Hivi ni kwanini viongozi wetu wa dini wanatuchagulia vifungu vya kutufundisha?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Tangu napata akili kipindi naanza kwenda mafundisho ya sunday school hadi nasoma kipaimara kwa sisi wakristo katika kitabu kitakatifu cha biblia katika vitabu vyote vilivyopo ndani ya biblia

Hakuna siku au mda mara moja kiongozi wa kipindi au mchungaji kanisani kwenye biblia : kitabu cha wimbo ulio bora" sura ya mwanzo hadi mwisho haijawahi kutolewa mstari hata mmoja tunafundishwa.
Hua wanarudia baadhi ya vitabu hadi mistari mingine tumeshaikariri hadi tumeichoka.

Je, ni kwanini hii mistari ya hiki kifungu cha wimbo ulio bora inatengwa?kwani sio mistari ya kutufundisha haifai?kwani imewekwa ya nini? Kama wanaona haifai kwa nini chuo cha biblia wasiirekebishe au kuitoa kama inawekwa tuu alafu hatufundishwi inarukwa?
 
Jukumu la kujifunza kila kitu ni lakwako viongozi wanakupa miongozo tuu kulinggana na somo husika.
Sio kweli kwani wanaruka kifungu hicho hadi inawafanya warudie baadhi ya vifungu vingine na mistari
 
Sasa mkuu si usome na kujifunza hivyo vinavyo rukwa. Shida ipo wapi?? Vile vinavyo rudiwa ndio haswa vya msingi
 
Tangu napata akili kipindi naanza kwenda mafundisho ya sunday school hadi nasoma kipaimara kwa sisi wakristo katika kitabu kitakatifu cha biblia katika vitabu vyote vilivyopo ndani ya biblia,
Hakuna siku au mda mara moja kiongozi wa kipindi au mchungaji kanisani kwenye biblia :kitabu cha wimbo ulio bora"sura ya mwanzo hadi mwisho haijawahi kutolewa mstari hata mmoja tunafundishwa.
Hua wanarudia baadhi ya vitabu hadi mistari mingine tumeshaikariri hadi tumeichoka.
Je? Ni kwa nini hii mistari ya hiki kifungu cha wimbo ulio bora inatengwa?kwani sio mistari ya kutufundisha haifai?kwani imewekwa ya nini? Kama wanaona haifai kwa nini chuo cha biblia wasiirekebishe au kuitoa kama inawekwa tuu alafu hatufundishwi inarukwa?

SI wanasema eti "Mungu KAWAFUNULIA"......waumini ni mabumunda kabisa!

Dini is by the stupids and for stupids only!
 
Tukubalini tu,waafrika tuliingizwa chaka...undefinedundefinedMimi kwakweli siwezi kupoteza mda wangu tena
 
Jukumu la kujifunza kila kitu ni lakwako viongozi wanakupa miongozo tuu kulinggana na somo husika.
Ushauri matata sana. Na hapa ndio watu wanakosea kusubiri kusomewa!!. Ni kweli viongozi wanapaswa kuandaa utaratibu wa waumini wao kujifunza maandiko, lakini haiondoi wajibu wako kujisomea na pale ambapo unakumbana na mambo magumu waulize wakubwa zako. Na maandiko mengine watu hawayapendi kwa kuwa yanaeleza mambo ambayo yasonda kabisa kile ambacho kinafanyika kwenye makanisa hayo. Kwa mfano kama kanisani kwenu kuna masanamu usitegemee kiongozi wako asome fungu hili
Kutoka 20:4-6
4 Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu cho chote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini duniani, wala kilicho majini chini ya dunia.
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
6 nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.

Utasubiri sana
 
Yes. Wengi wanatumia maadiko kama referrence kusapoti hoja au mafundisho yao. Hivyo lazima wawe selective na baadhi ya mistali
 
Tangu napata akili kipindi naanza kwenda mafundisho ya sunday school hadi nasoma kipaimara kwa sisi wakristo katika kitabu kitakatifu cha biblia katika vitabu vyote vilivyopo ndani ya biblia

Hakuna siku au mda mara moja kiongozi wa kipindi au mchungaji kanisani kwenye biblia : kitabu cha wimbo ulio bora" sura ya mwanzo hadi mwisho haijawahi kutolewa mstari hata mmoja tunafundishwa.
Hua wanarudia baadhi ya vitabu hadi mistari mingine tumeshaikariri hadi tumeichoka.

Je, ni kwanini hii mistari ya hiki kifungu cha wimbo ulio bora inatengwa?kwani sio mistari ya kutufundisha haifai?kwani imewekwa ya nini? Kama wanaona haifai kwa nini chuo cha biblia wasiirekebishe au kuitoa kama inawekwa tuu alafu hatufundishwi inarukwa?

Jibu unalo tayari, ni kwa sababu wanataka ukariri yale wanayotaka wao uyakariri. Narudia, achana na hizi dini za kuletewa na maboti mkuu....hazina tija kwetu hata kidogo.
 
Kama wewe hutaki kusoma biblia wafanyeje. Ndio maana wanakulisha hata upupu na wewe hujijui. Kwani umewahi kujiuliza kwaninu unasali dini hiyo? Na biblia imeikubali?
 
Nilizaliwa kwenyebdini hiyo na nilikuta wazazi wangu wakiwa nayo hivyo ni vigumu kupindisha
 
Hicho kitabu kinatumika sana katika mafundisho ya ndoa, hvyo zile semina ambazo wanandoa watarajiwa huenda sometimes reference htoka hapo
 
Wimbo Uliobora 3:5
" Usiyachochee wala kuyaamsha mapenzi hadi yatakapoona vyema yenyewe''

Lakni pia Metaphor au SITIARI ya Mungu na kanisa au mfuasi wake ni Bwana harusi (Mungu) na Bibi Harusi (wafuasi).
Kuzini au kuchapuka nje ya ndoa ni Kufanya dhambi, maana Yake umeenda kufanya mapenzi na shetani.

Ukidecode hicho kitabu kwa mtazamo huo utapata mengi pianya kujifunza humo na kukuza mahusiano yako na Mungu.
 
Back
Top Bottom