Hivi ni Kweli kanisa la Gwajima ndo lenye waumini wengi Tanganyika?

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
16,927
13,011
Nasikiliza hii audio iliyowekwa humu, kuna sehemu anasema kanisa lake ndo lina waumini wengi kuliko wote hapa Tanganyika.

Hii INA ukweli au alimaanisha nini mliomwelewa.
 
HaPaNa waauminI wengi ni watoto wa Mama mDogo. Wanaruka hadi Kareeti.halafu suruali kufika kwenye kisigino Kwao Mwikoo. halafu weNgi waNamkaAA KWENYe komwee pia WanapeNda kubishAna na kuteETEA fAce za KijinGa. HalaFu nimekumbuka Wana piga pApucha Nne.

Thank you vereeee much and good bye.
 
Nasikiliza hii audio iliyowekwa humu, kuna sehemu anasema kanisa lake ndo lina waumini wengi kuliko wote hapa Tanganyika.

Hii INA ukweli au alimaanisha nini mliomwelewa.

Deo, hivi hili nalo ni la kulifungulia thread?
Kama Gwajima ndo anaongoza kwa wingi wa waumini hapa nchini, Wakatoliki na Walutheri watasemaje? Zaidi ya Dar, sijapata kusikia Kanisa la Ufufuo na Uzima lina wafuasi mahali pengine
 
kanisa lake ndilo linalokusanya watu wengi kwa pamoja kuliko yote tz. ibada moja kwa pale kawe wanakaa watu zaidi ya 50,000. alfu hamsini ibada moja. ulishawahi kuona kanisa gani jingine linalokuwa na ibada kubwa kama hiyo hapa tz? pia makanisa mengi madogomadogo na yale yanayokua kwa kasi, wamesoma bible schook kwake na wametokea palepale. morogoro ana kanisa, mwanza ana kanisa. ukijumlisha waumini wote tz, kwakweli si wengi kiasi hicho, ila kwa dsm ni wengi sana. hata huko katoliki huwa wanakuja kusali ibada za mwanzo halafu wanakimbia kwenda kusali kwa gwajima.

hata wakatoliki wengi sana ni waumini wa gwajima, huko katoliki wanakuja tu kwaajili ya umoja wa vigango ila wakisali ibada ya kwanza huko kwenu kwenye vikanisa vya watu 2000 wanawahi kawe hadi saa nane mchaana. unaweza kuona kama ana wafuasi wachache lakini chini kwa chini ana wafuasi wengi sana sana.
 
Labda alikuwa ana maana nyingine, hata mimi nimeshangaa.
 
uwelewa ni mdogo kati yenu, amesema hivyo akimaanisha one mass, ndio maana kasema kanisa lake ndio kubwa tanganyika kwa wingi wa waumini ktk ibada moja na akasema wapo zaidi ya elfu 70. sasa mleta mda hukuelewa nn.
 
sawa Gwajima tumekusikia
 
Deo, hivi hili nalo ni la kulifungulia thread?
Kama Gwajima ndo anaongoza kwa wingi wa waumini hapa nchini, Wakatoliki na Walutheri watasemaje? Zaidi ya Dar, sijapata kusikia Kanisa la Ufufuo na Uzima lina wafuasi mahali pengine
wakatoliki hapa nchini ni karibia 10ml. lakini hawana influence yeyote. wakatoliki wengi sana siku hizi wanakimbilia makanisa ya ulokole kwasababu kule kuna maombezi na katoliki hakuna maombezi, utaona mtu amewahi ibada ya kwanza katoliki halafu anatoka haraka anaenda kanisa la kilokole. hivyo hata kama wakatoliki wanaweza kuonekana wengi lakini kiroho si wengi kiasi hicho.

walutheran (kanisa langu la kuzaliwa) ni wengi iringa, kilimanjaro, dsm, bukoba na kwingine. lakini makanisa yao yanakusanya watu wachache sana per ibada. tofauti na makanisa kama ya gwajima, efatha, kakobe full gospel, kina katunzi, peter nyaga na makanisa mengine mengi ya kilokole. walokole kanisa lake likiwa linaingia ibada watu chini ya 5000 anajisikia vibaya. wanapambana wawe na waumini zaidi na zaidi. lakini hayo makanisa kongwe hakuna lenye kuingiza ibada moja watu 4000. niambie kanisa la wapo la lutheran, katoliki au anglican linalobeba ibada moja watu zaidi ya 5000 alfu tano. nitajie tu.
 
uwelewa ni mdogo kati yenu, amesema hivyo akimaanisha one mass, ndio maana kasema kanisa lake ndio kubwa tanganyika kwa wingi wa waumini ktk ibada moja na akasema wapo zaidi ya elfu 70. sasa mleta mda hukuelewa nn.

Sasa si ndo maana nimeuliza?
 
sawa Gwajima tumekusikia
hahaha, usihangaishe akili. mimi wala si gwajima, ila nimeshasani kwa gwajima miaka miwili iliyopita baada ya kuhama dsm nasali kwenye makanisa ya kilokole mengine. originally nilizaliwa lutheran, nikiwa form two nikaokoka nikahamia makanisa ya penstecost hadi leo mtu mzima nimeshasali sana makanis amengi ya walokole na mimi ni mlokole hadi leo na sitaacha. kabla ya hapo nilikuwa simuoni Mungu nilikuwa nasali tu kama sheria lakini baada ya kuokoka namuona Mungu na ninajua nini maana ya ibada.
 
Mmeshajua ukweli, kanisa lake ndilo lenye wafuasi wengi wwingiao ibada kwa wakati mmoja, ana kama 70,000/. niambieni kanisa la Catholic au Lutheran liingizalo ibada moja watu 5000. ni nini hamjaelewa hapo?
 
try to imagine, watu 70,000 ibada moja na kila mtu anatoa sadaka. hahaha, unapata shilingi ngapi? na nyie wakatoliki ambao vikanisa vyenu lililokubwa sana linachukua waumini 2,000 mnachukua sadaka bei gani. hapohapo mnawazushia watumishi wa Mungu kuwa wana hela nyingi mno wanazitoa wapi, hadi mbasha amemzushia kuwa anauza sembe...hahahaha. akili ya kawaida tu hapo hauoni kama vinawiana?
 
Kumbe ishu ni sadaka?
Halafu unaitaje vikanisa?
 
Back
Top Bottom