Hivi Ni Kweli Kabisa TABIA Haina Dawa??.....hebu tujadiliane!!

Mazingira yanachangia bana

Kama umeishi wa watu ambao ni wasafi sana, lazima watakuathiri kiaina
Hebu angalia tu hata wavulana ambao walilelewa na mama mkali, lazima watandika vitanda

Hata wakienda kujitegemea, huwa wanatandika vitanda mara nyingi


Ukarimu ni suala pana zaidi
Lakini hata ukarimu bado unafundishika

Hivi Kongosho UKARIMU unafundishika au ni TABIA ya kuzaliwa nayo??..Na inawezekana mtu akazaliwa na TABIA ya UCHAFU??....
 
Mkuu ahsante kwa maada nzuri,

Najua siyo vema kuuliza swali juu ya swali lakini kuna mjadala kama huu niliwahi kuukuta nikajikuta unaniachia maswali na hapa nisingependa kujichanganya kwanza kabla sijapata mawazo ya wadau hapa juu ya swali kama hili.....

Kuna tofauti gani kati ya "TABIA" na "HULKA" au vyote ni kitu kimoja?

Key word iwe ni "MANTIKI" ... yaani LOGIC

Mwanadamu anweza kusukumwa na misukumo miwili tu!! "Mantiki" au "Hulka"

Honestly speaking? Hulka ni kwa ajili ya wanyama na Mantiki ni kwa ajili ya wanadamu kamili!!

LAKINI mwanadamu anaweza kuamua kusukumwa na Hulka ..Hence the foundation of this discussion!!

MTU anaweza kuendeshwa na TABIA ilijengwa na MANTIKI au ilijengwa na HULKA ...!!
 
TABIA = Mazoea yanayotokana na kurudiarudia hali, mwenendo au matendo

HULKA = Tabia ya mtu, mwenendo wa mtu, maumbile. Pengine huluka.

Kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili sanifu

Na vipi kuhusu SILIKA (SILKA)?
 
Mkuu Azimio Jipya naona umeamua kuingiza kitu kipya kabisa LOGIC....Na unasema ni aidha tu hiari ya mhusika kujijenga kitabia kwa kutumia hulka au mantiki!!....Hivi unaposema LOGIC sio ndo mambo ya REASONING??...Yaani pale mtu anapofanya jambo kwa kuangalia 'impact' ya jambo kwa hadhira yake au yeye mwenyewe...By the way how Logic to me is also LOGIC to you???

.....Honestly speaking? Hulka ni kwa ajili ya wanyama na Mantiki ni kwa ajili ya wanadamu kamili!!LAKINI mwanadamu anaweza kuamua kusukumwa na Hulka ..Hence the foundation of this discussion!! MTU anaweza kuendeshwa na TABIA yenye MANTIKI au yeye HULKA ...!!
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Azimio Jipya naona umeamua kuingiza kitu kipya kabisa LOGIC....Na unasema ni aidha tu hiari ya mhusika kujijenga kitabia kwa kutumia hulka au mantiki!!....Hivi unaposema LOGIC sio ndo mambo ya REASONING??...Yaani pale mtu anapofanya jambo kwa kuangalia 'impact' ya jambo kwa hadhira yake au yeye mwenyewe...By the way how Logic to me is also LOGIC to you???

Nakubaliana na hoja yako kuwa ni HIARI ya muhusika kujijenga kitabia kuotekea minisingi ya Hulka au Mantiki! Lakini nafikiri mziki unaazia hapo ... kwenye tabia za kihulka, naamini tabia zilizojengwa na mantiki hazileti contradiction ... Mfano post ya Kongosho ametoa mfano Mama mkali huwafundisha watoto wa kiume kutandika vitanda ... to me that is logic ... hivi nani haoni kuwa hiyo ni logic? ..mantiki? na it worth kujengwa kwa hao vijana kama tabia yao? Hata kama itagharimu Tough Love(Upendo wenye ukali na msisitizo) refer post ya King'asti
 
Last edited by a moderator:
Kimsingi hakuna tabia ambayo haiwezi kubadilika ikifanyiwa kazi. Ila urahisi au ugumu wa kubadilika tabia inategemea mzizi wa tabia yenyewe ulivyojikita ndani ya nafsi ya mtu. Kwa mfano kuna tabia za kurithi kutoka kwa wazazi, mf. hasira, ukali, nk. Hizi ndo tabia-hulka (nature). Tabia hizi zina mzizi mrefu sana, ili mtu aweze kubadilika anahitaji kusaidiwa sana, kutumia nguvu nyingi na njia nyingi, mazoezi mengi, na pia muda mrefu wa kutosha. Hata hivyo mtu hatabadilika kwa asilimia 100 lakini anaweza ku-improve.

Kuna tabia si za kurithi ila mtu kazipata kwenye mazingira aliyopitia mf. shuleni, vikundi vya marika, nk. Tabia hizi zina mizizi si mirefu sana japo zinaweza zikawa zimemkolea sana mhusika. Hizi zaweza kubadilika kirahisi kidogo ukilinganisha na zile za kwanza kwani hizi ni za kujifunza. Mtu akitumia nguvu, akajitahidi na kusaidiwa na wengine anaweza kubadilika.

Mtu anayekimbilia kusema: "we niache tu ndo tabia yangu" ni mtu aliyekata tamaa kufanya safari ya mabadiliko. Ni mtu anayetafuta udhuru, na asiye tayari kuumia ktk zoezi zima la kujibabadua na tabia yake (au kilema chake). Ni mvivu au mtu mwenye majivuno.

Hakika kila tabia hubadilika na wa kutoa MWELEKEO ibadilike kwenda kwenye HULKA au MANTIKI ni muhusika. Ni hali ya kawaida ya mwanadamu kuwa na ustaarabu uliojengeka kutokana na thamani za uasili wa kibinaadamu unaojitofautisha na hulka za wanyama wanaojiendesha pasipo mantiki yeyote ile!
 
Hivi Kongosho UKARIMU unafundishika au ni TABIA ya kuzaliwa nayo??..Na inawezekana mtu akazaliwa na TABIA ya UCHAFU??....

inasemekana watanzania ni wakarimu kuliko wakenya

ujamaa umewapelekea wa-tz kuwa hivyo, na wakenya kuwa 'rude' u-capitalist umechangia

hospitality college course zinapelekea watu kuwa wakarimu kwenye kada zao
 
Back
Top Bottom