Hivi ni kweli haya mashangingi ya serikali ndo yanauzwa milioni 280?! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni kweli haya mashangingi ya serikali ndo yanauzwa milioni 280?!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, May 3, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Toyota Land Cruiser - 2011 Pictures & Photo Gallery
  2011 Toyota Land Cruiser SUV Models and Prices

  Mimi nashindwa kuelewa, ukiangalia katika website ya Toyota, bei ya Land Cruiser VX G8 ni US$ 68,020 ambazo kwa Tsh. ni kama 102,000,000 tu, hata ukiweka gharama za kusafirisha haitofika milioni 280!!!. Sasa izo bei za milioni 280 zinatoka wapi? Ninavyojua serikali hailipii ushuru magari yake...afu kitu kingine cha ajabu, ukienda kwenye website ya Toyota (T) limited, jamaa hawaonyeshi bei za haya magari!

  Hawa Toyota(T) limited nafikiri wanakula na watu serikalini..na kwanini serikali kupitia kwa wakala wake wa manunuzi wasiwe wananunua moja kwa moja magari yao? kwani ni lazima wawatumie Toyota (T) limited au CFAO motors? (formerly known as DT DOBIE (T) Limited)... Yaani hii serikali yetu kila sehemu inachemsha na kuweka mianya ya watu kechezea fedha za umma.

  Kwa serikali iliyo makini na yenye wakala wa manunuzi ya vyombo vya usafiri vya serikali, middlemen kama akina Toyota(T) ltd na CFAO motors ni wastage ya resources. Hakuna haja ya kua nao..Fullstop.

  Nawasilisha.
   
 2. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 933
  Trophy Points: 280
  Welcome home...
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizi ndizo issues za kuongelea hapa kwa kuwa zina maslahi kwa Taifa. Kama kweli bei yake ni hiyo basi kuna kitu tena kikubwa tu. Ila ujue haya matoyota ya sasa yapo aina nne:

  1. Toyota Land cruiser Standard yenye mkonga (siyo hardtop wala Mark II) mengi kwa hivi sasa ni meupe serikalini yanaitwa Kilimo Kwanza
  2. Toyota Land cruiser Standard ambayo haina mkonga
  3. Toyota Land cruiser GX V8 - Haya ni ya kifahari mengine yana fridge na mengine hayana
  4. Toyota Land Cruiser VX V8 - Haya ni ya kifahari zaidi nayo kuna toleo la kwanza hayakuwa na fridge lakini matoleo ya sasa yana fridge
  Kwa hiyo mkuu hiyo bei isije ikawa ni ya hiyo Land Cruiser ya kwanza hapo juu. Bei pia inategemea na ma options mengine kibao ambayo viongozi wa serikali huwa wanayapenda na bei inaongezeka.
   
 4. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Vyovyote iwavyo, model hizi zote kwa uchumi wa nchi na hali za watu, bado ni ya kifahari mno! Hayafai hata kidogo kwani yana kunywa mafuta mengi mno. Haya siyo economical. Wanunue Toyota Hard Top za kazi siyo haya mashangingi ya starehe!
   
 5. m

  masssaiboi JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2011
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 637
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 33
  Manufacturer hawauzii wateja ila wanawauzia dealers then dealers ndio wanawauzia wateja kama govt.
   
 6. i411

  i411 JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 810
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  unajua hiyo linki uliyotoa ni ya toyota Marekani hizo ni price zao kwavile hayo magari yanatengenezewa huko kwahiyo price inakuwa cheap hivyo. lakini ukitaka kuliagiza huko price inaongezeka. bado hakuna kiwanda cha toyota afrika nachokijua lakini vikifunguliwa magari yatakua chipu kidogo. Manake hawa jamaa parts za gari zitakuwa zinatoka huko japani hau sehemu nyingine duniani alafu watakuwa tu wanaweka pamoja hizo parts zote kufanya gari. Nasikia nisani wanafungua assembling plant huko Kenya karibuni, kikifunguliwa hiko kiwanda hizo nissan patro zinaweza kuwa US $50,000 kwa ile ya top range wanaopendaga hao wazee wetu wa selikali. lets prey toyota wafungue assembling plant bongo. Kikwete umesikia ambia hao waa japani walete kiwanda bongo kama kawaida kodi tutawalipa siye nasikia mnafanya hivyo kwa watu wa madini…….
   
 7. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #7
  May 4, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,139
  Trophy Points: 280
  Kimbunga hii nchi inatawaliwa na utawala wa shetani, usishangae kitu
   
 8. L

  Lughe Senior Member

  #8
  May 4, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 118
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wana uafadhali mkubwa machifu waliokibadilishasha/waliokiuza watu wao kwa waarabu kwa kanzu na vito mbalimbali ang'avuilihali kwa wao kutoyajua madhara yanayoenda kuwafika ndugu zao huko uarabuni:
  kWASABABU YA UFINYU WA UWEZO WA FIKRA ZAO KUONA MBELENI KUTOKANA NA MAZINGIRA YA GIZANI.

  Ila kwa hawa watawala wetu SASA ni maskini sana wa fikra/NA KUNA KILA SABABU YA KUWADHARAU NA KUWAPUUZA kwani pamoja na kuwa na kusoma historia kutoka kwa mababuzetu haiwasaidijia kubaini lipi ni jema.

  Ningependa kuwaona viongozi waanchi yetu maskini kutojali hadhi za kukizi haja za fahali badala yake wawe wazalendo zaidi.Na nadhani wala hayo mashangingi wasinge yapa fursa katika maisha na harakati za kulitumikia Taifa.

  NA HII INADHIHILISHA KWAMBA MWL NYERERE UPEO WAKE ULIKUWA MKUBWA MNO!!!!!KWANI MAPEMA TU BAADA YA KUTOWEKA KWAKE MACHAFUFU YOTE YAPO HADHARANI.

  ili NCHI IJE ENDELEA LAZIMA VIONGOZI WETU WAKILI KWA VITENDO:WAPI JAMII ILIPOTOKA,IPO WAPI NA TUNATAKA KUFIKISHA WAPI?

  yamkini walishajiuliza na ndivyo wanavyoona staili kuyafanya hayo..!JEE SISI wanaJAMII TUNACHUKUA HATUA ZIPI?kama utakubaliana nami watumwa waliuzwa direct iliwezekana kutokana na uwezo wa mdogo wa kuweza kuepuka leo tunauzwa indirect kupitia SIASA.
   
 9. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280

  Mkuu heshima kwako..ebu visit iyo link ujionee mwenyewe...iyo bei ni ya hayo mashangingi (VX G8)....
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  izo options mkuu zina manufaa gani kwa taifa? au sina manufaa kwa mtu binafsi? kwa mfano fridge au vikolombwezo vingine kwenye gari vina manufaa gani kwa taifa?
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu bila hivyo uongozi usingekuwa unang'ang'aniwa ni madili kama hayo tuu!
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mkuu ilitakiwa liuzwe tsh 105,431,000.00 sasa mbona ni mala mbili yake?? na hata kama kunakafaida na usafiri haiwezi kufika hapo penye million 280 yaani tunaibiwa kwakweli!? EEETI WAMEJIVUA MAGAMBA KWELI HAWA NI NYOKA!
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nakuunga mkono asilimia mia nne. yaani huwa nashindwa kuelewa kabsaa hawa wakuu wetu huwa wanafikiria nini, maana dunia nzima hakuna Toyota inauzwa hata $120,000.00, labda iwe ni designer model with special features way far kuliko hiyo mitulinga wanayopakaziwa wakuu wetu na mengi yake hata features zake ni just basic!!!!!
   
 14. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Sisi mazuzu tuuuu!
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  May 4, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi naamini kuwa vikolombwezo vyote hivyo havina faida yoyote kwa nchi. Kwa mfano mkuu anaishi nyumba yake (Aliyopora toka serikalini pale Oysterbay) na anatoka pale kwenda ofisini mjini na huko ofisini kuna fridge na nyumbani kuna fridge vyote vya serikali. Sasa hiyo fridge ya kwenye gari inatumika wakati gani. Akienda mikoani anapanda ndege!! No value for money at all. Inabidi CAG afanye value for money audit ya magari ya serikali
   
 16. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa hawa wanaoishi kimjini mjini wale wapi mkuu ? hii ndio njia moja inayozalisha hawa mapedejee wanaomwaga hela kwenye kumbi za starehe.
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Halafu GB anafikiri eti Magari mapya watu hawachakachui....

  Mitanzania kweli TUMELALA. Ngoja watule ALIVE.
   
 18. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2011
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Toyota motor Corporation wanawawakala nchi mbalimbali duniani hapa kwetu wanawakilishwa na hawa wezi wahindi wa toyota tanzania ltd, mara nyingi ukiagiza gari kwao kama uko TZ au nchi nyingine yoyote wanakuelekeza kwa wale mawakala wao,hii mara nyingi ina apply kwa watu binafsi,makampuni na mashirika yasiyo ya kiserekali . Serekali inauwezo wa kuagiza moja kwa moja kiwandani na kupata punguzo nzuri tu, sasa hawa watawala inakuwa ngumu kwani wakifanya hivyo 10% hawatapata, Hawa jamaa wa toyota tz mjue ni wahindi na wanajua kula na myamwezi ndo maana hali iko ka ilivyo sasa. Mtambue wanawauzia magari serekali na taasisi zake na wao wao ndo wanawatengenezea hayo magari na kuwafanyia service, kwa bei kubwa kama nini. Na hizi garama zinaenda moja kwa moja kwa mlipa kodi, ndo maisha waliyotuchagulia hawa watawala wetu, Budget za haya magari zinaweza jenga mashule, zahanati kununua madawa nk, Rwanda kagame aliamua kuyapiga mnada yaya magari. Museveni nadhani ananunua moja kwa moja Japan, sie tunanunua Nyerere road wapina wapi
   
 19. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2011
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huu ni wizi na hongera kwa kufanya research ya kwanza. Yani hapa ni wizi na tunahitaji kuhakikisha tunafika mwisho wa hii ishu. Nina uhakika, kwanza, kuwa kama unaagiza gari 10, bei lazima ishuke. Na serikali inaagiza magari mangapi? Yani ujinga wetu unatumaliza!!
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Unajua nini mkuu hiyo monopolization ya Toyota hapo Tz huwa inanishangaza kabisa kwa sababu katk nchi nyingi Toyota huwa wanakuwepo wenyewe halafu na dealers maeneo mbali mbali. Hivyo basi kulitakiwa kuwe mfano toyota mwananyamala, toyota kimara, toyota Oysterbay, Toyota igoma, toyota mwanjelwa, toyota sekei etc. Sasa hao jamaa wao wenyewe ndiyo toyota na wao wenyewe ni dealers, wana authorized partners wao mikoani hawaruhusiwi hata kutumia jina la toyota.

  Halafu mtu unanunuaje gari mil. 280 na warranty ya miezi sita au mwaka. Toyota mara nyingi wanatoa warranty ya sio chini ya miaka 3, na kama umenunua gari jipya hata haya ya $20,000 service na maintenance huwa ni bure kwa kipindi hicho. Sasa sikilizia haya ya serikali yetu, eti toyota mil. 280, halafu baada ya hapo lina bajeti ya service na matengenezo mil. 15 kila mwaka. Dili kama hiyo Mercedes wanaweza hata kukutengenezea magari ya kipekee na made to fit mazingira ya bongo.

  Kwa hiyo kuna mawili wizi lakini na jingine kufahamu. Hako kawaziri kalikuja moto (Nyalandu) kaambieni kaongee na toyota japan waondoe hiyo monopoly tz.
   
Loading...