Hivi ni kwanini wanaume waliooa ni wavivu katika mapenzi..?

FL hili swala kweli lipo na hii inatokana na kuchokana na pia saa nyingine wa mama tunajiachia sana, inabidi kila wakati uwe unaita.
 
mbu upo?
baby anakusalimia sana....!

eti mbu kuna mabadiliko yoyote ya tabia-teamo kabla na baada ya kuwa na kale ''kamgeni''?

...ha ha, nipo bro,
pole na ulezi. Hebu ianzishie topic hii
si unajua penye wengi haliharibiki neno?

Kwa muono wangu, "tabia-mbu" ziliathiriwa kwa kiwango fulani hasa
zile siku za awali, mpaka pale "kamgeni" kalipokuwa kamechangamka
na kutupisha angalau kwa siku mbili tatu tukumbushiane na mama'ke..

Kwani vipi? kibao kimekugeukia? LOL
 
Wanaume wakishaoa ni wavivu sana kwenye mapenzi hao waliooa wajifunze wajue mahitaji ya wake zao na maInfii wao

FL1, Salute! kwa mara ya kwanza wanawake wafunguka!

Tatizo tukishawaoa na nyie mnapunguza mvuto, badala ya kujiremba kama wakati tunaiba mnajiacha hovyo na hasa mkishazaa mpaka mwamme anakuwa hana hamu ya mapenzi. Kingine mnatupikia mapochopocho mengi kiasi kwamba tunakuwa Obese na perfomance inapungua!!

Wewe unakuwa wapi hadi mkeo anajiachia hivyo? Hiki ni kijisababu tu maana wengi wa hao wanawake bado wanajitunza na kupendeza tena zaidi. Na nyie mkipikiwa mapochopocho mkanenepa mnazidia kuvutia ehhh? Na je lawama ndio abebe mke
kwa kukupikia au wewe mwenyewe kwa kula ovyo ovyo? Asipopika nayo itakuwa sababu ya kukimbilia nyumba ndogo! Kwa taarifa yako, wanawake wananenepa shauri ya kuzaa..wanabeba mimba matumbo yanatanuka, je nyie huo unene na ubwanyenye unatokana na jukumu lipi? Mbebwe kwa mbeleko ipi?

ngoja uolewe na wewe utayaona. bnafsi naona wasichana wengi wanajisahau sana baada ya kuolewa na ndio maana nyumba ndogo haziwezi kuisha


swali la FL..umelisona na kulielewa?.....

kabla ya kuoa kuku anakua sio wako.lazima umshikie manati (ujitume mpaka jasho la damu linaweza kutoka) ndo uweze kumuiba.lakini ukishaoa kuku anakua wako, manati ya nini.

bora umekuwa mkweli...

Sio wanaume tu hata wanawake walioolewa nao pia wanakuwa wavivu, ndio maana kunakuwa na nyumba ndogo nyingi.

Nyumba ndogo??? Fikiria tena...

Oyaaa!
Jamani tuoneeni huruma!

Spidi hiyo tutapata wapi, wakati unajua niko na wewe 24/7?...Nikilala upo, nikiamka upo, nikistuka usingizini upo, nikigeukia upande wa pili upo..huh!, sa nguvu zote hizo zitoke wapi besti?

Usilinganishe mambo ya uchumba na ndoa sista!..ni kama mbingu na ardhi!.Hujaona watu wanaenda kwenye appointment na mchumba wakiwa na mashati ya kuazima?..ambapo kwenye ndoa tunakula kilichopo!:pray:

Kua uyaone!

HILI NENO PJ!

Halafu staili hiyohiyo kila siku....lazima hamu itapungua.

hILI NENO..ILA USISAHAU ITS BOTH WAYS

Nashangaa!! Ndio maana wanaume hukimbilia kwenye nyumba ndogo, nasikia wao hujituma na ni wabunifu!

JAWABU JEPESI KWA SWALI GUMU!

Mi nilikuwa nafikiri wanawake ndiyo huwaga hawajitumi, labda kutokana na majukumu ya nyumbani.
Uchovu na..........................kumbe na wanaume nao ni wavivu......
................!!!!!!


YAANI! WE ACHA TU! NOW WE KNOW!
 
Kwani ni mashindano jamani? Halafu wengine wanapta matatizo ya kuangalia yale mamovie wakiona watu wanaperform for hours wanafikiria kila mwanamme yuko kihivyo! Matokeo yake mwisho kutesana tu. Kwa ufupi, wanaume wengi ni wa kawaida tu wala siyo mashujaa kama walivyo wanawake wengine. Maana mwisho watu mtaanza kuwekeana stop clocks ili kuona nani anafanyanini kwa muda gani! Mapenzi starehe, nje ya hapo ni adhabu!!
 
unajua mi sielewi_maana tendo la ndoa mara zote linapojadiliwa huwa ni kuridhishwa mwanamke tu, na wanawake wamejipanga kama wao ndo wanaopungukiwa mbona mentality hii inakua kiasi hiki_angalien msiwe mnapigana wakati aliyeanzisha ugomvi kishaondoka_katika hili nadhan psychology treatment ni muhim otherwise propaganda hiz zitasaidia sana uuzaji wa Viagra na kuumizana unneccessarily_kuridhika is not due to how much but psychological thing
 
Hoja ni ya msingi sana na inajadilika tatizo ni kwamba suala hili haliepukiki kwa sababu zifuatazo:
1. Mkishaoana kama mambo ya ndoa yamekwenda vizuri ina maana kwamba majukumu yataongezeka katika muda mfupi sana wa ndoa hiyo, mfano mna mtoto mchanga hizo mishemishe zake za usiku mara mwili joto limepanda mara analia na vinginevyo vina hamisha attention na kushughulikia yanayoonekana muhimu kwa wakati huo.
2. Kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu kwamba uwezo wa mke kujitunza na kupendeza vyema kama wakati wa uchumba haiwezekani tena hii pia inatokana na majukumu yaliyopo sasa, na hasa ukizingatia kama lengo la kujitunza vyema limeshafikiwa (kuolewa) haina haja tena kutumia muda na pesa kwa ajili hiyo ukizingatia muda pia ni haba wakati huu.
3. Kwa asilimia nyingi attention ya mama huhamia kwa mtoto hasa anapokuwa na umri mdogo na hivyo nafasi ya baba inakuwa sio kivile kama hapo awali.
4. Kina dada wengine hubadili tabia ghafla baada tu ya kuolewa kwa mfano mlikuwa mnatoka wote enzi za wizi kwenye matembezi ya jioni lakini mara baada ya kuolewa huwa hawapendelei matembezi ya jioni pamoja na wapenzi wao hii pia huleta sintofahamu hasa mwanaume akichelewa kurudi nyumbani kwa kuwa hawakuwa pamoja hisia mbaya huanza kujengeka na hii pia huathiri mahusiano na hivyo hamu hujiendea zake.

Cha kukumbuka hapa ni kwamba jana ni jana na leo ni leo siku hazifanani.
 
kuna mabo kadhaa nionavyo;

kwanza wanawake tunapenda sana maandali, by maandalizi I mean not just physical but also meantally. kwa mfano mpo kazini wote, mwenzio anakupigia simu anakujulia hali na kuongelesha maneno matamu ya mapenzi. hapo tayari mwana mama utaanza kufikiria tendo na ukifika nyumbani utajituma

pia wanawake tunapenda kujua kuwa mwenzio anakufikiria, so kumhonga mwenzako vijizawadi vidogo vidogo pia is a part of foreplay.
also jaribuni kubadilisha mazingira, kwa mfano mnaweza mkaamua lunch time mkapelekana guest/hotel mkapigana cha chap chap, kwa kweli inakuwa inaleta msisimuko wa aina yake

cha kushangaza ivi vyote wanaume huvifanya wakati wa uchumba wakishaoa wanasahau, mi nasema inabidi waendeleze. sio kumpigia sim mwenzio mpaka kuwe na jambo la kifamilia au la dharura.

naomba kuwakilisha

Naona humu waaangaliaji wa picha za sinema za mapenzi hasa zile za kigeni ni wengi.
 
Hili balaa hili ndo maana sijaliona

Hivi FL tuseme pamoja na kwamba umedai kuwauliza waliooa na nyumba ndogo, huna kauzoefu kidogo ka kutoka na mwanaume aliyeoa ili uhakikishe mwenyewe:wink2:
 
kwahiyo mwanamke akuhamasishe wewe tu,kisha umparamie mwenzako kisa mwiko uko tayari kupikia.huo ni ubinafsi mkubwa

Hujaolewa ndo maana unaloloma hayo yote. Wewe mwenyewe hapo hata kama mzee anajituma vipi, mwili ukiwa hoi kwa shughuri mbalimbali
speed haiwi kama ulivyokuwa bado kwenu/kwako hamjaowana. Akijitahidi utundu zaidi utafika kileleni lakini huko hoi hutaki kwenda hata round ya pili.

Unaongea mambo ya kufikilika hujaingia uyaone. Kwa sasa unaona ndo shughuri nyeti lakini kuna mambo mengi yanakuwa yanawakabili. Hilo mnalifanya kuhitimisha penzi lenu la ndoa. Karibu kwenye chama ili uweze kuongea katika uhalisia wa mambo.
 
Nyie watoto mnadhani ndoa ni kubanjuana tu. Wakati wa uchumba mnakuwa na majukumu gani? Almost none. Lakini mkioana hata kama hamjazaa tayari mnaanza kukabiliwa na majukumu ya kifamilia, mipango inaongezeka, na mambo kedekede. Sasa katika mazingira kama hayo usitarajie uwezo wa kubanjuana uta-remain constant. Kinachotakiwa ni wote wawili kuwa wabunifu wa kuendelea kuenjoy sexual life. Mmoja akijisahau anakuwa kero kwa mwenzie.
 
Wanaume wakishaoa ni wavivu sana kwenye mapenzi kuliko awali kabla hawajaoa.unakuta zamani kabla hajaingia kwenye ndoa dume lilikuwa linajituma mpaka mtoto wa kike anakolea,ila akiingia kwenye kiapo anakuwa mzito sana.hasa wanaume hawa waliooa wakishikwa hamu hakuna tena maandalizi kwa wenzi wao,huishia kuwaparamia kama vile wamehesabiwa muda wa mechi.nimejaribu kuwauliza wanawake kadhaa walioolewa na baadhi ya nyumba ndogo za wanaume kadhaa, wote wamelikiri hili. Wanajamvi wenzangu naomba mnisaidie kujua sababu ili nami nikiolewa nsikutane na mwanaume mzembemzembe.pia hao waliooa wajifunze wajue mahitaji ya wake zao na maInfii wao

FL it takes two to tango! Quality ya mapenzi ikiwa ni pamoja na kujituma zaidi kabla ya ndoa utokana ushirikiano wa pamoja. Ukweli ni kwamba kama quality (foreplay, lasting long) ya mapenzi imepungua ni wazi kuwa wote mnahusika inaweza kuwa ni kwa asilimia tofauti.

Hivyo mapungufu yanatokea kwa sababu wote for some reasons mnakuwa hamtimizi wajibu wenu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom