ujatuma hela ya kutolea nikamwabia ndio hiyo nilikuwa nayo tuu akanijibu basi poa akakata simu yangu . ......

Na HAPA ndipo najiuliza ivi sahihi mtu kukudaii hela ya kutolea wakati we mwenyewe umejitolea kama msaada
 
Hilo jipu....linakufanya wewe ndio wa kutatua shida yote...tena umefanya vizuri ili apate akili nyingine ya kupatia elfu mbili ya kujazia. Kuna miwatu hainaga shukrani...usije ukamsaidia hadi shida ikaisha kabisa...maana utamuharibu mwenzio atakuwa hawazi kitu. Ni maoni yangu tu!
 
Unaomba hela ya msaada au mkopo nitakayo kutumia ni ile uliyoniomba tu, nyingine ya kutolea utajiongeza mwenyewe, (except wazazi)

Maana mtu wa dizain ya kudai ya kutolea mara nyingi hata akikurudishia hakurudishii ya kutolea.
 
Yaani umemtatulia tatizo 99% lakini shukurani 02%
Si lazima kutuma ya kutolea.
OVA.
 
Hilo jipu....linakufanya wewe ndio wa kutatua shida yote...tena umefanya vizuri ili apate akili nyingine ya kupatia elfu mbili ya kujazia. Kuna miwatu hainaga shukrani...usije ukamsaidia hadi shida ikaisha kabisa...maana utamuharibu mwenzio atakuwa hawazi kitu. Ni maoni yangu tu!
Tena jipu kweli kweli sio kitoto mkuu
 
Hii ipo hata kwenye michango ya harusi. Mtu anataka utume na ya kutolea
Uko nako ni jipu, watu wanalazimisha uchange, bila kuangalia una magumu gani kwa wakati huo, usipotoa unakuwa adui. Mtu harusi inafanyikia sehemu ya mbali na mlipo kwa maana kwamba hautaweza kuhudhuria huko, lakini mchango unaambiwa kuanzia laki, yaani ni shida......
 
Sawa na kumwabia aje achukue amakwambia hana nauli Ha ha haa
 
Hata kama ni mkopo sasa hivi natuma kamili. Watu kama watatu hivi nilishawatumia na hela ya kutolea lakini cha kushangaza wakati wa kurudisha hawakutuma hela ya kutolea.
 
Hata kama ni mkopo sasa hivi natuma kamili. Watu kama watatu hivi nilishawatumia na hela ya kutolea lakini cha kushangaza wakati wa kurudisha hawakutuma hela ya kutolea.

Kwanza hata ukituma pesa kamili, tayari kuna gharama ya kutuma pesa unakatwa wewe. Hata siku akirudisha kiasi ulichomtumia hiyo pesa ni hasara kwako.
Sema watu tuna ubinafsi sana, hatuthamini fadhila kabisa, tena usipokua makini wema utakuweka matatani.
 
Huko ni kukoswa shukrani, yaani huyo ata kurudisha ni bahati
....Hii inanikumbusha unakutana na mshkaji yuko vibaya unachomoa pochi na kumkatia uchache kidogo jamaa anapokea na kuanza kuzihesabu kwanza mbele yako.
 
Ni vema ukamtumia na ya kutolea ili apate kile kiasi alichokuomba. Huwezi jua leo wewe kesho yeye. Kuna wakati nikiwa pale kwenye branch ya Tritel kwa mwanamboka alikuja dada mmoja ambae alikuwa na tatizo la hela ampeleke mtoto wake hospitali alikuja kuuza simu yake. Bahati nzuri alinikuta na tulikuwa tunajuana siku za nyuma sana. Ila hakujua kama angenikuta pale. Nilimsaidia hiyo hela bila yeye kuuza simu yake. Alifurahi sana na alienda zake. Miaka ikaenda na pale kwenye ofisi niliachishwa. Nikawa na hali mbaya sana ya kifedha. Nikaja kukutana na yule dada niliemsaidia akaniambia Vodacom inafunguliwa tanzania na alinisaidia kupata kazi.
 
Back
Top Bottom