Hivi ndoa ni suluhisho la wapendanao??

Huwa naona baadhi ya watu huwa wanajiiba sana wanaenda kumaliza haja zao kwa wale wapenzi wao wa zamani pindi mama mwenye nyumba anapokuwa ana :mimba::mimba::mimba:

waachen watoto wadogo waje kwangu maana ufalme wa mbingun ni wao kijana karibu ufalme wanguumenifurahisha
 
Hizi Ndoa atutaacha kuandika hata kama kurudia mara mia maana madhara yake ayanaendelea kujirudia kila mtoto akizaliwa ana shida ya ndoa yy????????????????
Mi niliumizwa sana ndio maana najitahdi kuwakumbusha wenzangu wasiumie kama yaliotukuta ingawa aikufika kwenye ndooa ila ilikaribia al manusra ile kwangu..kuna mtu wa Mungu akanijia na kuniambia aniombee nipate mke mwema nikamwambia ombea huyu mchumba wangu nilie nae kupata nishapata ila kuoa nafikiria..akasema yeye ajali alie nae bali anajali kusudi la Mungu wapendwa msipime Huyu Mungu,, mwanamke alipozidi kukremishwa ndoa mwezi wa ^&*** basi kichwa akikajaa maji yule jamaa nikamrudia nikamwambia sasa ombea kusudi la mungu kama wangu niwe nae kama sio ile kwake ,..nakwambia mwezi mmoja na nusu jamani....yule dada alikuwa kama kapata ukiachaa wa ndoa alafu moyoni nikamwona kama jini fulan ....nikamwaga manyanga kabla ya binti kudai amechoka na wanaume wa tanzania akaanza kunywa ovyo nina miaka nae 2 nanusu sijawah kuona kilevi mdomon mwake..weeeeeeeee wachen haya mambo sio mchezo..nikaja kukapata kabinti kamoja kakiwa kanafanya mtihan open na mie nafanya akatoka analalamika na mie nikallaamika wametugonga leo kuelekea parking kumbe kapaki pemben yangu kuwasha gari aiwaki nikachukua miwaya yetu kimoyo moyo namwambia mungu jaman si unipe huyu awe wangu..wee..gari ikawaka akaogopa ikazimka nikamwambia endesha yangu m niendeshe yako akaanza kufikiria nikamwambia usiogope unakula upako wa magari ya wanakondoo wa YESU akatangulia mbele nikawa nyuma tukfika KIFRUITS Duh nkasema sio mchezo....kama ujuavyo na mafuta yetu .nkamwambia mungu kama nilivyokanyaga hii ardhi nitakanyaga nikiwa nakuja kwa wakwe zangu leo hii ndio mama FAITH wangu..jamani msicheze na ndoa.....wewe unaeingia ukiwa unajua malengoyako kumuumiza nakuhakikishia MUNGU atakupa kichapo take frm me..hapa hapa duniani..
 
Pamoja na kuchangia kooooote, lkn mwanamke au mwanaume bila mke mme, hutaheshimika ktk jamii, utaonekana muhuni muhuni tu! Umri ukishaenda huna ujanja, tuchaguane mapema kabla ya machweo jamani!
 
At last leo nimefurahia thread yako ubarikiwe big up to mama Faith huyo ndie uliyepangiwa ukataka kujiforce kwa mwingine lol,Tusichoke kuhubiri hizi ndoa huwezi jua unaweza saidia wengi
 
hapo mie ndio nachokaga kabisa, mtu kaoa jana , leo yupo na hawara wanaburudika, ndio mana wengine tunatanguliza ubabe....ndo cku hizi ni urembo wa kujivalia mapete tu.
Kuna limtu nalijua lilienda kutafuta chumba cha honeymoon na bibi yake wakalala huko mpaka siku ya harusi kavalishwa suit kaenda kanisani kuapa ndoa! na usiku ule honeymoon ikaendelea unadhani hapo kuna mapenzi kweli kwenye ndoa ya aina hiyo?
 
Kuna limtu nalijua lilienda kutafuta chumba cha honeymoon na bibi yake wakalala huko mpaka siku ya harusi kavalishwa suit kaenda kanisani kuapa ndoa! na usiku ule honeymoon ikaendelea unadhani hapo kuna mapenzi kweli kwenye ndoa ya aina hiyo?


hayo yalikuwa majini mahaba bila kujijua na baya zaidi wachungaji waliofungisha yawezekana walijua wanatokea wapi siku hiyo??ni Mungu asaidienhaya makanisa yetu dia
 
Kila kitu ulichokuwa unafanyiwa wakati wa bf/gf relationship ndio unacho hamishia kwenye ndoa hakuna jipya. Kama mlikuwa mnatembea na watu wengine wakati wa uhusiano wenu wa bf/gf, basi msitegemee mabadiriko mtakapo oana.Manake kuna wengine wanasema labda nikimuoa huyu atatulia au labda nikimlazimisha anioe atatulia , hapana, tabia yake atakuja nayo kwenye ndoa hata kama si mwanzoni mwa ndoa baadae tabia itaendelea.

Kama wote waaminifu katika mahusiano yenu ya bf/gf basi uhaminifu utaendelea kwenye ndoa. Kwani hio tamaa haiwezi kuanza ghafla tu kisa ndoa, toka mwanzo itakuwa ilikuwepo labda uhuru kidogo utakuwa umepungua wa kutoka nje ya ndoa.

Kuhusu watoto, kama wote hamko tayari kuwa na watoto, basi bora msubiri mpaka mtakapo kuwa tayari. Hata kwenye uhusiano wa gf/bf kama mimba ikija mmoja hakuwa tayari lazima uhaminifu utapungua na ukorofi kuanza. Sio kwamba mtoto akija kwenye ndoa mtu anaanza kwenda nje, wako pia wale ambao hawajaolewa wana watoto wanakimbiwa pia. Kwahio swala sio kwenye ndoa tu tatizo watu wengi hawajiandai na mabadiriko ya kuja kwa mtoto kwenye ndoa au uhusiano wa kawaida na kujumlisha kasumba yetu ya kwamba mwanamke akishazaa ndio kasha fuja. Kama mtu anawazo hayo ni vizuri akakaa mbali na swala mtoto/watoto na amtafute mwenzake ambaye wote watakubaliana kwamba hakuna mtoto/watoto kwenye uhusiano wao . Ni vizuri watu tukaelimishana zaidi kuliko kutumia watoto kama kisingizio cha kutembea nje ya ndoa. Vizuri ni kujiandaa kama wote hamko tayari haina haja ya kuwa na mtoto/watoto.Kama wote mko tayari ni rahisi kushirikiana kwa pamoja na kuweza kudumisha mapenzi yenu.

Kwa wanaolewa kwa kufata tamaa ya pesa haina haja kuwazungumzia kwani kila kibarua lazima ukitolee jasho.
 
hayo yalikuwa majini mahaba bila kujijua na baya zaidi wachungaji waliofungisha yawezekana walijua wanatokea wapi siku hiyo??ni Mungu asaidienhaya makanisa yetu dia
Yaani we acha tu, watu wengine utadhani wameshikiwa bunduki kuoana
 
Back
Top Bottom