Hivi ni kweli miti hujongea/kuwasiliana na kuna aina fulani ya miti ina miujiza?

Nimeona mti mmoja Inama nijichumie
1-40.jpg
 
Ni kweli usemayo, miti mingine ina maajabu yake,

Mf: Mti wa Muashoki, hii miti watu wanaipanda tu ila ni mti mibaya kabisa,

Mf: Mti wa 'uzazi wa mpango' huu nao una mabalaa yake mengi tu,

Kiufupi miti kama vilivyo viumbe hai vingine vina mambo yake na maajabu yake.
Nimeamini kuwa hii miti mingine ni nuksi, pine tree (miashoki) inateketeza Israel
 
niliwahi kusikia miti ya mikungu inapendwa na majini, pia niliwahi kusikia hivyo kwa maua ya jasmin ile inayonukia...

mwingne alizidi hadi kusema mti wa mbaazi ni kiboko ya wachawi....

yote hayo nimeyachukulia ni hadidhi tu zsizo na ukweli.
 
Habari wakuu. Hii thread nimeipenda sana na nimejikuta nakumbuka research iliyofanywa nadhani uki google utaipata. Hii research ni kwamba waliandaa vyumba viwili na kuweka aina moja ya musiki( hard rock) kwenye chumba kimoja na soft music kwenye chumba kingine. Baada ya hapo wakaingiza mimea humo na kuyahudumia kwa kama wiki 1 kama sijakosea. Basi mimea yote iliyokuwa kwenye chumba cha musiki wa hard rock..ilikufa na mimea iliyokuwa kwenye soft music room ikastawi balaa.
This was scary sijawahi sahau.
Basi kwa ukweli conclusion ni kwamba mimea huwa na hisia na wanatusikiliza. So up to you.
 
kwa ambao kiasi kikubwa cha maisha yetu imekuwa ni porini tunadhani na pia tunaimani kuwa mitimiti..ina uhai na ni viumbe na pia kama ilivyo kwa viumbe wengine miti hujikinga na maadui kwa kutoa homoni fulani ambayo ni ita act kama defensive mechanism, miti inaweza kujika kwa kutokana na sumu, au harufu, au miba au hali ya umbo lake lilivyo au hata mahali unapoota.

miti kama ilivyo viumbe hai vingine hutafuta mahitaji muhimu ili kukua na kupata afya...

miti kama ilivyo kwa viumbe hai vingine hujongea, kwa kukuwa kwenda juu au kwa kutambaa kwa ajili ya kutafuta mahitaji yake...
miti huzaliana kama vinavyozaliana viumbe vingine na kwa namna hiyo miti ina kuwa na familia...na hivyo hushirikiana na kusaidiana....
miti pia ina tabia kama viumbe vingine...
miti ni michumi..kama viumbe vingine vilivyo...mfano miti sawa na mimea mingine huwa inauwezo wa kutunza mazingira kwa matumizi ya baadae , mfano miti fulani ikiota sehemu isiyo na maji inaweza kukusanya na kutunza maji kwa ajili ya vizazi vijazyo, au ikitokea kuoteshwa kwenye tindiga inaweza kuifanya sehemu ile ikawa ya kawaida kwa unyevu unyevu, mifano hio ipo dhairi tulipo...

KUTOKANA NA SIFA TAJWA HAPO JUU, BASI MITI IKITOKEA KUTUMIKA VIZURI NA BINADAMU INAWEZA KUWA CHACHU YA UTAFITI ENDELEVU WA MAMBO MENGI KWA MANUFAA YA WALIMWENGU.
MFANO: kutambua madini yalipo na vitu vingine vya thamani...
kutambua maadui walipojificha au kuwa sehemu ya kujikinga na maadui...
makazi ya viumbe vya ajabu...
kujua au utabiri wa hali ya hewa..
kutengenezea dawa mbalimbali na virutubisho vya miili yetu.
kutengenzea sumu...

*baadae naondoka naona wife kaamka na huu muashoki ulioota hapo nje najua kuna timbwili lina kuja*
 
Ni kweli usemayo, miti mingine ina maajabu yake,

Mf: Mti wa Muashoki, hii miti watu wanaipanda tu ila ni mti mibaya kabisa,

Mf: Mti wa 'uzazi wa mpango' huu nao una mabalaa yake mengi tu,

Kiufupi miti kama vilivyo viumbe hai vingine vina mambo yake na maajabu yake.
Walituambiaga mti wa uzazi wa mpango ni mmbaya lakini sina taarifa ya mti wa Miashoki kama na yenyewe ni mibaya
Ubaya wa muashoki anijuze
 
Halafu kuna mmea fulani hivi upo kama vijikamba kamba hivi hupendelea kujiviringisha kwenye miti juu au kwenye nyasi za kawaida chini, huo mmea hauna shina wala mizizi, hata ukae unatafuta shina lake au mizizi yake huoni ilipo, kwa hio chanzo chake unaanza tu! Na utakuta umeshamiri kweli huo mmea wa kijani.
 
Inasemekana kuna mti maarufu huko Gilberton, Alabama Marekani. Mwanamke mwenye jina la Linnie Jenkins alikuwa akilalama anasikia sauti ngeni na vilio zikitoka kwenye mti wa Pecan uliokuwa mbele ya nyumba yake. Jambo hili lilivuta vyombo vya habari, na mwaka 1981 maelfu ya watu walikuja kushuhudia jambo hilo la mti wa ajabu. Na baadaye iligundulikana kwamba nyumba ile ilikuwa imejengwa juu ya makaburi ya zamani ya kihindi, na watu wakaamini vile vilio vilkuwa ni vya wale wafu waliokufa miaka ya huko nyuma.

Ushawahi kusikia "HUNA"? Huna ni falsafa ya kale ya watu wa Hawaii. Wao huamini kwamba kila kitu ni hai, kinawajibika na kina ufahamu. Kwahiyo kila kitu kina roho.

Huna hufundisha kwamba roho huungana hata kama ni za watu au vitu tofauti. Mfano: roho ya binadamu huendana kiukaribu na roho ya binadamu mwenziwe, lakini pia huweza endana na za wanyama kama vile farasi na mbwa.

Huna huamini pia binadamu huendana roho na miti na ndio mana pale tunapoona mti au miti hukatwa huwa tunaguswa kwasababu fulani. Ni kwasababu kuna muungano upo baina yetu. Hata baadhi ya watu pale wanapojisikia kukwazwa, kujisikia vibaya ama kutengwa hupenda kukaa chini ya miti kupumzika. Ama matawini.



Kwa mujibu wa Kerrian Flanagan.
Hapo ya kukaa chini ya mti umenikumbusha long time ago nilikua na tabia nikiwa down naenda coco beach kuna mti flan nilikua napenda kukaa, nawazaaa nikitoka hapo lazima nitoke na solution,
Ajabu ni kua kama siku nikifika nikamkuta mtu yule mtu lazima anyanyuke nibaki peke yangu, hali ile ikaniteka kiasi kwamba nikawa eti naumiss mti wangu naenda kuuona, mmh nikashtuka nikasema kuna siku nitakuja kupotelea kwenye huu mti.

Baada ya kua mkubwa nikakata mguu.
 
Back
Top Bottom