Hivi ni kweli tuna polisi wazuri kihivyo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli tuna polisi wazuri kihivyo?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kireka1980, Nov 30, 2009.

 1. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Juzi nimesikia kwenye habari polisi wamewaua majambazi 6 wenye silaha nzito za kivita na mabomu, kinachonishangaza hkuna polisi hata mmoja aliyejeruhiwa (siombei wajeruhiwe), kwenye mpambano huo.
  mm nahisi hawa jamaa walikamatwa na kupigwa risasi. hii imetokea kigoma
   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Hebu tupe data last, week ilikuwa Biharamulo leo kigoma halafu mambo yote yanafukiwa kwenye carpet jamani mbona balaa, nola, Tume ya haki za binadamu, kituo cha sheria na haki za binadamu mbona mko kimya je ninyi mnaona hii ni sawa kweli????????
   
 3. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kwani una uchungu jambazi akishikwa akauwawa! Je ulishawahi kuvamiwa na majambazi wenye silaha za moto ? kama bado usiombee ikutokee
   
 4. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  Aisee hizo habari ni za kweli, jamaa (Polisi) wako makini sana, na unajua wapo makini kwa sababu nadhani ni miezi miwili au mitatu imepita kuna Askari mmoja aliuwawa maeneo ya huko Chato/Biharamulo na jamaa wakaondoka na Silaha ya askari (SMG) ikiwa na risasi nyingi, sasa polisi wapo kwenye operation maalumu
   
 5. Kireka1980

  Kireka1980 JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2009
  Joined: Mar 18, 2008
  Messages: 304
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  ISSUE ni kwamba majambazi sita wenye mabomu ya kurusha kwa mkono, na bunduki za kivitu hata polisi mmoja hajajeruhiwa eh "mapambano ya kurushiana risasi"!
   
 6. Mlango wa gunia

  Mlango wa gunia Senior Member

  #6
  Nov 30, 2009
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mkuu kireka hili linawezekana kabisa kuwa waliuawa kwenye scene bila polisi kujeruhiwa kwani hata kama una silaha nzuri kiasi gani usipoitumia/kuifyatua haitakusaidia/haitafyatuka yenyewe.
  kwa hapa nyumbani mara nyingi polisi huwa wanakuwa na info,na hivyo hupata muda wa kufanya appreciation yao na kuweka ambush kabla ya hao majambazi kufika mahali wanapokwenda kushambulia/kufanya ujambazi.Na majambazi wakiingia kwenye target (ambush) basi fire supremacy aka mvua ya risasi ndio inayomaliza mchezo kaka, kumchinja kobe kwahitaji timing.
  Kama ni majambazi na sio watu innocent basi kwa kweli hata wakiwakamata wakiwa hai si watanzania wala polisi wetu tunawahitaji. Majambazi acha wafanyiwe finishing mkuu,hizo ndio rafu za kwenye game.Do or die.wamezidi kutuchapa na wamefanya Tz shamba la bibi,kila siku majambazi toka kenya,kongo,burundi nk wanapeta tuu,huku uchumi wetu una collapse
   
 7. M

  Magezi JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nashangaa mtu anahoji jambazi kuuawa? Acha wauawe tena bahati mbaya hatuna askari wazuri wengi, hao hao wachache wanajitahidi lakini na uovu umeongezeka sana.

  Kwanza tuwapongeze polisi wetu kwa kazi nzuri na tuwasaidie ili wafanya makubwa.
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  una uhakika gani kama ni majambazi, ndio maana kuna rule of law ukiacha polisi auwe jambazi kwa upande mmoja ina maanakwa upande wa pili kama wewe unamdai mtu hutahitaji kwenda mahakamani kutaka hukumu utaenda moja kwa moja nyumbani kwake na kuchukua mali zake, hivyo hivyo kama mpangaji wako hajalipa kodi unaweza kuchukua mali zake bila kufuata utaratibu.

  Nchi yoyote lazima iwe na utaratibu fulani, hata mtuhumiwa wa ujambazi ana haki zake nyingi tu hatakiwi kuuwawa elewa hilo ndugu yangu. Vinginevyo itakuwa udikteta na haitafika miezi sita utaanza kulalamika kuwa polisi wanatumaliza, kama utakuwa hai that is.

  Nchi yoyote iliyostaarabika lazima kuwe na rule of law.
   
 9. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  utavuna ulicho panda......majambazi wamevuna walicho panda kuuliza kwa nini polisi hawajajeruhiwa ni ishu nyingine.
  kwanza polisi wana mafunzo zaidi ya majambazi
  pili polisi kupigwa risasi kama ambavyo tumekuwa tukisikia ni uzembe
  tatu polisi wana taimingi nzuri zaidi ya hao majambazi.
  mlitaka wauwawe?
   
 10. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #10
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Wewe ulitaka wajeruhiwe? Wamepitia mafunzo ya kujihami hao hawako lelemama
   
 11. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  nafikiri sheria ya jambazi kuuwawa ni muhimu sana kuwepo! kama china ukiwa jambazi la ufisadi kitanzi! Sioni sababu ya jambazi kuishi
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Dec 1, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  una uhakika gani kuwa ni majambazi?????

  KAMA WANATIMING NZURI KWA NINI WASIWASHIKE BILA KUWAUWA???

  POLISI KUUWA RAIA NI UUAJI HAKUNA SEHEMU AMBAYO POLISI ANARUHUSIWA KUUWA. ELEWENI HII KITU.
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Dec 1, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  kama unavyoona juu hiyo sheria haipo, na hata kama ipo lazima chombo kimoja kitoe tamko kuwa mtu fulani ni jambazi na ndipo huyo mtu anatakiwa auwawe. Haiwezekani RCO tu anaamua uwa watu ni majambazi kisa sura zao mbaya, au kabila, au wakimbizi au wana macho mekundu. tusiruhusu.

  Sasa kwa sababu sheria hiyo haipo hao polisi ni wauaji na washitakiwe mahakamani kwa kosa mauaji.
   
Loading...