Hivi ndivyo ccm inavyohujumiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ndivyo ccm inavyohujumiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Jun 20, 2012.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Wahenga wanatwambia kama unaishi kwenye nyumba ya vioo usiwatupie maadui zako mawe. Ninapata shida sana kufuatilia hoja za wabunge wa ccm bungeni, kama kuna kitu wanafanikiwa ni kuwakejeli wabunge wa upinzani. Bahati mbaya kejeli hizi ni mafanikio kwa wapinzani.

  Bajeti inayojadiliwa bungeni ni ile ya serikali ambayo wapinzani wanaipinga kwa hoja ambazo zimewasilishwa kupitia waziri kivuli na michango mingine ya wabunge inayoendelea bungeni sasa. Wabunge wa ccm kuivalia njuga hoja ya waziri kivuli ni kufirisika kimawazo. Hoja ya waziri kivuli ni mchango na mawazo ya upinzani. Utashanga ccm wameacha agenda na kuunda agenda yao. Mwisho wa siku ccm wote hawatakuwa wamemtendea haki waziri wa fedha maana hakuna cha maana anachopata kutoka kwao.

  Wamepoteza wasikilizaji nje ya bunge wakiona wa ccm anasimama wanasema ni wale wale wa yaleyale.
  Hakuna kitu kibaya katika siasa kama kupoteza mvuto na maana yake ni kukosa fursa ya kusikilizwa. Ukisifiwa na mke wako, watoto na ndugu zako wewe si kitu, maana unatekeleza yale wanayotegemea kutoka kwako. Ni vema ukafanya vizuri na kuvutia watu wengine nje ya wale ambao wanakuhusu.


  Kwa hiyo kama watu wanadhani wabunge wetu wa ccm wanakijenga chama kwa kuwakejeli wa upinzani hii ni bahati mbaya sana tena sana kwani matokeo yake ni kinyume. Ccm inabomolewa na wabunge wake bungeni. Ccm inabomolewa na makada wake serikalini na ccm inabomolewa na wanasiasa wake uchwara majukwaani. Kama ingekuwa siasa ni mchezo wa pointi kama ngumi sasa hivi refa wa mpambano wa wapinzani na ccm alipaswa kusimamisha mpambano kwani ccm inatoka damu kila sehemu ya uso na majeraha yamekuwa makubwa mno.

  Bondia wa namna hii anaweza kupandwa hasira na kushika silaha ya aina yoyote akaishia kuua nataahadharisha washabiki na bondia anayepambana nae kuchukua tahadhali mapema.
   
 2. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 554
  Trophy Points: 280
  Umenisababisha nione kama damu inatoka kiukweli
   
 3. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Wanajua kabisa kwamba hata wakichangia hajuna kitakacho badilika kwenye bajeti yao. Baadhi yao walijaribu kuipinga wakapigwa mkwara waka fyata mkia. Kwa hiyo wameona wapoteze muda ambao wangeutumia kuijadili na kuchangia kuwaponda wapinzani. Mwisho wa siku bunge la bajeti litakwisha na wao wanabeba posho zao.

  Tunawasubiri tu uraiani 2015 ni kikomo. Na wakijaribu kuchakachua haki ya nani tutabeba silaha..bora tuishe wote kuliko kuishi kwenye shida wakati mali tunazo.
   
 4. A

  Alhandro Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 91
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Ulichokiongea kinamsaada mkubwa kwa watu walio tayari kusaidika,lkn kwa vile wapewao ushauri ni sawa na sikio la kufa, bado litaenelea kutoa usaha tu kuelekea kuzimu hata ufanyeje.Na nina kutahadhalisha ukae mbali kwani kwa jinsi lilivyo kwisha halibika nakusihi ukae mbali kwani unaweza kutumbukiwa na pindi litokeapo hilo stashangaa kwani ni kawaida ya mgonjwa huyu pale aonekanapo kusaidiwa kumgeuka msaidizi wake kwa matusi na kejeri kibao na kisha kujigamba kuwa yeye ni doctor tena daraja 1 ktk hospitali ya rufaa ilihali haonyeshi mawazo ama mchanganuo wowote wa kitabibu unao weza kuleta ufanisi.Sijui ni DR gani huyu hata mganga wa kienyeji hawezi kuwa hivyo.Ama kweli kama asemavyo Andanenga,"Usione mgongo kutuna ukadhani umeshiba,macho kuona,ukadhani yatizama,kila uonacho,usione ukadhani"
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145

  Majibu haya hapa:

  Mghaka Unasema....!


  Nami nimeyasema jana haya unayoyasema leo!


  Mghaka hii Point yako....


  Mie nili iyona kwa mtazamo huu:


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. B

  Bob G JF Bronze Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ccm ziku zote inajimaliza yenyewe ili kuijenga CDM
   
 7. c

  chigwiye JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 353
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na hakika CCM watamwaga damu tu, hilo ndilo litakua azimio la mwisho.Naionea huruma nchi yangu kwa yatakayoikumba siku za usoni
   
 8. G

  Geru Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Waache waendelee na nidhamu ya woga lakini mwisho wao ni hukumu ya 2015. Tunaoiombea mema nchi hii tuhakikishe tunapiga kura 2015 na kuilinda!
   
Loading...