Hivi ni kweli ni kosa letu watanzania??!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli ni kosa letu watanzania??!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sajenti, Dec 28, 2009.

 1. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ni muda mrefu sasa kumekuwa na manung'uniko kutoka kwa watu mbali mbali hapa nchini na hata hivi karibuni wanasiasa waandamizi walidiriki kusema wazi kuwa uongozi wa raisi kikwete umekuwa goi goi. Mengi yamezungumzwa na yanaendelea kuzungumzwa. Kwa upande wangu naumia roho kuwa mwaka 2005 wakati wa uchaguzi mkuu nilitumia takribani saa 2 kukaa kwenye foleni kusubiri kupiga kura. Na nakiri nilimpa kura yangu JK kwa matumaini kuwa nachangua kiongozi anayejua shida zetu watanzania na hivyo anaweza kuyatafutia ufumbuzi matatizo yetu. Kwa mtazamo wangu mimi na watanzania wenzangu wengi tulikosea kumpa kura ya ndio JK!

  Napata picha kuwa umefika wakati nchi inakosa kilanja wa kusimama na kukemea uvundo unaondelea. Ufisadi mwigi uliotokea na unaondelea kutokea huenda ukatufikisha mahali Tanzania ikawa shamba la bibi kila mtu anajichukulia awezavyo bila shaka yoyote.

  Naelewa wazi humu ndani ya JF kuna watu watakaokuwa tayari kuanza malumbano yasiokuwa ya lazima ili mradi kutetea uozo wa serikali hii ya awamu ya 4. Nilifurahi sana niliposikia kuwa polisi walipiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika Dar eti kumpongeza JK na serikali yake na pia kuwashutumu wale waliomsema JK na serikali yake kwa utendaji mbovu. Huu unafiki wetu watanzania ndio hutuletea vilio na kusaga meno kila wakati. Naomba niseme wazi kuwa endapo nitakuwa hai mwezi Oktoba 2010 wakati wa uchaguzi JK hatopata kura yangu. Mtadai kuwa hata nisipompa kura mimi wengine watampa, lakini nina imani na mwenyezi mungu analiona hili kuwa wengi wataamka usingizini na kuwakomboa watu na hili jinamizi lililoikumba nchi yetu.Kuna watakaokwazika na hiki nilichoandika lakini ndio ukweli wenyewe.Ujinga wakati wa kwenda sio kurudi!!
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Wangapi kati ya watanzania wote wanajua madai yako kwamba JK na uongozi wa awamu ya nne ni goi goi? labda 20% tu ndiyo wanajua na hawa wapo mijini - na kati ya hao wapo unaowaita Wanafiki. Asilimia iliyobaki yaani 80% hawajui chochote kuhusu uongozi na hatma ya nchi hii na wanaishi vijijini ambako hakuna JF, Gazeti na TV, wana shida lukuki sasa unategemea nini kuhusu uchaguzi ujao? na mbaya zaidi shida zao zote hawajui zinatokana na viongozi waliowachagua wenyewe.

  Hii ndiyo asilimia 80% ya wananchi hawana uelewa wa kuchambua mambo, wanasikiliza nani kasema nini na katoka chama gani, hawa ndiyo wanaochagua Rais, Wabunge na Madiwani.

  Amini nakuambia tegemea mabadiliko kidogo sana ya uchaguzi 2010, lakini CCM lazima ishinde tu ingawa hata mimi binafsi nisingependa iwe hivyo.

  Hii asilimia 80% ya wananchi mpaka itakapoelewa uchambuzi wa siasa ndiyo tunaweza kufikia mapinduzi ya kweli, kwa sasa tegemea viti 90% vya ubunge toka CCM na Rais wao hiyo nakuambia ukweli, haijalishi wame perfom au laa.

  Cha msingi ni kuomba mwenyezi mungu tu awaondoe ndani ya CCM mafisadi wote sababu CCM watatuongoza tena term inayokuja, sisi hatutaweza kuwaondoa kwa sanduku la kura.

  Kwa bahati nzuri 2005 mimi sikupiga kura kumchagua rais na wabunge wenu, ila wakati huo nilikuwa kijijini niliyoyaona yanakatisha tamaa na ndiyo maana nakwambia 2010 itakuwa yale yale na wao wanajua hilo.

  Nitawakera wengi lakini ukweli inabidi tuseme tu, sitegemei mabadiliko yoyote uchaguzi ujao, ni yale yale na tutegemee maumivu ya kimaisha kwa miaka mingine mitano ijayo hadi hapo wananchi wa vijijini (80%) watakapokuwa na uelewa juu ya elimu ya uraia, na kutambua kuwa kofia, fulana, pilau, ngoma, chumvi na pesa haviwezi kununua haki yako ya uchaguzi.

  Lakini nani alale njaa wakati kuna pilau la kampeni lipo pale viwanja vya CCM? nani asikubali familia yake yote ichague CCM wakati kapewa bahasha nono tena na kada anayemjua? tena jirani yake wa miaka anayemsaidia kwa shida zote? kampeni za nyumba kwa nyumba ni hatari sana zinatafuna demokrasia.

  Aliyeishi kijijini atanielewa vizuri...

  We still have a long way to go....
   
 3. e

  echonza Senior Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu sasa unaonaje tukianzisha taasisi ya kuelimisha wapiga kura juu ya haki zao za msingi wanazotakiwa kuzipata kutoka kwa viongozi wanaowachagua? Najua tutakuwa tumechelewa kufanya hivyo kwa sasa kwa ajili ya uchaguzi wa 2010, lakini tutafanya hivyo kwa kuwaandaa sasa kuwa na fikra zilizokomaa na kujaa kuwezesha na kujitambua kuwa kama wanadamu haki zao ni a to z. Hivyo, chaguzi zitakazofuata baada ya huo wa 2010 basi 80% ya wapiga kura aghalabu kiasi kikubwa chao itakuwa na uelewa muhimu katika kuamua nani achaguliwe kuwa kiongozi wao!!!
   
 4. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,364
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Hilo sasa ndio neno nililokuwa nikilisubiri toka vinywani mwa watanzania!!
   
 5. S

  Sabi Sanda JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 412
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kazi ianze. Redio la TV zitumike kila siku kwa ajili ya Elimu ya Uraia iliyo sahihi. Muswada wa BUNGE ni muhimu ili kuwa na sheria maalum ambayo itawezesha kutengwa fedha za kutosha katika bajeti ya Serikali kila Mwaka wa fedha kwa ajili ya elimu maalum ya URAIA kwa Watanzania.
   
 6. TingTing

  TingTing Member

  #6
  Dec 29, 2009
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 93
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swali ni...Je, wewe binafsi kiongozi elnino unafanya nini hili kuweza kusaidia uenezaji wa elimu kwa wadau wote hapa Tanzania hususan wale wa vijijini?

  A five year plan would be a failure but a 10-15years plan would luk 2 b a gud plot i suppose.
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu hiyo si kazi rahisi unavyofikiria, ni kazi ngumu mno. kwa mfano tuamue tuanzisha vipeperushi tuviite Jamii Forum, tuweke yote mazuri tunayo discuss hapa tupale wana JF wanaoweza ku edit then tuvitume kila wilaya, kata, vijiji hadi vitongoji.

  Vikwazo vitakuja watasema sisi wachochezi, wameturuhusu tu tuongee hapa kwa sababu ni asilimia 5 tu ya watanzania wanatumia hii Forum kwa hiyo hawajali, lakini forum hii ikianza kuwafikia wote 95% itakuwa na vikwazo vingi sana.

  Anyway tusikate tamaa, tuongee na JF founders, tupate editors then discusstion zetu muhimu ziwe zinachapishwa zinasambazwa kote nchini kama vipeperushi kila mwezi.

  hilo wazo ni langu, just to start with.......
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Dec 29, 2009
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Nani apitishe sheria ya kumtafuna mwenyewe, hilo bunge ni la nani? hujui kwamba wananchi wakielewa haki zao ulaji utapungua? vuguvugu la ukombozi halitaanzia kwa watawala kamwe, litaanzia kwetu sisi wanyonge tunaoonewa.
   
Loading...