Hivi ndivyo Barrick watakavyotupiga chenga matrilioni yetu

Mandesy

Senior Member
Mar 22, 2018
116
250
Ikiwa bado watanzania wakisuburi hatma ya mazungumzo kati ya serikali na kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick yenye makao makuu yake nchini Canada, kampuni hiyo imeanza kujinasua, hali itakayosababisha Tanzania kukosa fedha inazodai takribani dola bilioni 194 za Marekani.

Barrick ambayo inamiliki asilimia 64 ya Acacia, kampuni tanzu ambayo imewekeza kwenye migodi mitatu mikubwa ukiwemo ule wa Tulawaka Biharamuro ambao ulifungwa na makapi kukabidhiwa Stamico, imeanza kuicha solemba Tanzania.

Wakati serikali ikijinasibu baada ya kuahidiwa dola million 300 na Barrick, matumaini ya kuipata hiyo fedha hayapo tena, labda huruma ya Barrick wenyewe.

  • Kwa sasa Barrick inanunua kampuni ya Randgold ya Afrika kusini kwa dau la dola bilioni 18, hali hii inaonyesha kwamba wanaelekeza zaidi nguvu ya kibiashara Afrika Kusini, ambayo ni miongoni mwa nchi zinazozalisha dhahabu kwa wingi sana Africa
  • Barrick inaanda mpango wa kuchukua his azote za Acacia kutoka asilimia 64 za sasa, hii ikiashiria kwamba, huenda kampuni ya Acacia ikawa 100 per cent inamilikiwa na Barrick.
  • Wakati hayo yakiendelea, Acacia hiyo hiyo imeuza mgodi wake wa dhahabu wa Nyanzaga uliopo shinyanga (asilimia 51) kwa OreCorp Limited. Mpango wa baadaye ni kwamba OreCorp itamalizia kuzinunua hisa zilizobaki asilimia 49. Katika mradi huo, Barrick watabakiza mtambo wa kuchenjua dhahabu tu na OreCorp watakuwa wakizalisha na kuchenjua kwenye mtambo wa Barrick uliopo mgodini hapo
  • Kampuni ya Barrick imeanza mazungumzo ya kampuni ya Shandong ya China kwa ajili ya kuingia ubia kwenye miradi yao ya dhahabu ulimwenguni. Hadi sasa wanamiliki kwa pamoja mgodi ulioko Argetina. Katika makubaliano hayo, Shandong itachukua asilimia 50 ya hisa za Barrick na barrack kuchukua asilimia 50 za hisa za Shandong Limited.
Baada ya makubaliano na Shandong, huenda jina la Barrick litatoweka na itaanzishwa kampuni moja ya ubia kati ya Barrick na Shandong ama watampa Shandong ya China, ambayo ni rafiki wa Africa na Tanzania kuendesha miradi yake Tanzania. Kampuni hiyo huenda ikaitwa Shandong ama jina lingine ili mradi Barrick Gold, ambayo ina beef na Tanzania itoweke na tushindwe wa kumkamata.

Mwisho wake, tutaona Acacia inachukuliwa na Barrick, Barrick inabadilisha jina la kampuni ya Ubia na Shandong ama kubakiza Shandong, jina ambalo halina madhara na ukizingatia China ina urafiki wa karibu na Tanzania. Huenda China wakaahidi kuisaidia Tanzania kwa misaada ili kuzima madai yake kwa Barrick, ambayo kimsingi, baada ya kushirikiana na Shandong, yeye atakaa pembeni kama mwanahisa na kuwaachia wachina wakiendesha migodi yake ikiwemo hii ya Tanzania, Nickel na Uranium kupitia Uranium One.

MWISHO WAKE, BARRICK WATAISHIA NA TUTABAKI NA SHANDONG GROUP TOKA CHINA, AMBAYO KIMSINGI HATUNA MGOGORO NAO

NA ALEX MANDESY, KARAGWE- KAGERA
 

Handsome Rob

Senior Member
Jan 12, 2017
136
500
Yaan kama unafikiria wale Acacia watalipa zile pesa hahahahaaa labda kama utakua unaota..!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom