Hivi ni nini maana ya "kauli na matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani ktk kipindi cha uchaguzi"?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,349
6,476
Kuna askofu huko Mbeya wa kanisa moja amewataka viongozi wa siasa wasitoe 'kauli na matamko yanayoashiria uvunjifu wa amani katika kipindi hiki cha uchaguzi', na viongozi watokane na "haki ya kidemokrasia".

Source: ITV :: Viongozi Wa Dini Wawataka Wanasiasa Nchini Kuacha Kutoa Matamko Yanayoashiria Uvunjifu Wa Amanimbeya

Maswali: 1. kauli au tamko linaloashiria kuvunjika kwa amani ndio linakuwaje? Je, kusema ukweli ndio kiashiria cha uvunjifu wa amani? 2. Je, hakuna viongozi wa serikali hasa wa vyombo vya ulinzi na usalama wanaotoa kauli na matamko ya uvunjifu wa amani? 3. je, matendo ya vyombo vya usalama na ulinzi kuzuia maandamano, na kupiga watu mabomu ya machozi sio tatizo kwa amani? 4. je kwa viongozi kusema ushindi ni lazima sio dalili za kuvuruga amani? 5. Je, matamko na kauli za kudumisha amani ndio zinakuwaje?

Kwa ujumla je, hii ni mbinu ya kuwatisha wananchi?
 
Back
Top Bottom