Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,700
- 9,778
Wakuu, Natumai mko poa!
Kwanza nianze kwa kukili kuwa JamiiForums ndio social media pekee ambayo members hujadili mambo yenye manufaa, maisha na shauri chanya!
Kama kawaida, members wa jamiiForums ni watu ambao wako stable kiuchumi, wanaendesha maisha yao katika hali ya kulizika kwa kuwa laki kwao si pesa, milioni kwao ni pesa ya sabuni! Ni members wachache sana ambao hawana magari, wengi wao humiliki ma M.W
Pia members ni watu wa kuhudhuria clubs kila siku, wengine kila weekends, huacha malaki ya pesa mezani pasi na matumizi au kwa ajili ya watoto wazuri, kisha kuingia ndani ya ndinga zao za viwango
Nyuzi zinazotengenezwa humu ndani ni zile za kuomba shauri za kawaida sana katika ndoa kama vile "mke wangu kanikosea, nimpeleke nchi gani bara la ulaya ili akajifunze kutoka kwa wanawake wengine?" Kwa kuwa waswahili wa pwani hujuana kwa vilemba utakuta replies za kutosha na reasons! Lakini mwenzenu nitaleta uzi wa "Kaniacha kisa nimeshindwa kumpatia 50k ya kusuka" ndipo watakuja member watano tu na kusema Tafuta hela! Kisha wengine wawili kuusindikiza uzi na emoji za kunicheka, kisha uzi utafungwa
Hata nitakapojaribu kuomba ushauri juu ya biashara gani nifanye kwa mtaji fulani, nitaishiwa kupondwa tu, wengine wataishia kudandia siti ya mbele kwa dereva, wengine wataanza kujuliana hali ndani ya uzi wangu wa kuomba utatuzi wa jambo.
Juzi nimeanzisha uzi wa "Nina laki na nusu nifanye biashara ipi?" Mdau wa kwanza kaja kudandia siti ya mbele, wakati kwenye uzi wake mmoja anadai boss wao katoa nafasi arobaini za kazi kwa wenye elimu kidato cha nne! Mwingine kafuata na kusema "Tafuta hela kijana " Mwingine kaja kusema "Hama hapo kwa shemeji ulipolala" Aliyefunga uzi kaandika "Hii ni Chai" Aliyem-qoute kaandika "Mods wafute huu uzi" na uzi ukapotea!
Kwa kufupisha mashtaka, Kama kuna mtu ana connection ya kazi yoyote yenye mshahara ambao anahisi nitaweza kuhandle maisha hadi kufikia stage ya kuanzisha familia anisaidie, hata kama ni kazi ya kiwandani ni sawa, hata kama ni kazi ya kununua ni sawa tu, ili mradi mwisho wa siku na mimi nianze kitengeneza nyuzi za "Hili gari langu nahitaji kulichoma, nikalichomee wapi?" ili watu waangushe replies za kutosha na mimi niwe mtu kati ya watu!
Hivi kweli members, mnajiskiaje mkiwa mnatengeneza nyuzi za kutafuta viwanja vya mamilioni halafu mimi naanzisha uzi wa kuibiwa elfu ishilini ndani? Hii haijakaa pouwa! Mwenye connection ya kazi almost hapa Dar anishtue basi twende sawa.
Kuna watakaokuja kusema HII NI CHAI, wengine wataususa uzi, nitawakumbusha mpite hapa hata kwa kuwaita.
Elimu kidato cha sita, ila nilifaulu.
Asanteni kwa kupita hapa!