Na vipi unapokuwa na namba ya simu ya mtu wakati yeye hajui kama unayo namba yake, siku unawasiliana naye kwa mara ya kwanza swali la kwanza ni; "nani kakupa namba yangu?". Silipendi kabisa hili swali.
Namba ya simu haiwezi kuwa siri wala ya binafsi. Kama unawasiliana na watu mbalimbali na wengine hata huwajui lakini wakitaka kukupigia au ukitaka kuwapigia unaweza. Sasa inakuwaje siri?
Nijuavyo mimi lengo la simu ni mawasiano,Inakuaje kwamba namba ya simu ionekane ni kitu cha siri sana kiasi kwamba watu wengi hukataa kuweka wazi au kupewa mtu mwengine bila ridhaa yake?
Kwani tatizo ni nini?
Du nimeipenda hiyo.Jinsi ilivyo namba za simu ulizo nazo asilimia 98 ni wale watu unaoendana nao ktk hali yako kimaisha.
Mifano:
1.anaetumia jiko la umeme hawezi kua na namba ya muuza mkaa.
2.Mvuvi hawezi kua na namba ya mchimba madini.
Labda wawe wana undugu.