Elections 2010 Hivi Mwenyekiti NEC aliwahi Kujibu Barua ya Mwanakijiji ya Agosti 27?

Mtu wa Mungu

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
444
19
WanaJF naomba mwenye taarifa anisaidie hapa!!!!!!!!!! Comment zangu kwa barua hiyo ni hizi hapa!!!!!!!!!
MwanaJF M. M. Mwanakijiji naungana na Great Thinkers WanaJF kukupongeza kwa kuchukua nafasi ya kipekee kuelimisha umma wa Tanzania juu ya mada hii ya msingi kuhusu haki ya msingi ya kila raia wa Tanzania. Kwa unyenyekevu mkubwa natoa pongezi kwa kila mwanaJF aliyechangia na kuipa mada hii umuhimu wa kikipekee!!.
Mimi kwa mara ya kwanza nilisoma makala yako katika gazeti la Mwanahalisi, Jumatano, Septemba 17, 2010, Ukurasa wa 6 kichwa "Wabunge Waliobebwa ni Batili". Kwa thread hii ya leo nimetiwa moyo zaidi kuona kwamba kumbe ulikwishafika mbali zaidi kwa kumwandikia Barua ya Wazi Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi mapema zaidi, Agosti, 27, 2010. Huu ni ushahidi tosha ni kiasi gani umetoa maisha yako kuona haki ya msingi si jambo la kufanyia mchezo katika taifa hili. Jitihada zako pia zimeonekana kwa kutuhabarisha juu ya hatua aliyofikia Rev Mtikila kwa mujibu wa gazetila IPP MEDIA Nipashe Jumatatu, Novemba, 22, 2010.
Kwa wanaJF wenye memory wanaweza kukumbuka miaka ya zamani sana katika jimbo moja la uchagu, kama sikosei, Korogwe?, ambapo wapigakura 2, kitu kama hicho, waligangamala mahakamani mpaka mbuge aliyekwisha dumu bungeni kwa muda mrefu kuvulivuliwa na mahakama ubunge!!!.
Hili ni somo kwetu kwamba kama watakuwepo wapigakura wenye uchungu ambao hawatakuwa tayari kuona na kunyamazia serikali ya sisiemu ikinyang'anya kidhuluma wapigakura halali katika majimbo ya uchaguzi 19 haki yao ya kikatiba!!!. Hiki ni kitendo cha kinyama!!!!!!!!!!!!!! kwa nchi inayopigia debe kuendesha utawala wa kisheria; na hata kuwa na Tume ya Haki za Binadamu!!!!!!!!!!!
Mimi naungana na wanaJF ambao wametupeleka katika hatua za kufungua kesi mahakamani kwa hoja za msingi bila kujali kwamba mahakama zitachakachuliwa au la. Hatuwezi kujua; Mungu anaweza kutuinulia majaji mfano wa marehemu Mwalusanya, na wengineo waliotoa maisha yao kuona haki inlindwa kwa gharama zote. Itakuwa ni kosa la kujutia kama tutaishia tu kwa hisia za mahakama kutotenda haki. Lalamiko la namna hii lije pale ambapo kesi imechakachuliwa, au haki imecheleweshwa!!.Aidha tusiogope gharama. Penye nia pana njia!!!!!!!!!!
Pia naungana na wanaJF walioleta wazo la kuhamashisha vyama, hasa CDM ambao ni victim mkubwa- na pia taasisi zote za Haki ya Bindamu, pamoja na ile ya serikali-ile ya Jaji Manento!!!!!!!! Seriousness katika uhamasishaji itaipa jambo hili kuvuta hisia za watu wengi na taasisi nyingi na kulifanya jambo hili kuonekana kupata uzito kitaifa na hata kimataifa ili kupata msukumo wa kufanya wabunge husika kujutia tendo hilo !!!!!!!!!
MwanaJF Mwanakijiji naomba ukubali jukumu la kutuongoza katika mipango ya kufungua kesi, na uhamasishaji!!!!!!!!!
progress.gif

Edit Post Reply Reply With Quote Thanks :target::target::target::target::target::target:
 
Back
Top Bottom