Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Loo, wanacheka, wanarukaruka, wanacheza wakifurahia uzinzi, ulevi, ulaghai, wizi, na anasa za dunia. Wanadhani maisha hayo hayana tatizo. Lakini Biblia iko wazi kabisa: maisha ya dhambi yana mwisho mbaya mno. Ni mateso ya milele na milele. Tafadhali, fuatana nami leo tuitafakari habari ya tajiri na Lazaro iliyoandikwa katika Luka 16:19–31, pamoja na maandiko mengine, tuone kwa undani mateso yanayowasubiri wanaoendelea kufurahia dhambi na kukataa kuokoka:
1. Watu hao wakifa tu, wanaingia moja kwa moja mahali penye mateso. Biblia inasema tajiri aliyekuwa akifurahia maisha ya anasa alikufa na mara moja akaingia katika mateso:
“Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso...akalia” (Luka 16:22–23)
Hii ni tahadhari kwa wale wanaoishi katika dhambi: kifo sio mwisho wa maisha, ni mwanzo wa mateso ya milele kwa wasiotubu.
2. Wanateseka katika moto mkali usiozimika. Tajiri aliyezoea starehe, alijikuta akililia tone la maji kwa sababu ya mateso:
“Akalia, akasema, Ee baba Abrahamu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, aupoze ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu.” (Luka 16:24)
Wale wanaoishi maisha ya ulevi, uasherati na dhambi nyingine hawatapata tena faraja wala kicheko, bali mateso makali yasiyo na mwisho:
“Nao watatupwa katika tanuru ya moto; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.” (Mathayo 13:42)
3. Wanajuta sana, lakini majuto ya marehemu hayana faida. Tajiri alitamani ndugu zake waambiwe ili wasiende mahali alipo kwenye mateso, lakini alikuwa amechelewa:
“Basi, nakuomba, baba, umtume Lazaro... awashuhudie.” (Luka 16:27–28)
Majuto hayo yatawapata wote wanaodharau habari njema za Yesu Kristo. Ni heri ujute sasa na kuacha dhambi zako kuliko kujuta milele bila msaada.
4. Watahukumiwa na kisha kutupwa katika ziwa la moto. Kuzimu ni hatua ya kwanza tu. Baada ya hukumu kuu ya mwisho, watenda dhambi wote watatupwa kwenye ziwa la moto la milele:
“Na iwapo mtu yeyote hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.” (Ufunuo 20:15)
Hii ndiyo hatima ya mwisho ya wale wanaoendelea kufurahia dhambi bila kutubu. Jehanam ni mahali penye maumivu, upweke, huzuni, hofu, na mateso ndani ya moto usiozimika, milele na milele.
Ndugu yangu usipoteze bure fursa ya kuingia mbinguni. Kama tulivyoona, wenye dhambi wanapokufa bila kutubu, hawana tena nafasi ya kubadilisha hatima yao. Tajiri alimwona Lazaro akiwa kifuani mwa Ibrahimu, lakini hakuweza kufika huko (Luka 16:26).
Furaha ya dhambi ni ya muda mfupi, lakini athari yake ni ya milele. Mtu akiikataa neema sasa, ataukosa uzima wa milele baadaye.
Bado nafasi ipo. Leo ni siku yako mwafaka ya kuacha dhambi na kumrudia Mungu, na kumpokea Yesu awe Bwana wa maisha yako. Usingoje hadi uwe mfu ndio ujue uzinzi na ulevi vilikuwa mtego wa ibilisi.
Naamini umenielewa na utafanya uamuzi wa kuokoka sasa hivi. Kumbuka, hakuna aijuaye siku ya kuondoka duniani. Kwa sababu hiyo, usiupuuze ujumbe huu, vinginevyo ukifa kabla hujatubu na kuokoka, utaingia kwenye mateso hayo ya milele.
“Tazama, sasa ni wakati uliokubalika; tazama, sasa ni siku ya wokovu.”
(2 Wakorintho 6:2)
cc: Binti wa zamani Mallerina Lamomy I feel good leo dada