Hivi ni lini raisi alitangaza kuvunja baraza la mawaziri?

Insabhunsa Gusa

Senior Member
May 13, 2011
109
88
Wana jf,

Naomba mnisaidie hapa..nijuacho ni kwamba raisi akivunja baraza, hutangazwa na kuwa gazzeted!! Katika kipindi chote hiki cha vuguvugu la baraza jipya, sijawahi sikia tangazo rasmi likisema raisi kalivunja baraza na kwamba ataliunda upya!! Na kama hakulivunja..itakuwaje kwa wale mawaziri ambao hawajabadilishwa wizara zao kama John Pombe na Bernad Membe, wataapishwa kwa sababu zipi ili hali wao wanaendelea na wizara zao na kwamba baraza halikuvunjwa??!!!! Naipenda Tanzania yangu!!!!!!!!
 
Rais hajavunja baraza la mawaziri, amelifanyia marekebisho. Kulivunja baraza ungeona na PM yuko chali. Alichofanya ni kuzibaziba nyufa hapa na pale kwa maelekezo ya CC ya CCM.
 
Rais hajavunja baraza la mawaziri, amelifanyia marekebisho. Kulivunja baraza ungeona na PM yuko chali. Alichofanya ni kuzibaziba nyufa hapa na pale kwa maelekezo ya CC ya CCM.

Sawa, Kama hivyo ndivyo...Kuna haja ya kuwaapisha John Pombe na Bernad Membe na wengine ambao hiyo re shuffle haijawagusa? Kwa tafsiri yangu ni kuwa raisi ameridhishwa na utendaji kazi wao ndo maana hakuwabadilisha!
 
Amefanaya reshufle hajavunja baraza.

Sawa, Kama hivyo ndivyo...Kuna haja ya kuwaapisha John Pombe na Bernad Membe na wengine ambao hiyo re shuffle haijawagusa? Kwa tafsiri yangu ni kuwa raisi ameridhishwa na utendaji kazi wao ndo maana hakuwabadilisha!
 
Mh. ninachijua mimi hawa jamaa walisha Apa na akiwaapisha tena itakuwa mambo basi,,
Mimi hofu yangu kuu ni Hawa walioteuliwa kuwa Wabunge Bila Kuapishwa kwenye kikao cha Bunge
wanateuliwa kuwa Mawaziri, Hapa kwenye Ibara ya 66 hadi ya 68 nimesoma kwa makini sana
Raisi amekenda kinyume na katiba,, Kwa maana hiyo inawezekana Raisi akawa amevunja katiba..
 
Mmmh kaazi ipo humu ndani; Rais JK bana alilivunja baraza la mawaziri pale alipojiudhuru EL ktk nafasi ya uwaziri Mkuu lkn hii ya hivi punde ilikua ni marekebisho tu ya baraza la Mawaziri.
 
Wanaapishwa wale wapya tu na wale ambao wamebadilishiwa wizara. Magufuli na Membe hawaapishwi leo.

umetoa hoja yenye mashiko bahati mbaya hakuna aliyekujibu, yaani hawajakuelewa. hoja ni kwamba kuna haja gani ya kuapisha waziri ambaye anaendelea na kazi yake ambaye alisha apa siku alipochaguliwa?
 
Mh. ninachijua mimi hawa jamaa walisha Apa na akiwaapisha tena itakuwa mambo basi,,
Mimi hofu yangu kuu ni Hawa walioteuliwa kuwa Wabunge Bila Kuapishwa kwenye kikao cha Bunge
wanateuliwa kuwa Mawaziri, Hapa kwenye Ibara ya 66 hadi ya 68 nimesoma kwa makini sana
Raisi amekenda kinyume na katiba,, Kwa maana hiyo inawezekana Raisi akawa amevunja katiba..

Soma na Ibara ya 56 itakupa muelekeo; alafu weka wazi ni kifungu gani cha Katiba Rais amekivunja?
 
Back
Top Bottom