a4afrika
JF-Expert Member
- Apr 13, 2012
- 1,786
- 1,819
Unamaanisha kwamba hata watawala tulionao ni moja wa maadui wakubwa wa maendeleo yetu ya Kifikra na kiuchumi? ndio maana sasa hakuna kiongozi anaweza akatuelezea muungano wa tanganyika na zanzibar bila kutumia vitisho? na sahihi kabisa kuamini kwamba kwa muda mrefu watu wachache wametumia opportunity ya ujinga wetu kujineemesha huku wakitumbaza kwamba sisi ni wamoja? thanks to the expanding gap between the rich and the poor, sababu sasa hata dhamira zetu halisi japo ni primitive lakini zinadhihirika, no wonder why the president is very unconfortable to approach us.
Adui wetu sio watawala wetu, ila ni mfumo uliowasimika ndio adui yetu. Hakika, hakuna zao tofauti na hili chini ya demokrasia. Viongozi wetu kwa udhaifu wao walibariki mfumo huu, wengine kwa ahadi na wengine kutokujua, lakini mwisho ni huu, UNYONGE UNYONGE KILA KONA. Wameshapumbazwa, aidha kwa makombo walayo mezani mwa wanyonyaji wetu ama uvivu na ufinyu wao wa kufikiri, bado wanatuhubiria kupita njia sio. UNAFIKI WETU RAIA, UFINYU NA UVIVU WETU WA KUFIKIRI NDIO UWAPAO KIBURI. Kumbe nafsi zetu zimeshatawaliwa tayari, basi adui wako wa kwanza unayetakiwa kumshinda ni NAFSI YAKO MWENYEWE! Mshinde huyo kwanza, kwa kutafuta ukweli, ukishaupata utapigana na walioupindisha (wazungu), tutawashinda.
Mungu wetu anaita!