Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
2,825
6,259
Nakumbuka miaka ya 80-90 ilikuwa jambo la kawaida kukuta jamaa wanapigana mitaani halafu watu wanashangilia sana.

Yaani ukiwa mtemi au gangwe basi unaonekana wa maana sana. Hata baadhi ya disco ilikuwa lazima ziishe kwa ngumi.

Kwa wale wa Iringa mtawakumbuka kina cool 9, shedadi, Ray nk
 
Siku izi ukirusha ngumi. Wanakupiga chupa ya kichwa. Ndio maana watu wamekuwa wastaarabu. Au unapigwa spana ya mdomoni lazima meno yatoke. Na ndio maana mtaani ukipata mdaa ukapita unakutana na vijana wengi awana meno iyo ni spana ya mdomo. Maeneo mengi vijana wamepoteza meno
 
Daah, ilikuwa si mchezo, yaani watu wazima, mbabe wa kila mtaa wanakutana na zinakunjwa huku watu wamezunguka
Nakumbuka Mtaani kwetu kulikuwa na Zitto na Jamali, sikumtimu zao zinacheza lazima mkono uwekwe
 
Anyway! Sishabikii watu kupigana muda wa kupigana tutumie kutafuta maisha.Lakini sikweli kwamba watu hawapigani watu wanapigana ikibidi. Mimi mwenyewe siwezi kukumbuka ni lini ila nishazipiga hivi karibuni na watu fulani ambao walikuwa wananiletea habari zao ambazo sio!.
 
Watu siku hizi wanapigana na kazi wapate hela....hayo mambo yalikuwa enzi hizo ukiwa na mia tano unakula mpaka unasaza....ukienda hospitali madawa ya kumwaga na vitanda mpaka mnapiga msamba........kodi ya nyumba shilingi elfu tano.....ukienda kariakoo kazi kibao tu.....sasa hivi ukiuchokoza ugomvi ni balaa lako....maana utamlisha mtu na familia yake mpaka uione dunia chungu......
 
Mleta mada unanikumbusha mbali sana 1981 ama 1982 kama sijakosea kuna dogo flan aliingia anga zangu kijijin huko mbarali kwa kumtongoza mchepuko wangu. Nilitembeza vitasa kijiji kizima kwa madogo wote wenye umri kama wake. Maumiv makal sana niliwakabiz kwa kosa la mtu mmoja. Yan nilikuwa na bwaka nikiibuka 10 ardhin nikizama nikichomoza 20 wengine chali. Nikamchukua dogo mwengine mwembamba hiv nikamtumia kama fimbo kwa kuwacharaza. Ila kwasasa nimejikita zaid kusaka hela uzee nao ndio huo. Ila miaka iyo ya themanini nilikuwa mtemi sana
 
Back
Top Bottom