Hivi ni kwanini katika kila familia kuna watu hawa?

Binafsi siamini kabisa hayo Mambo,na pia uzao wa Kwanza ninao wajua karibu wote wamefanikiwa kwa Hali zote...
 
Ni kwa sababu jamii zetu nyingi bado zipo katika kizazi cha kwanza cha kiuchumi. Katika jamii zilizopiga hatua katika maswala ya kiuchumi, hamna kitu kama hicho.

Angalia jamii zenye biashara kubwa za kifamilia kama vile Waarabu, Wahindi na Wazungu.

Kama ni valid basi ingekuwa universal, ingeapply hata kwa familia ya Rockerfeller, kina Walmart, British royal family, kina Rostam, Mo, Dangote, familia ya Kenyatta, Moi, Jaramogi etc.

Tatizo kubwa ni umaskini wa kurithi na changamoto(constraints) za kimazingira.

Imagine umesoma kwa shida toka day one unaanza shule, unasoma kwa bidii, unamaliza na shahada ya kwanza kabisa, Mungu ni mwema na ukapata na kazi yako ya kwanza na mshahara mzuri tu.

Lakini sasa wadogo zako nao bado wapo kila ngazi ya elimu kuanzia msingi. Wanahitaji msaada wako.

Wazazi kijijini wana nyumba ya msonge na kuezekwa na majani, wewe na shahada yako ukiona unachanganyikiwa. Unaona huna mahali pa kurudi likizo au unaogopa hata kuwapeleka marafiki zako akiwepo na mtoto wa watu atakayekupenda.

Wazazi hawana kitega uchumi chochote.
Sasa hapo utafanikiwaje haraka kiuchumi?
Huku mjini unahitaji vitu kibao kwa ajili ya geto lako na maisha yako ya kila siku.

Hakuna laana, shida ni umaskinj wa kurithi. Na inaweza kuwa na chain kali sana.
Unakuta upande wa babu mzaa mama nao ni maskini, upande wa babu mzaa baba nao ni hohe hahe, fukara.

Yaani poverty depth ni kubwa sana na hata severity yake inakuwa kubwa sana.

Sasa kinachowakuta wazaliwa wa kwanza ni "Poverty Severity" kutokana na familia nyingi za Sub Sahara Africa kuwa katika wakati wa kuchomoza jua la asubuhi(mawio).
Kuweza kupambana na umaskini huo lazima watu waache kuzaa hovyo hovyo.
 
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
Hizo Imani tu hakuna cha mtoto wa kwanza wala wa mwisho mafanikio yanategemea na wewe unajituma vipi..mengine porojo na kujazana ujinga tu
 
Kwenye maisha kila mmoja ana njia yake ya kutoboa....baba yangu aliwahi kunihusia.."ukipotea wewe maana yake na wadogo zako wote watafuata njia hiyo"...
Maisha yanendelea.. Mzee anajua njia niliyopita..
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
Umefanya uchunguzi kwa kiasi gani kujiridhisha hii ni hali halisi na si kughafilika kwako tu?
 
Mtoto wa Kwanza ni lango la kifamilia, ni rahisi mno kuwa attached na maadui maana adui anajua akishalifunga hili basi kawafungia wote na hata ambao hawajazaliwa. sasa bila maombi, sadaka mafanikio huwa ni ngumu mno.

Hakikisheni mnawajenga watoto wenu kwa kwanza kiroho ili adui asipate mwanya wa kupita kupitia wao, kwani wao wamebeba lango la familia.

Malango au Lango ni nini?

Lango au Malangoni eneo katika ulimwengu wa roho ambalo Mungu Mtakatifu hulitumia kupitishia Baraka kutoka ulimwengu wa roho na kuja hapa duniani. Vilevile kama malango yameharibika yanaweza kutumiwa hata na shetani.
Mfano wa malango ni kama ifuatavyo nayo ni;
(i) Mzaliwa wa kwanza.
(ii) Viuno vya baba mzazi.
(iii) Tumbo la uzazi la mama.
(iv) Malango ya uchumi au fedha.
(v) Malango ya ndoa.
(vi) Malango ya Kanisa.
(vii) Malango ya utumishi.
(viii) Malango ya mji.
(ix) Malango ya nchi.
(x) Malango ya kabila
 
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
Hizi ni imani tu,hapa mtaani kwetu Kuna jamaa tupo nae ofcn,yeye ni mtoto wa mwisho,kaka zake wanamkwanja mrefu balaa,jamaa alipoanza kazi na kuoa,mmoja wa kaka zake akaamua kumwachia Mshikaji Lodge/guest house yake aiendeshe apate pesa na yeye ajijenge.
Hao ma braza wapo vzr balaa na ma business kibao.
Wakiona deal nzuri wanampa mdogo wao Ili na yeye ainuke.
Wao ndio waliomsaidia kupata hiyo ajira,
Inategemea tu.
 
Kuna mengi yanayochangia iyo hali;

1. Umaskini wa familia/kutegemewa
2. Kuhisi kukataliwa/kutengwa hasa akizaliwa mdogo wake, ubaya wanajikuta wanakuwa na hiyo hali hadi ukubwani
3. Kutokubali kufundishwa, kujiona mkubwa.
4. Kuzidiwa tu maarifa na wadogo zake.

Ila kwa ujumla kufanikiwa kunatokana sana na mwenendo binafsi wa maisha ya mhusika.
Bila shaka we sio mzaliwa wa kwanza
 
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
ungesema hivi wazaliwa wa kwanza hasa wa kiume
 
Cain alikuwa maskini tu kuliko Abeel!
Yusufu aliuzwa mdogo alikuwa tajiri kuliko Reuben mkubwa wao!
Musa alikuwa tajiri kuliko mkubwa wake aliye mpeleka mtoni
Yakobo alikuwa tajiri mpaka leo tunamjua kuliko kAKA yake ishmael
Yesu ni tajiri mpaka leo kuliko kaka yake shetani
Nyerere alikuwa tajiri kuliko kaka zake wote
orodha nindefu!!! ile mbegu ya kwanza inakuwaga ni ya shetani anataka kupotezea malengo ya Mungu. ukiona mkubwa ametusua basi jua kabisa kuna kimimba hapo kati kimechomoka kwa kujua au kuto kujua!
 
Mzaliwa wa kwanza ni mlango wa kupitisha baraka Kwa ajili yake na Kwa ajili ya wengine
Kwa hiyo siku zote uelewe mlangoni ndio Mahali vita vinafanyikia
Hivi hizi imani potofu zitaisha lini? Inasikitisha sana, soma sababu hapa chini...
Tatizo waaafrika na sisi tunazaa mno watoto wengi wakati uwezo wa kuwalea ni wakuunga unga. Matokeo yake first born anaanza kujikuta ana jukumu la kulea wadogo zake 7 atapataje mafanikio sasa? Halafu wazazi wakishazaa wao wanajitoa utasikia "unajua mdogo wako kamaliza la saba"
 
Kwahiyo mtoto wa kwanza wa rostam azizi au wa Saidi bakhresa huko alipo anapitia hali ngumu sana? Mawazo ya watu waliokata tamaa yanashangaza ulimwengu mzima
 
Kuna mtoto wa kwanza (kaka au dada), mara nyingi anakuwa hana maisha. Kuna mtoto wa mwisho au wa kati kati, hawa ndio huwa nguzo na hubarikiwa kifedha na kuiinua familia.

Kuna mtoto aliye karibu mno na baba au mama.

Kikubwa ni hiki, kwanini wanaofanikiwa karibu katika kila familia huwa si wazaliwa wa kwanza?
hivi kumbe zee korofi wakt mwingine unaonaga mbali sanaa!! daaa jua kuwa Tangia eden watoto wa kwanza wana wivu sana kwao kufanikiwa ni sifuri sababu shetani anawawinda sana! ndo lango
 
Back
Top Bottom