Hivi ni kweli wanawake uwezo wenu wa kufikiri ni mdogo kulinganisha na wanaume?

bigmind

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
12,457
12,682
Binafsi nakiri kupitia kipindi kigumu kupita maelezo kusema kweli.

Iko hivi umri wangu unaniruhusu kabisa kupata mwenza au kuwa na mke kabisa au kama kusema nakaribia kuchelewa yaani kuanza kusemwa vipi mbona huleti mwenzio home tukamwona.

Shida kubwa ni kuwa nimekuwa nikianzisha mahusiano na wadada tofauti tofauti nikiwa na lengo moja tu ili tuwe mke&mume au wenza shida inaibuka hivi kila mwanamke ninae ingia naye kwenye mahusiano ni wiki moja tu ananichosha kwa vitendo na vitimbwi vyake.

Huwa nawaona wanawake kama watu fulani wenye uwezo mdogo wa kufikiri nikimpima kwa vitu vidogo naona kama ni kimeo kisha natamani tuachane maana huwa naona kama anakero nyingi na kufikiri kwake ni duni.

Kitu kingine napenda mwanamke wa kunichallenge katika kujenga hoja na kutafuta masuluhisho ya maisha maana najua akiwa hivyo huwa inanisaidia kufikiri zaidi na zaidi kama kiushindani fulani sasa dada zangu kila ninaye angukia naona kama kimeo (small brain) tu.

Nakiri kuwa na mahusiano na wadada wengi mno ata idadi siikumbuki kusema kweli ingawa siyo mwepesi kufanya mapenzi na mdada kirahisi ila sasa mwisho nimechoka mpaka naanza kuona labda hakuna mdada wa type yangu.

Ushauri mimi nina tatizo au ni mtazamo wangu au kweli wadada ni small brain make naelekea kukata tamaa na hawa viumbe.

Natamani kumpata mdada ambaye ni bigbrain awe MENTOR wangu nami pia MENTOR wake. Sikwamba natangaza ila kiukweli nahitaji mdada mwenye POWERFUL MIND alipo ajitokeze, kama haujiwezi/jitoshelezi please don't try this please!
 
Wapo wanaume ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri, kama ambavyo wapo wanawake wenye uwezo mdogo pia wa kufikiri. Ila point ya msingi sio wote. Wapo wanawake ambao wana uwezo mkubwa sana wa kufkiri, na ukisimamishwa nao ili mshindane kujenga hoja huchomoki hata ufanyaje
 
pole na hongera kwa kuwa na idadi kubwa ya wanawake .. kwanza weka akilini hakuna binadamu mkamilifu .. namna yako wewe ya kuchambua mambo na kuona mambo ni tofauti na watu wengine so kwa mantiki hiyo jua hutafuti mkamilifu ila unatafuta wa kuziba mapungufu yako na wewe uzibe yake pia ili muende sawa............. kwanye mahusiano hakuna mambo ya big brain au small brain.? sababu hutafuti business partner ila unatafuta msaidizi.. acha kuweka vigezo ambavyo havipo mbele kwa mafano ndani ya mwezi huwezi nitongoza badala ya kula bata na wewe nianze kukwambia tufungue biashara kwanza mawazo ni mengi mmh huyu mtu tunafuture gani naye? je kama nitashindwa kuendana na madhaifu yake inabidi nimuache itakuwaje ? at list ungekuwa unakaa na demu mwaka mmoja halafu ukaona hana mchango kwako hapo naelewa ... ila umenitongoza ndani ya wiki nianze ohhhhhhh tufungue duka ili kitokee nini? hapana chalii UNAMATATIZO NA MAPUNGUFU MAKUBWA WEWE NA WALA SI HAO MADEMU KABISA...............
ingia kwenye uchumba oa uone kama hutapata challenge utazipata mpaka ukimbie mwenyewe......
 
Wapo wanaume ambao wana uwezo mdogo sana wa kufikiri, kama ambavyo wapo wanawake wenye uwezo mdogo pia wa kufikiri. Ila point ya msingi sio wote. Wapo wanawake ambao wana uwezo mkubwa sana wa kufkiri, na ukisimamishwa nao ili mshindane kujenga hoja huchomoki hata ufanyaje
Lakini si rahisi kuwajua ndani ya muda mfupi kama wa mleta mada wanawake huwa tunatabia ya kuficha mambo
 
Ndio maana tulipewa jukumu la kuwaongoza na kuishi nao kwa akili chukua tu jinsi siku zitakavyokuwa zinaenda kwenye ndoa ndivyo atakavyokuwa anabadilika hata kimawazo
 
Mkuu mimi nina wasiwasi na wewe , unahitaji mwenye uelewa mkubwa , je , wewe umejichunguza uelewa wako kwanza huenda wewe ni tatizo .
Hivyo vitendo vyao vinavyokuchosha baada ya wiki ni vipi ?
 
Mkuu mimi nina wasiwasi na wewe , unahitaji mwenye uelewa mkubwa , je , wewe umejichunguza uelewa wako kwanza huenda wewe ni tatizo .
Hivyo vitendo vyao vinavyokuchosha baada ya wiki ni vipi ?
wakati ndani ya wiki ni mapenzi moto moto hata swala la uchumi hapo uwazi.. anamapenzi ya kibabe huyu hahahaha
 
Maana yake tayari una mawazo hasi juu ya wanawake,nafikiri huo uwezo mdogo utakuwa umeuona pia kwa nduguzo wa kike ndio maana umekata tamaa na wanawake kwa kigezo cha akili ndogo.Nafikiri unakutana na wanaofanana na wewe.
Jamani! Sielewi km niko sahahi au wrong ila nahitaji kushare uzoefu wenu wadada na wakaka.
 
Usiishie kuwachunguza wadada uwezo wao wa akili pia jichunguze nawe uwezo wako wa akili...usikute wewe ndo mwenye uwezo mdogo wa akili kuweza kuishi nao

Mwanaume unatembea na wanawake wengi unashindwa kumpata mmoja wa afadhari kidogo tena mpaka unashindwa kujua idadi tena katika ulimwengu huu wa magonjwa yasiyo na tiba
 
Back
Top Bottom