Hivi ni kweli kuwa wanawake huwa hamuamini kuwa waume zenu kuna muda hawana hela?

Sina hela ya kwangu haifanani na ya kwako.
Sina hela yangu inaweza maanisha hela iliyopo ni kwaajili ya dharula pekee.
Wakati wewe unamaanisha ulikuwa unakunywa bia tatu kwa siku sasa unakunywa kachupa kamoja tu.
Au unamaanisha umeshindwa kujaza gari mafuta na hivyo unapanda daladala.

Zipo aina nyingi za kuishiwa. Mkeo inabidi aelewe aina yako ya kuishiwa.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Vipi na wale mawifi wanaomsakama mkeo wakihisi kaka yao anafilisiwa na mkeo?

Wale huwa hawahisigi kama kaka yao haishiwi pesa?
Na mama wakwe pia, hulaumu kuishiwa kwa watoto wao wa kiume kunahusiana na matumizi mengi au ya hovyo ya wake zao.
 
Yes tupo, tena mimi hata bila ya kunambia najua tu maana hela zinazotoka za matumizi unaziona kabisa sio zile umezizoea hivyo hata huulizi unajua tu Mr hana

Yeye ni binaadam kana wengine na najua maisha najua fika kuna kukosa na huwezi mzuia maana hana akaibe au akakabe??
Alafu hili Jina Mr mnalimisuse sometimes. Utasikia nipo na Mr., mara Mr. Kasafiri njoo, oooh Mr. Yupo.
 
Ndugu zangu habarini za mwisho wa wiki,

Leo naombeni walioko kwenye ndoa hasa wanawake wanisaidie jambo moja ambalo nimeliona. Mara kadhaa nimesikia wanawake wakisema kuwa "Mwanaume haishiwi pesa" kitu ambacho kiukweli wanaume wanajua kuwa si kweli. Kuna muda mwanaume unaishiwa hadi mwendo wa kutembea unachange.

Naombeni kujua uhalisia upoje ni baadhi ya wanawake wachache tu ndio huamini hivyo au ndio wote mpo hivyo?
Yaani mwanaume hata akisema hana hela lakini utakuta mwanamke huyuhuyu haamini juu ya hilo

Mawazo yenu na michango yenu ni muhimu kwa ajili jambo hili.

Natanguliza shukrani
Ni mwanamke/mke wa namna hiyo ni yule anayekufanya unakuwa na Maisha ambayo hata ukiishiwa unakopa kwa ajili ya familia. Unaweza kuwa na pesa muda wote Ila pia unakuwa na madeni muda wote. Umeelewa Sasa.
 
Huyo ni mke au hawara? Si mnaishi ndani pamoja, upigiwe au kutumiwa ujumbe kivipi?
Kwani utakuwa unaishi ndani tu hutoki?
Huna safari za kikazi? Huna mbishe mbishe zinazokuweka mbali na familia?
Come on man
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Back
Top Bottom