Hivi ni kwanini katika kila familia kuna watu hawa?

Zee Korofi

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,612
1,410
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
 
Ngoja Mr Mshana aje akupe hintis za uzao wa kwanza kuwa lango la baraka/laana ktk familia
  • Uzao wa kwanza ktk viumbe hai utamtolea bwana sadaka
  • Mshahara/kipato/faida ya kwanza ktk biashara utatoa kama sadaka, eti hapa ndipo tunapokosa baraka na kupelekea familia kuwa na hivyo ulivyoainisha
 
Kuna mengi yanayochangia iyo hali;

1. Umaskini wa familia/kutegemewa
2. Kuhisi kukataliwa/kutengwa hasa akizaliwa mdogo wake, ubaya wanajikuta wanakuwa na hiyo hali hadi ukubwani
3. Kutokubali kufundishwa, kujiona mkubwa.
4. Kuzidiwa tu maarifa na wadogo zake.

Ila kwa ujumla kufanikiwa kunatokana sana na mwenendo binafsi wa maisha ya mhusika.
 
Majukumu ni mengi maana mtoto wa kwanza akianza kazi kama wazazi hawajiwezi sana anakua yeye baba kwa wadogo zake anapoteza vingi sana mpaka wadogo zake wasimame.

Sasa mpaka wadogo wanasimama unakuta yeye hajajijenga wala nini pesa zote zinaishia kwa madogo halafu wao wanakua hawana wa kumuangalia wanaanza kusema sisi wazembe aloo basi tu.
 
Hakuna cha kwanza, pili, tatu,nk. Ilikuwa zamani sana.

Kujituma ndio suluhisho pekee. Kuna mtu amezaliwa Ifakara, mama na baba yake walikuwa hawana kitu. Akafaulu darasa la saba. Alichowasumbua wazazi ni ile mahitaja ya kwanza tu! Maana ilibidi wazazi wauze ng'ombe wao.

Baada ya hapo hakujua kitu kinaitwa likizo. Likizo ilikuwa ni mwendo wa kufanya vibarua mashambani kwa kwenda mbele, toka day one mpaka mwisho. Na alikuwa naweza hata kuwaachia wazazi kitu fulani cha matumizi.
Baadae akapiga zake Tambaza.

Mengine mtajaza wenyewe. Ni Ofisa fulani Total.
 
Ni kwa sababu jamii zetu nyingi bado zipo katika kizazi cha kwanza cha kiuchumi. Katika jamii zilizopiga hatua katika maswala ya kiuchumi, hamna kitu kama hicho.

Angalia jamii zenye biashara kubwa za kifamilia kama vile Waarabu, Wahindi na Wazungu.

Kama ni valid basi ingekuwa universal, ingeapply hata kwa familia ya Rockerfeller, kina Walmart, British royal family, kina Rostam, Mo, Dangote, familia ya Kenyatta, Moi, Jaramogi etc.

Tatizo kubwa ni umaskini wa kurithi na changamoto(constraints) za kimazingira.

Imagine umesoma kwa shida toka day one unaanza shule, unasoma kwa bidii, unamaliza na shahada ya kwanza kabisa, Mungu ni mwema na ukapata na kazi yako ya kwanza na mshahara mzuri tu.

Lakini sasa wadogo zako nao bado wapo kila ngazi ya elimu kuanzia msingi. Wanahitaji msaada wako.

Wazazi kijijini wana nyumba ya msonge na kuezekwa na majani, wewe na shahada yako ukiona unachanganyikiwa. Unaona huna mahali pa kurudi likizo au unaogopa hata kuwapeleka marafiki zako akiwepo na mtoto wa watu atakayekupenda.

Wazazi hawana kitega uchumi chochote.
Sasa hapo utafanikiwaje haraka kiuchumi?
Huku mjini unahitaji vitu kibao kwa ajili ya geto lako na maisha yako ya kila siku.

Hakuna laana, shida ni umaskinj wa kurithi. Na inaweza kuwa na chain kali sana.
Unakuta upande wa babu mzaa mama nao ni maskini, upande wa babu mzaa baba nao ni hohe hahe, fukara.

Yaani poverty depth ni kubwa sana na hata severity yake inakuwa kubwa sana.

Sasa kinachowakuta wazaliwa wa kwanza ni "Poverty Severity" kutokana na familia nyingi za Sub Sahara Africa kuwa katika wakati wa kuchomoza jua la asubuhi(mawio).
 
Ni kwa sababu jamii zetu nyingi bado zipo katika kizazi cha kwanza cha kiuchumi. Katika jamii zilizopiga hatua katika maswala ya kiuchumi, hamna kitu kama hicho. Angalia jamii zenye biashara kubwa za kifamilia kama vile Waarabu, Wahindi na Wazungu. Kama ni valid basi ingekuwa universal,
Shabaash, "chain inaweza kuwa kali sana", hapo nimekuelewa mno, ila cha kushukuru ni kama wazazi hawakutegemei wewe, na huna ndugu wanaosoma wa kukutegemea.
 
Hakuna cha kwanza, pili, tatu,nk. Ilikuwa zamani sana.
Kujituma ndio suluhisho pekee. Kuna mtu amezaliwa Ifakara, mama na baba yake walikuwa hawana kitu. Akafaulu darasa la saba. Alichowasumbua wazazi ni ile mahitaja ya kwanza tu! Maana ilibidi wazazi wauze ng'ombe wao.
Baada ya hapo hakujua kitu kinaitwa likizo. Likizo ilikuwa ni mwendo wa kufanya vibarua mashambani kwa kwenda mbele, toka day one mpaka mwisho. Na alikuwa naweza hata kuwaachia wazazi kitu fulani cha matumizi.
Baadae akapiga zake Tambaza.
Mengine mtajaza wenyewe. Ni Ofisa fulani Total.
Nani huyo? Au ni wewe?
 
Inategemea kuna familia ambazo mtoto wa kwanza kawa msaada mpaka wengine wameweza kusimama na bado yupo vyema, na kuna wengine wa katikati au mwisho na bado wameweza kuiinua familia

Issue ya mtoto mmoja kuwa attached kwa baba au mama hainaga formula hutokea tu naturally na kukuta hata mzazi akijaribu vipi kubalance upendo kwa wanae wote bado kuna mmoja atawazidi wengine
 
Ukiona Kuna mtoto kwenye familia yenu hafanani na nyie kitabia ,akili na wengineyo jua mama alipiga ndefu akawaletea kiumbe ambaye si damu ya baba yenu,
Tabia mbaya/nzuri/akili /upunguani/umasikini, vinategemeana na mbegu ilikotoka
 
Tatizo waaafrika na sisi tunazaa mno watoto wengi wakati uwezo wa kuwalea ni wakuunga unga. Matokeo yake first born anaanza kujikuta ana jukumu la kulea wadogo zake 7 atapataje mafanikio sasa? Halafu wazazi wakishazaa wao wanajitoa utasikia "unajua mdogo wako kamaliza la saba"
 
Mzaliwa wa kwanza ni mlango wa kupitisha baraka Kwa ajili yake na Kwa ajili ya wengine
Kwa hiyo siku zote uelewe mlangoni ndio Mahali vita vinafanyikia
 
Ukiona Kuna mtoto kwenye familia yenu hafanani na nyie kitabia ,akili na wengineyo jua mama alipiga ndefu akawaletea kiumbe ambaye si damu ya baba yenu,
Tabia mbaya/nzuri/akili /upunguani/umasikini, vinategemeana na mbegu ilikotoka
Ila hii sio kwa sehemu kubwa.
 
Back
Top Bottom