Hivi ni kweli wamasai hawali samaki?

tilmikha

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
496
604
Habari zenu!
Naomba mwenye ufahamu juu ya mambo haya niliyoyashuhudia kwa watu kabila la Wamasai anipatie majibu yake.
1)Je kwanini hawakubali kuengezewa damu wakati mmoja wao anapokua na upungufu wa damu.?!
Iikua mnamo mwaka wa 2015 majira ya saa 10:35 jioni hafla palizuka mtafaruku katika chumba kikubwa cha operations wakati mmgonjwa wa kike wa kabila la kimasai alipotaka kufanyiwa upasuaji wa tumbo (laparatomy), ila baada ya majibu kuja kutoka maabara iligundulika kuwa alikua na upungufu wa damu hivo angehitaji kuchangiwa damu wakati was zoezi la upasuaji likiendelea.Cha ajabu watu. wa karibu na mgonjwa walikataa kata kata mgonjwa wao kuongezewa damu.Baada ya mjadala mkubwa akafika kiongozi wa hawa wamasai nae pia alikua mzito kukubali mgonjwa wao kuekewa damu mpaka walipotishiwa polisi ndio wakakubali.Je ni kwanini wamasai hawakubali kuchangiwa damu?
2) KUTOKULA SAMAKI
Hili nalo liliniweka kinywa wazi na ndio Mara yangu ya kwanza kulisikia Leo, nilikua mkahawani mda sio mrefu na orodha ya vyakula ilikua kama ifuatavyo:
A-wali
B)-Supu nyama
C)-Ugali
D)-Chips
Baada ya kumuuliza mama mpikaji ni chakula gani kilichokua tayari akaniambia Ugali, nikamuuliza nafaham fika wenyeji wa hii sehemu sio walaji wa Ugali je wateja wenu ni wakina nani? Akaniambia ni wamasai sasa nikauliza ni mboga gani wanatumia pamoja na huo Ugali nikajibiwa nyama na mboga za majani kwani wamasai hawali Samaki. Nikamuuliza sababu ambayo inapelekea wasile samaki akaniambia hajui.
Je ni kweli wamasai hawali samaki na kama kweli hawali ni kwasababu gani?
3) Naomba kufahamishwa ni imani gani walio nayo wamasai baada ya MTU kufa?
Tulikua katika mazishi mwaka huu 2019 , eneo ambalo ni mita chache kutoka ufukwe wa bahari, aliefariki ni mtu wa imani ya kiislam ,wakati mazishi yakiendelea walikuja wamasai wapatao 10 wakashiriki huku nyuso zao zilionekana zimejawa mawazo mazito juu ya lile tukio lililokua likiendelea , ukisoma sura lazma utagundua ni wazi wanaamini kitu tofauti kabisa na wanavyoamini watu wengine au inawezekana na wao wanaamini kama tunavyoamini Mimi na wewe ila kutokana na kujali kwao labda ndio mana wameguswa sana na lile tukio, kwani waliacha kazi zao na kuja kushiriki katika ule msiba hadi kwisha na aliekufa hawamjui ndewe wala sikio.Je wamasai wanaimani tofauti na watu wengine, simaanishi kuwa wamasai ni Aliens hapana ila naona ni watu pekee walio kua sticky na mila pamoja na tamaduni zao.
Lipo na jengine ila nimehisi ukakasi kuliuliza kwani sijui wadau mtalichukuliaje pia sina hakika kama linaendana na rules pamoja na regulations za Jf. Napenda kuchukua fursa hii kutoa pole kwa wafiwa wa Ajali ya moto sambamba na kuwaombea kupona haraka wale walioko Hospitals,mwenye ufahamu naomaba anifahamishe.
 
Hiyo ilikuwa zamani wakati wanyama walikuwa wengi na malisho mengi, wamasai sasa wanakula kila kitu, maisha yamebana sana hakuna uwezo wa kuchagua chakula. Siku hizi sio tu ni wafugaji bali wanalima na wanafanya biashara pia.
 
Ni imani tu potofu zisizo na mashiko kisayansi.
Niliwahi ona mmasai akitoka nje ya hoteli kisa tu aliona samaki kwenye sahani ya jirani yake mezani.
 
Ahsante Sana kwa majibu na maelezo wakuu ila naona majibu kama sijapatiwa? Ila nimefaidika kuwa inawezekana imani potofu pia kutokana mfumo wa maisha ya ufugaji hapo zamani.ila vipi kuhusu suala la kuchangiwa damu?
 
we wanakula..ila ambacho nna uhakika nacho kua hawapendi ni chupi.!bwana wamasai wana alergy na kuvaa chupi bwana.
 
Wamasai samaki hawali hata kuku ni wachache sana wanakula...istoshe bado mila zao kali inatokana sehemu na sehemu simanjiro bdo wana mila kali
 
Hawali hata nyama ya wanyama pori usishangae sana,,kama mila zetu sisi hatuli panya wala sungura
 
Hiyo ilikuwa zamani wakati wanyama walikuwa wengi na malisho mengi, wamasai sasa wanakula kila kitu, maisha yamebana sana hakuna uwezo wa kuchagua chakula. Siku hizi sio tu ni wafugaji bali wanalima na wanafanya biashara pia.
Siku hizi wanakula mpaka mlenda nini samaki na wadada wa kimaasai wanasuka na kuweka nywele dawa wakati enzi za mwaalimu ni kama kukutana na chatu feri
 
Siku hizi wanakula mpaka mlenda nini samaki na wadada wa kimaasai wanasuka na kuweka nywele dawa wakati enzi za mwaalimu ni kama kukutana na chatu feri
Ila nataka kufaham sababu za kuchukia hivo vitu unajua ile kesi ya kukataa kuchangia damu ilikaribia mgonjwa apoteze maisha
 
Back
Top Bottom