Hivi ndivyo tutakavyomkwamisha Dk. Magufuli

ngozimbili

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
1,398
1,006
Kwanza niondoe shakashaka yoyote juu nia,uwezo na sababu za DK MAGUFULI za kulipeleka taifa letu tunalolipenda sana kwenye ustawi.

Lakini napata mashaka makubwa kama taifa kwa maana ya wananchi tupo tayari kushirikiana na Rais wetu kuelekea tunakokukusudia,
tulitarajia baada ya uchaguzi kuisha na waliopata dhamana kutangazwa taifa lingerudi pamoja kwani kwenye demokrasia hakuna mshindi na mshindwa bali TAIFA huwa ndio limeshinda.

Hapa lazima niwe mkweli sikutegemea kubeza na kununa kwa upande wa upinzani(kwani walichopata si haba toka kwa chama dola kama CCM).

Lakini sikutegemea kuzomea,kejeli ama kujaribu kulibinafsisha taifa kutoka kwa CCM.

Kwa mujibu wa tume UKAWA wana 40% ya ushawishi ktk nchi na ili nchi iende inahitaji kuwa wamoja kama taifa na hapa ndipo yalipo majukumu yetu kama wananchi.

LAZIMA TUFAHAMU HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAEWEZA KUFANIKIWA BILA YA KUUNGWA MKONO TAIFA.
 
TAIFA NI JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
Hii sio JAMHURI YA ZANZIBAR na wala sio JAMHURI YA TANGANYIKA hii ni JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
ikiwa uchaguzi ZANZIBAR utafutwa bila shaka MAGUFULI atakuwa rais wa TANGANYIKA na ikiwa kura zilizosimamiwa na ZEC na zikapelekwa NEC kutoka majimbo yote ya ZANZIBAR zikatambuliwa kama kura HALALI sasa kuna haja gani ya kutaka kufuta uchaguzi wa ZANZIBAR.
ZEC itangaze matokeo tusitafute balaa,
lakini kwa kuenenda tunavyoenenda kama ya ZANZIBAR hayatuhusu basi huu ndio MPASUKO mkubwa kuliko yote ktk taifa letu,
na mpasuko utatutagharimu sote lakini hasa mtu anaeitwa JOHN POMBE MAGUFULI.
 
Hakuna mjinga yoyote wa kumkwamisha Magufuli. Ulishawai ona ndege inarudi rivasi? Magufuli ni kama ndege kwa sasa ndio inaanza kasi ata kupaa haijaanza. Wanaosema ana nguvu ya soda ni wale wanaoishi kwa nguvu ya viroba.

#Hapa kazi Tu
 
Hao viongozi wa Ukawa wengi wao waliamua kusutia uapishwaji wa Dr. Magufuli. Kabla ya hapo wanaukawa walikuwa wanafurahia kuzomea zomea wakati wa kampeni. Hata baada ya Dr. Magufuli kushinda kwa kishindo (manaake alikuwa anapambana na vyama vinne chini ya Mh. Lowassa), Ukawa bado wanaendeleza tabia ya kususa na kutokuunga mkono jitihada zozote zinazofanywa na Mh. Magufuli katika kutatua matatizo ya wananchi na kulipeleka taifa mbele. Sasa ni nani anayetaka kulipasua hili taifa? Upinzani Tanzani bado sana. Eti ukiwa mpinzani maana yake ni kujivua uzalendo. Endeleeni na huu upuuzi wenu lakini mjue wananchi walio wengi sio wajinga kama mnavyodhani.
 
Hakuna mjinga yoyote wa kumkwamisha Magufuli. Ulishawai ona ndege inarudi rivasi? Magufuli ni kama ndege kwa sasa ndio inaanza kasi ata kupaa haijaanza. Wanaosema ana nguvu ya soda ni wale wanaoishi kwa nguvu ya viroba.

#Hapa kazi Tu

Mzee wa msonga mbona walimkwamisha??na kumbuka alianza kwa kasi mwisho wakongwe wa siasa wakamtoa kwenye mstari wa maendeleo na kumpeleka kwenye starehe hakawa mzee wa kubadili anga leo marekani kesho kule akasahau maendeleo watanzania waliomtuma.sokoine pia.

swissme
 
kwanza niondoe shakashaka yoyote juu nia,uwezo na sababu za DK MAGUFULI za kulipeleka taifa letu tunalolipenda sana kwenye ustawi,lakini napata mashaka makubwa kama taifa kwa maana ya wananchi tupo tayari kushirikiana na Rais wetu kuelekea tunakokukusudia,
tulitarajia baada ya uchaguzi kuisha na waliopata dhamana kutangazwa taifa lingerudi pamoja kwani kwenye demokrasia hakuna mshindi na mshindwa bali TAIFA huwa ndio limeshinda.
hapa lazima niwe mkweli sikutegemea kubeza na kununa kwa upande wa upinzani(kwani walichopata si haba toka kwa chama dola kama ccm).
lakini sikutegemea kuzomea,kejeli ama kujaribu kulibinafsisha taifa kutoka kwa ccm,
kwa mujibu wa tume UKAWA wana 40% ya ushawishi ktk nchi na ili nchi iende inahitaji kuwa wamoja kama taifa na hapa ndipo yalipo majukumu yetu kama wananchi,
LAZIMA TUFAHAMU HAKUNA KIONGOZI YEYOTE ANAEWEZA KUFANIKIWA BILA YA KUUNGWA MKONO TAIFA.

Mkwere anasema hiyo 42% ni wanywa viroba
 
Wengi ni wachanga wa siasa nchini..na pia wamekosa pa kuficha aibu..wapenda maendeleo tupo wengi kuliko wao wapenda upinzani..rubani wetu magufuli habadili gia angani
 
akitaka tusimuangushe apitishe ile rasimu ya warioba, ile kiboko itamfanya raisi aszurure kwenye mawizara maana inawajibisha hata yeye atakua anaweekend daily
 
Hakuna mjinga yoyote wa kumkwamisha Magufuli. Ulishawai ona ndege inarudi rivasi? Magufuli ni kama ndege kwa sasa ndio inaanza kasi ata kupaa haijaanza. Wanaosema ana nguvu ya soda ni wale wanaoishi kwa nguvu ya viroba.

#Hapa kazi Tu

Uwe unashirikisha ubongo wako kufikiri.
 
Ujinga zaid ni kuamin lowassa alpata 39%, wakat kwa uhalisia alionewa huruma tu na NEC
 
Hakuna mjinga yoyote wa kumkwamisha Magufuli. Ulishawai ona ndege inarudi rivasi? Magufuli ni kama ndege kwa sasa ndio inaanza kasi ata kupaa haijaanza. Wanaosema ana nguvu ya soda ni wale wanaoishi kwa nguvu ya viroba.

#Hapa kazi Tu

"GREAT THINKER AT HIS LOFTY HEIGHT"
Hamia FB
 
Akili za kijinga kama zako ndio zitakazomkwamisha Dr Pombe Magufuli.
Yaani unamfanya Magufuli hana akili kiasi hili?

Back
Top Bottom