Hivi ni kwa nini?

Rubi

JF-Expert Member
Oct 5, 2009
1,615
326
wataalamu naomba mnisaidie kunijuza. binafsi napenda sana kunywa uji hasa uji lishe kuliko kunywa chai hasa ikiwa ya rangi.

Tatizo nikisha kunywa uji baada ya muda kupita kama nusu saa hivi naanza kupatwa na usingizi natamani hata kulala nakuwa najitahidi kujizuia kulala kwa sababu niko kazini hivyo nitazunguka hapa na pale pia na kunywa maji ili nisisinzie.

Sasa ni kitu gani kinasababisha mtu kusinzia ukishakunywa uji?
 
Huo unga wa uji unaokunywa anaanda nani,unakunywa mama lishe au?watu wengine wanachanganya amira,wengine wanachanganya muhogo,wengine wanachanganya na valiumkidogo.kama kweli unapenda afya yako tafuta mazingira mazuri ya kuandaliwa labda mkeo,dada,mama au mwenyewe.vinginevyo kuna tatizo la tumbo lako wakati wa myeyusho wa chakula tumboni,na kama ni hali ya kawaida tu wewe unachongangani nini?
 
Kaka A nikiri kuwa mimi sio mtaalamu wa haya mabo ya food and Nutrition/Biology lakini ki layman understanding ni kwamba uji hushibisha kuliko chai. Normally baada ya kula kifuatacho ni process ya digestion ambapo nguvu kubwa ya mwili hutumika katika hyo process. Hapa ndipo kausingizi kanapokujia. Sio uji tu hata ukishiba sana au uakila chakula km maharagwe utajikuta unasinzia mda mfupi baada ya kula.
 
uji una starch "wanga" mwili unakuwa busy kufyonzwa every nutrients till to the last drop ndio maana unajihisi kuchoka.. thats the only scientific reason behind
 
uji una starch "wanga" mwili unakuwa busy kufyonzwa every nutrients till to the last drop ndio maana unajihisi kuchoka.. thats the only scientific reason behind
asante njiwa kwa maelezo ya kitaaluma yamejitosheleza. Maana hata usiku nikishakula huwa najisikia kulala mara baada ya kula. ila huwa najikip bize nisilale kwa sababu inashauriwa sio vizuri kumaliza kula na kulala hapo kwa hapo nagalau saa nzima ipite ndio ulale.
 
Samahani kwani wewe ni mtani wangu (unabana matumizi au), uji tumia mara moja moja, siku nyingine kunywa chai yako na bites nzuri, haaa uji kila siku umekuwa mtoto mdogo.
 
Samahani kwani wewe ni mtani wangu (unabana matumizi au), uji tumia mara moja moja, siku nyingine kunywa chai yako na bites nzuri, haaa uji kila siku umekuwa mtoto mdogo.

Tehetehe mtani, binadamu tunatofautiana yaani mimi nikiamka asubuhi nakunywa maji ya moto (warm) nusu lita na kama nimeamka mapema sana nakunywa hata lita moja na kama kuna ndizi mbivu nashushia kama tatu au nne hivi ndio naenda oga najianda kwenza kazini. kati ya saa nne na saa tano nakunywa uji ambao najua una virutubisho vyote ninavyohitaji, i.e. ngano, soya, mbaazi, mchele n.k huo uji nakunywa na vitafunwa kama bites n.k ambacho ninacho kwa siku hiyo. Jioni nala dinner yangu kama kawa bila kusahau matunda ambayo naweza kula wakati wowote lakini kabla ya mlo kwa tofauti ya nusu saa mapka saa moja.

Kwa kweli mimi sio mpenzi sana wa chai hata nikikosa sijuti. Chai kwangu mara mojamoja tena ikiwa ya maziwa fresh ndio napenda; haswa ikiwa imechanganywa na tangawiz fresh, au michaichai, au mdalasini, cocoa, n.k. yaani iwe inanukia kwa ladha ya kupendeza na isiwe ya rangi.
 
Back
Top Bottom