Hivi ni kwanini CCM na Mwenyekiti wenu Taifa mnapenda kutufanya Watanzania wote hamnazo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,694
109,128
Hivi kweli CCM mnataka Kutudanganya Watanzania kuwa Mapendekezo ya kuweka Tozo Umiza kwa Wananchi yaliyofanywa na Waziri wa Fedha Dk. Nchemba kwanza hayakupita Kwenu kama Chama Dola na hata kwa Mwenyekiti wenu Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na mkayabariki?

Sasa iweje leo tena mnatuonyesha Undumilakuwili wenu wa Kujifanya nanyi mmeguswa na Machungu ya Tozo Umiza kwa Wananchi ambayo nyie nyie mliibariki na sasa kuitaka Serikali ( ambayo inaundwa na CCM ) ipitie upya hizi Tozo Umiza ili kuwapunguzia Machungu Wananchi ambao wengine ni wana CCM Wenzenu?

Na wala msianze kusema sijui GENTAMYCINE ni Mpinzani hivyo anatumika Mimi ni Shabiki Mwandamizi ( ila bado sijawa Mwanachama ) wa CCM na hiki ninachokiwasilisha hapa nakitoa katika Fikra nyingi za Watanzania ambao kutokana na Fani yangu nakutana nao 24/7 na Wanalalamika mno.

Kitendo cha leo hii CCM kujitokeza hadharani kuhoji hizi Tozo Umiza zenu wakati zilipitishwa na 99% ya Wabunge wa CCM, ikabarikiwa nanyi CCM kama Chama Dola na Kubarikiwa zaidi na Mwenyekiti wenu Taifa Rais Samia Suluhu Hassan ni Unafiki Usiovumilika kwa Sisi Watanzania wenye Upeo, Maono na Akili Kubwa kuwazidi.

Mtanichukia ila Ukweli ninawapeni!!!
 
We unaona ccm wanaakili kweli?
Wape kazi ya kuiba pesa kuanzia ngazi ya kitongoji hadi huko juu serikalini hakuna mwenye kujali masilah ya umma..
 
Hivi kweli CCM mnataka Kutudanganya Watanzania kuwa Mapendekezo ya kuweka Tozo Umiza kwa Wananchi yaliyofanywa na Waziri wa Fedha Dk. Nchemba kwanza hayakupita Kwenu kama Chama Dola na hata kwa Mwenyekiti wenu Taifa Rais Samia Suluhu Hassan na mkayabariki?

Sasa iweje leo tena mnatuonyesha Undumilakuwili wenu wa Kujifanya nanyi mmeguswa na Machungu ya Tozo Umiza kwa Wananchi ambayo nyie nyie mliibariki na sasa kuitaka Serikali ( ambayo inaundwa na CCM ) ipitie upya hizi Tozo Umiza ili kuwapunguzia Machungu Wananchi ambao wengine ni wana CCM Wenzenu?

Na wala msianze kusema sijui GENTAMYCINE ni Mpinzani hivyo anatumika Mimi ni Shabiki Mwandamizi ( ila bado sijawa Mwanachama ) wa CCM na hiki ninachokiwasilisha hapa nakitoa katika Fikra nyingi za Watanzania ambao kutokana na Fani yangu nakutana nao 24/7 na Wanalalamika mno.

Kitendo cha leo hii CCM kujitokeza hadharani kuhoji hizi Tozo Umiza zenu wakati zilipitishwa na 99% ya Wabunge wa CCM, ikabarikiwa nanyi CCM kama Chama Dola na Kubarikiwa zaidi na Mwenyekiti wenu Taifa Rais Samia Suluhu Hassan ni Unafiki Usiovumilika kwa Sisi Watanzania wenye Upeo, Maono na Akili Kubwa kuwazidi.

Mtanichukia ila Ukweli ninawapeni!!!
Maendeleo imekuwa kisingizio cha kuumiza wananchi. Ukisoma bajeti hayo maendeleo yamepangiwa asilimia ngapi unabaki kuhuzunika tu. Miezi michache iliyopita CCM hao hao na serikali yao walisema uchumi umeshuka sababu ya Covid na Vita ya Ukraine. Lakini bajeti inafika wananchi wanawekewa tozo umiza kwenye akiba zao zilizoko benki. Yaani kwa nchi uchumi umeshuka sababu ya Covid na Vita lakini Covid na vita havijaathiri uchumi wa Wananchi? Hizi hesabu zimepigwa na Mchumi mwenye Mawe 3 na anayejitapa Elimu imemkomboa na hakuna mchumi kama yeye kama alivyojitapa juzi Tarime ambako naona Wanaume wote wamehamia Kitunda Dar maana wakati wa Tarime asilia asingekwenda kuongea upuuzi ule wakamuacha hasa ukizingatia anatokea Iramba ya Singida na siyo Iramba ya Majita.
Lakini pia ni yeye huyu aliyesema alitumwa na wananchi kuleta tozo lakini ghafla anasema ameunda tume ya kuchunguza KERO ya tozo yaani tozo zimekuwa KERO na kweli ni kero. Chama na serikali wanakaa kuandaa KERO kwa wananchi wanaowaongoza? Halafu bado kuna watu wana imani hiki Chama kina nia njema na Watanzania wakati kila siku kinabariki KERO dhidi yao?
 
Huyu hapa kasema alitumwa na Wananchi, sijui ni wa Iramba Singida au wa Iramba Majita?
IMG-20220901-WA0005.jpg
 
Mtoa hoja hii mengi binafsi ninaafiki na ni ukweli kuwa watanzania hasa working class wengi ni mazuzu, waoga wa kupambania haki yao na kila kitu tu wepesi wa kukimbilia humu kulalama, kuna mtu alitufanya mazuzu na matokeo yake kikundi kidogo cha watu kinafanya kinavyotaka with pure impunity, mwanza huko police wameua as usual tutalalama humu then kimyaaaaaaa
 
Back
Top Bottom