Hivi mwanamke bora katika ndoa ni yupi shostito...? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi mwanamke bora katika ndoa ni yupi shostito...?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Msindima, Sep 2, 2009.

 1. M

  Msindima JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Anayejua kuvaa, anayejua kujikwapua, anayejua kujishau, anajua kujichubua au anayejua kula hela ya mumewe vizuri...!?
  Kwa mujibu wa wataalam wa mambo haya mwanamke bora katika ndoa ni ....

  1.Anayejua mumewe anataka nini.
  Wanasema mke mwema ni yule anayejua kumsoma mumewe na akamjua ipasavyo.

  Unajua mara nyingi hawa wenzetu wanatarajia wafanyiwe mambo sahihi, na pale wanapotenda yale ambayo hayakongi hisia zao, hujawa na hasira au kuvunjika moyo. Ukijifunza kumjua na kujua mazuri na mabaya katika mapenzi yake utasimama tofauti kati ya wale anaokutana nao barabarani na wewe uliye mkewe.

  2. Anayekubali kujishusha
  Kila mtu ana asili ya kujiona yeye ni bora kuliko mwingine, lakini lazima ufahamu kuwa kujishusha hakumaanishi kuwa unapunguza ubora ulionao. Wanaume wanapenda kujihisi wao ni kichwa katika nyumba. Mpe nafasi hiyo, ikibidi kujishusha ili yako yakwendee ...Hewallwa. Kujifanya mbishi na mjuaji unamfanya aamini alikosea kukuchagua wewe kuwa mkewe. Upo shosti.

  3. Anayeridhika na alichojaaliwa...
  Si busara kumnanga mwanamme wa watu kila siku kwa kile ambacho ameshindwa kukufanyia.

  Wapo wanawake ambao huamini kuwa kwa kumkera mumewe kuhusu vitu fulani wanaonyesha uhodari waojuu yao. Lakini ukweli unabaki pale pale kuwa kama huridhiki na ulichojaaliwa nacho huto kaa uridhike.

  4. Anayejua kunyenyeekea... Wanasema unyenyekevu ni mbolea ya mapenzi, kila mwanamme angependa arudi kwake akute faraja na si karaha. Unyenyekevu hapa hucheza nafasi nzuri katika mapenzi kwa kuonyesha hisi zako wa mwenzako na kumfanya ahisi kuwa yeye ndiye yeye.
   
 2. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,242
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Yatosha uloandika kumpata mke bora.
  Sababu ya 1-4 safii,ila kama kuna nyengeza ni kuboresha zaidi.

  Swadaktaaa!!
   
 3. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  nafikiri mke mwema anatoka Mithali 31 Hayo yote mnayoandika si sahihi. Ni mambo ya kiulimwengu.
   
 4. Shishi

  Shishi JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,244
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  I love the P31 wife....that one existed only those days...leo hakuna chako....ati she never tires, is the first to rise and last to retire blah blah blah...Mr wangu anaipenda sana hii statement .. eti he's waiting for the p31 wife..atangoja sana ahahahhaha!
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...mbona 'hauz-geli' anaweza?
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Vile vile anayejua kujiexpress
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Sep 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Mwanamke bora katika ndoa ni yule anayejua role yake na si yule anayetaka kuwa au anaye act kama mwanamme.
   
 8. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Amen hii inahusika sana otherwise kuna uwezekano wa kumpata mke kimeo hata kama ana sifa zote hizo hapo juu
   
 9. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mke mwema lazima atambue kuwa mme ni kichwa cha familia na vile vile atambue role yake katika familia.
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  huyu atakuwa mke kweli tena kaka?
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Tufafanulie tafadhali NN
   
 12. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hawa wenye utambuzi huu nasikia siku hizi wamekwisha kabisa
  wako kwa uchache sana hapo kwetu Umasaini ingawa in the long run nako wanategemewa kwisha na kubaki kuwa na vichwa viwili vya nyumba hadi pachimbike hapo. Heri yao waliokwisha maliza game hii hapa na wanacelebrate at least 10 years ya ndoa zao
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Mkuu ndo maana wengi wa wanawake wanajifanya wana haki kama wanaume lakini wanasahau mwanaume hawezi kubeba mimba sasa sijui haki wanayolilia ni ipi mwanamke abaki kuwa mwanamke na mwanaume abaki hivyo hivyo. Unafikiri kwa nini ndoa nyingi zinaenda kwa kuchechemea? Hiki ndicho kinacho watafuna wengi.
   
 14. nkawa

  nkawa Senior Member

  #14
  Sep 2, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nahisi wewe ni mwanaume tena usie na huruma........mke awe kama house girl yaani afanye kazi zote za usafi na kupika ndani, awe ni mke...akutimizie mahitaji yako yote, awe ni mama awajibike kwa watoto, na bado awe mwaajiriwa...awajibike kwa boss wake....atapona kweli!!!!!!!!!!!!!!!!

  Housegirl hapo wajibu wake ni mmoja tu....naamini nae akiolewa hataweza vyote atatafute housegirl wakumsaidia...upo hapo
   
 15. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #15
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu mimi siku hizi siongei sana kwani ukiongea sana anatokea WOS anakwambia acha porojo. Ila kimsingi ulichokizungumza hawawezi kukikwepa. Wenyewe wanasema Feminist Transfomation. Mwanamume atabaki kuwa mwanamume na mwanamke atabaki kuwa mwanamke. Kwa maana hiyo lazima mke amuheshimu mume hiyo imempasa na wala sio hiari
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Sep 2, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,655
  Likes Received: 35,417
  Trophy Points: 280
  Lakini swala la heshima ni la wote. Wote inabidi mheshiane sawa. Siyo mmoja apewe heshima kuliko mwenzake...what kinda BS is that?
   
 17. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Kweli mzazi hapo umelonga unajua wanawake iwa wanakurupuka tu oooh tumetoka Beijing haki zetu lazima ziheshimike unajua sisi ni Waafrica tuna mila na desturi zetu asilia ndo kama hivyo mme anatambulika kama ndo kichwa cha familia lakini hapo hapo utakuta wanawake wengi baada ya kunogewa na tamaduni ambazo si za Kiafrika wanaanza kulazimisha mambo na mama kujiona kama ndo kichwa wa familia ndani ya familia katika maamuzi na kila kitu kunatokea misuguano ndani ya familia na hawataki kujishusha.
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hili nalo neno zuri
   
 19. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135


  Hapo Sipo umekosea, katika kipengele cha heshima inapasa kila mmoja amuheshimu mwenzako.
   
 20. Kaniki1974

  Kaniki1974 JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 352
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Haya yana ukweli kwa kiasi kikubwa.......japo muhimu pia si kuigiza bali kuwa halisia.
   
Loading...