Hivi nchi ndogo ya Rwanda imetushinda nini?

Hivi nchi ndogo ya Rwanda imetushinda nini?

Unalinganisha Kigali na Dsm au Tanzania na Rwanda?
 
No body can tell you that you are inferior unless and until you admit that yourself!

Kwa hiyo hapo wanachotushinda hao jamaa ni hayo magorofa au kuna kingine?

Ila ninachowasifu; Rwanda (read Kigali) wanajitahidi kwa usafi kwa kweli. But so is Moshi!
 
uzalendo; uwajibikaji; kujitambua;

hapa tumekalia majungu tu na ushabiki.
 
Tofauti kati ya "Rwanda ya sasa" na sisi ni UONGOZI. Kabla ya uongozi wa Kagame Rwanda ilikuwa ya kusikitisha. Baada ya Kagame kutwaa madaraka Rwanda imekuwa ya kuigwa. Funzo kwetu ni kwamba uongozi ndiyo kila kitu.

Tanzania tuko hivi kwa sababu hatujawahi kuwa na uongozi wa kiwango cha Kagame. Awamu zote wamekuwa wakijali zaidi kulindana, na hilo limeruhusu kukubuhu kwa rushwa, ubadhirifu na wizi wa mali ya uma.

There is light at the end of the tunnel.It's called the Bulldozer.
 
Uswahili ndiyo gunia letu la msumari tulilotwikwa kichwani.

Mswahili hauwezi ukakubaliana nae kitu, au kupanga nae mpango, halafu aheshimu makubaliano. Hii ni kwa mtu binafsi na imeenda mpaka katika serikali. Mikataba haieshimiki, taasisi zinajitungia sheria kila kukicha kwa kuangalia sura, watu kubaguana eti kabila fulani halifai. Hasa hili la kuangalia sura na kubatizana mzalendo au siyo mzalendo. Angalia hata post zilizotangulia na uhesabu ni mara ngapi hii dhana ya "mzalendo" imerindima. Ni uswahili na unafiki mtupu. Matendo ya mtu hayatokani na uzalendo, bali utokana na kufahamu kuwa kuna utawala wa sheria ambao utamuwajibisha akifanya makosa - hakuna malaika dunia hii.

Pamoja na hayo, Rwanda ni nchi ndogo. Mikoa yetu kama Morogoro ina ukubwa mara mbili na zaidi ya Rwanda. Rwanda kwa ukubwa naifananisha na mkoa wa Simiyu. Kama sisi tungekubali kuzipa tawala za mikoa uwezo wa kujiamulia mambo yao zaidi (ugatuzi), sii ajabu tungefika mbali pia. Badala yake tumeconcetrate nguvu zote Dar, na hata tumeanza kuwanyan'ganya vyanzo vyao vya mapato (kodi za majengo etc). Mabaraza ya Halmashauri yanaingiliwa katika maamuzi, wanafungwa mikono wanakuwa ni kazi bure.
 
the kigali cbd masterplan developed by a Singaporean office

original_81504_TJ_ksP8N7QBDscQFeqNnAAt5A.jpg


original_81504_AsQNa22haSdToMSZ3PM2PI1Mj.jpg


original_81504_8xK8g7mHufh3LGBpP0fGglq3k.jpg


original_81504_hFNGns5neENwHPvPrwt0sNMYW.jpg


original_81504__MDnn2DvEVeHQFgeBehA6o_Kn.jpg

__________________
 
Back
Top Bottom