Hivi ndivyo hofu zinavyotugharimu kwenye safari ya ujasiriamali

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
HOFU INAVYO TUGHALIMU KWENYE SAFARI YA UJASIRIAMALI

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapenda kuwa kama Mengi siku moja. Tunavyokuwa tunaendelea kutamani kuwa kama wakina Azam au Mengi nyuma ya pazia tuna matatizo nayo ni hofu kuu,

1. Hofu ya kuchekwa
Wengine tuna hofu ya kuchekwa kwamba tunafanya biashara gani hizi? Tuna lima kilimo gani hiki au tunafuga nini? Kuna watu hofu ya kuchekwa tu inatosha kumtoa Barabarani mazima. Mtu leo hii anashindwa Kuanzisha project anayo peda kwa sababu tu anaogopa kuchekwa

2. Hofu ya kushindwa kabla ya kuanza
Tuna hofu za kushindwa, naona nikifuga kuku nitashindwa, naona nikilima nitashindwa tu, hofu hii inatufanya tuone bora kusubilia kwanza
Fear of Unknown inatusumbua.
Watu tunashindwa kuanzisha miradi kisa tu mtu anaogopa kushindwa.

3. Hofu baada ya kuona walioa anza wakashindwa
Hii ni kubwa sana, mtu anakuambia fulani alifuga Broiler wakafa wote, fulani alifuga layers wakamshinda, Fulani alilima nyanya kavuna debe moja tu, fulani.
Watu wengi tunashindwa kuanza kwa sababu fulani alishindwa. Sikiliza fulani sio wewe, fulani ana akili yake na wewe una akili na nguvu zako.

4. Hofu ya Elimu zetu.
Kuna walio bahatika kusoma hadi Univesity na wana Degree na Wengine Masters. Sasa elimu zetu nazo zimekuwa. kikwazo, mtu anaona kwa elimi yake hapaswi kufanya aina fulani ya biashara, hapaswi kufuga au kulima anapaswa kufungua Yard ya kuuza Magari
Elimu zetu ni kama tulienda kusomea uoga vile.

5. Hofu ya Ndugu, jamaa, Marafiki na kadhika.
Kuna mtu mpaka sasa hawezi fuga au anzisha mradi kwa sababu tu ndugu jamaa na marafiki hawatamuelewa. Mama hatanielewa kwamba nalima na nimesoma, Mama mkwe na Baba mkwe watanishangaa sana kwamba nafuga Bata, Mchumba hatanielewa kabisa na anaweza nikimbia mazima kwa sababu nalima Nyanya na nina Degree,

6. Hofu ya kukosa baadhi ya vitu.
Mtu anaona kuliko akose kwenda kutazama mpira na washikaji bora huo mradi usianze tu, kuliko nishindwe kwenda viwanja bora nisianze ,siwezi enda kulala shambani nikashindwa kwenda kuona npira au kucheki move.

Kwa Kifupi tuna hofu nyingi sana zinazotugharimu.

SASA BASI
Kama unaishi kwenye hofu za aina hizo kamwe sahai kufanikiwa labda tu ukomae na ajira,

Nilazima utambue kwamba uko wewe na honor uwezo wako, ipe heshima Uwezo wako. Ukiona hofu hizo ni kikwazo kwako na huwezi ziacha kama una mtaji basi kanunue vipande ya hata UTT na usubilia gawio, au nunua hisa za kampuni na subiliaga gawio kulingana na faida.

Kwenye ulimwengu wa Ujasiriamali lazima kwanza Uonekane mwehu, lazima second person akuone kichaa, lazima watu wakushangae ,

Ujue hata kichaa yeye huwa hajui kama ni kichaa ila second person na third ndo tunaona na tunajua kwamba fulani ni kichaa, the same na wewe kwamba lazima ifikie mahali watu washindwe kukuelewa kati ya haya yaani wajiulize maswal mengi bila majibu.

- Fulani hivi kafukuzwa kazi?
- Fulani hivi kweli alimaliza chuo? Au alidisco?
- Fulani anaongea mwenyewe barabarani
-Fulani maisha ni kama yamemkamata, hapa kisa tu huonekani viwanja.
-Fulani haonekani viwanja kabisa.
- Fulani anacheza na ujasiriamali hiyo awaachie wakina Mengi

Watu wakianza story za aina hizi basi jua uko kwenye track nzuri.
UJASIRIAMALI SIO ISHU YA KITOTO, LAIZMA UWE KAMA UKO ULIMWENGU MWINGINE KABISA

Weekend Njema
By Chasha Farming
0767 691071

NB: Kuna watu wanacopy kazi za watu wengine na kufanya ni zao.Huu ni wizi na ni aina ya uvivu wa kiwango cha juu kabisa.
 
A
HOFU INAVYO TUGHALIMU KWENYE SAFARI YA UJASIRIAMALI

Wengi wetu tunapenda Mafanikio, tunapenda kufika mbali tunapeda kuwa kama Mengi siku moja.

Tunavyo kuwa tunaendelea kutamani kiwa kama wakina Azam au Mengi nyuma ya pazia tuna matatizo nayo ni hofu kuu,

1. Hofu ya kuchekwa
Wengine tuna hofu ya kuchekwa kwamba tunafanya biashara gani hizi? Tuna lima kilimo gani hiki au tunafuga nini? Kuna watu hofu ya kuchekwa tu inatosha kumtoa Barabarani mazima.
Mtua leo hii anashindwa Kuanzisha project anayo peda kwa sababu tu anaogopa kuchekwa

2. Hofu ya kushindwa kabla ya kuanza
Tuna hofu za kushindwa, naona nikifuga kuku nitashindwa, naona nikilima nitashindwa tu, hofu hii inatufanya tuone bora kusubilia kwanza
Fear of Unknown inatusumbua.
Watu tunashindwa kuanzisha miradi kisa tu mtu anaogopa kushindwa.

3.Hofu baada ya kuona walioa anza wakashindwa
Hii ni kubwa sana, mtu anakuambia fulani alifuga Broiler wakafa wote, fulani alifuga layers wakamshinda, Fulani alilima nyanya kavuna debe moja tu, fulani.
Watu wengi tunashindwa kuanza kwa sababu fulani alishindwa. Sikiliza fulani sio wewe, fulani ana akili yake na wewe una akili na nguvu zako.

4. Hofu ya Elimu zetu.
Kuna walio bahatika kusoma hadi Univesity na wana Degree na Wengine Masters. Sasa elimu zetu nazo zimekuwa.kikwazo, mtu anaona kwa elimi yake hapaswi kufanya aina fulani ya biashara, hapaswi kufuga au kulima anapaswa kufungua Yard ya kuuza Magari
Elimu zetu ni.kama tulienda kusomea uoga vile.

5. Hofu ya Ndugu,jamaa, Marafiki na kadhika.
Kuna mtu mpaka sasa hawezi fuga au anzisha mradi kwa sababu tu ndugu jamaa na marafiki hawatamuelewa. Mama hatanielewa kwamba nalima na nimesoma, Mama mkwe na Baba mkwe watanishangaa sana kwamba nafuga Bata,
Mchumba hatanielewa kabisa na anaweza nikimbia mazima kwa sababu nalima Nyanya na nina Degree,

6. Hofu ya kukosa baadhi ya vitu.
Mtu anaona kuliko akose kwenda kutazama mpira na washikaji bora huo mradi usianze tu, kuliko nishindwe kwenda viwanja bora nisianze ,siwezi enda kulala shambani nikashindwa kwenda kuona npira au kucheki move.

Kwa Kifupi tuna hofu nyingi sana zinazo tugharimu.

SASA BASI

Kama unaishi kwenye hofu za aina hizo kamwe sahai kufanikiwa labda tu ukomae na ajira,

Nilazima utambue kwamba uko wewe na honor uwezo wako, ipe heshima Uwezo wako.
Ukiona hofu hizo ni kikwazo kwako na huwezi ziacha kama una mtaji basi kanunue vipande ya hata UTT na usubilia gawio, au nunua hisa za kampuni na subiliaga gawio kulingana na faida.

Kwenye ulimwengu wa Ujasiriamali lazima kwanza Uonekane mwehu, lazima second person akuone kichaa, lazima watu wakushangae ,
Ujue hata kichaa yeye huwa hajui kama ni kichaa ila second person na third ndo tunaona na tunajua kwamba fulani ni kichaa, the same na wewe kwamba lazima ifikie mahali watu washindwe kukuelewa kati ya haya yaani wajiulize maswal mengi bila majibu.
- Fulani hivi kafukuzwa kazi?
- Fulani hivi kweli alimaliza chuo? Au alidisco?
- Fulani anaongea mwenyewe barabarani
-Fulani maisha ni kama yamemkamata, hapa kisa tu huonekani viwanja.
-Fulani haonekani viwanja kabisa.
- Fulani anacheza na ujasiriamali hiyo awaachie wakina Mengi

Watu wakianza story za aina hizi basi jua uko kwenye track nzuri.

UJASIRIAMALI SIO ISHU YA KITOTO, LAIZMA UWE KAMA UKO ULIMWENGU MWINGINE KABISA

Weekend Njema

By Chasha Farming
0767 691071

NB: Kuna watu wanacopy kazi za watu wengine na kufanya ni zao.Huu ni wizi na ni aina ya uvivu wa kiwango cha juu kabisa.
.

Ahsante mkuu Shasha.Wengi tulikukumbuka.Hoja makini ya mtu makini husomwa na watu makini na huchangiwa na watu wachache makini.

Ukweli unakimbiza wengi.Umegonga mahali sahihi tulio tayari tutajitathmini na kuchukua hatua.Walalamikaji na waogopao hawaoni kitu.Uthubutu ni Zaidi ya mtaji,uvumilivu ni nyenzo ya mafanikio.Mawazo yako ukiyafanyia kazi ni kielelezo cha ukomavu wa akili yako.

Wengi wanasubiria kudesa kama walivyodesa kupata misonge mingi shuleni na uraiani misonge hiyo haizai tija Zaidi ya malalamiko ya uhaba wa ajira,mishahara kiduchu na huduma duni.Fursa hawazioni hadaharani wala vichwani mwao,kisa hofu.Ahsante kwa somo zuri tutaikataa hofu.
 
Mkuu umesema kweli na yote hiyo ni ili mtu athubutu tu, lakini humo ndani ujasiriamalini kuna mitihani. kuna kipindi kama hujatulia unaweza wehuka..

Mie mtu akinitajia ujasiria mali nakumbuka level ya u sensei kwenye martial art , mengi unakutana nayo mwishoni unakuwa na nidhamu ya hali ya juu..
 
Nimejifunza kitu aisee mkuu...ila.ni kama kuna maandiko yako mengine waweza nipa heading nikayasoma
 
Ukweli mtupu, ,,.Nilikua Na hofu nyingi sana baada ya mkwamo wa kibiashara ila nikapiga moyo konde na kuanza upya kidogo kidogo. Safari inaendelea kwa matumaini makubwa.
 
MKUU UMECHOMA PENYEWE, HONGERA SANA UMEONGEA UKWELI BILA GANZI.

MATOKEO YAKE HOFU HZ HUMFANYA MTU AFE MASKINI.
 
Back
Top Bottom