Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Wakati Nduli Amini anavamia nchi yetu mwaka 1978, Mwalimu nyerere aliweza kuwamobilize watanzania pamoja na majeshi yetu yakaingia vitani na kuweza kumuondoa Amini katika ardhi yetu.
Nimekuwa najiuliza kwa muda sasa, kwamba iwapo itatokea nchi yetu ikavamiwa na Taifa lolote la Jirani,Je Kiongozi wetu ataweza kutumobile watanzania na kuingia vitani kupambana na adui kama ilivyotokea 1978.
Sababu kubwa inayonipa mashaka ni kwamba, Kiongozi wetu amepoteza kabisa courage ya kutukabili wananchi wake na kutupa maelekezo, ama makaripio, ama ushauri, ama miongozi, ama ushauri n.k na hata anapopata ujasiri wa kufanya hivyo anaishia ama kwenda kujificha Studio ama kuchagua watu wachache, wazee na kuongea nao.
Kiongozi wetu amekuwa mlalamishi kama tunavyolalamika sisi, hata pale tunapotegemea kwamba yeye ndio atatoa kauli ya mwisho juu ya swala lenye utata atafanya hivyo kwa kuchelewa sana ama anaweza kuruka kabisa hiyo issue hata kwa kusema na yeye hajui.
Zaidi, nikiangali dissatisfaction ya wananchi wengi kwa utawala wake, napata shaka kama kweli anaweza akasikilizwa na wananchi wake,na hapa ndio panaponipa hofu zaidi, nabaki kujiuliza au anategemea kutumia nguvu za majeshi yetu peke yake ambayo at least mpaka sasa ndio sehemu kubwa ya Jamii yetu inayoonyesha kumtii.
Kingine ni kwamba, Hii mifarakano inayojitokeza kati ya majeshi yetu na wananchi, likitokea tatizo la kiusalama inawezekana kweli makundi haya yakashirikiana kwa kufanya kazi moja pamoja?
Kama haya hayawezekani, ni nini kinaweza kutufanya tukafikiri tuko salama dhidi ya uvamizi kutoka nje, achilia mbali dhidi ya uvamizi kutoka ndani, hapa ndio nakumbuka yaliyotokea Unguja, hivi kweli hakukuwa na mwananchi hata mmoja ambaye alipata taarifa ya mipango ya uhalifu mkubwa namna ile na kuziwasilisha kwa vyombo vya usalama?
Kwa kweli nimejawa na wasi wasi mkubwa sana, nadhani nahitaji japo maneno ya faraja.