Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

Hivi Mwakyembe ana power kuliko Pinda?

Ukishapewa Kagold cha 20g na ukapigiwa kangoma cha FISI utaweza kumuwajibisha nani? Wapi?
 
Wana JF, nimekuwa katika mawazo mazito sana toka Dr. Mwakyembe aanze kushughulikia sakata la ATCL. Hili jambo limejadiliwa sana hapa jamvini. Wengine wakisema Mwakyembe kakosea wakati wengine waki-support. Hoja yangu iko tofauti na hili. Siko upande wowote wa mjadala huu.

Mara nyingi sana tumeshuhudia au kusikia Pinda akichelea kuchukua hatua juu viongozi waiopatikana na makosa kwa kisingizio kuwa anayepaswa kuwachukulia hatua za nidhamu ni Rais!!

Sasa Mbona Dr. ameweza kuwachukulia hatua hawa vigogo wa ATCL? Pinda, ambaye ni boss wa Dr, anashindwaje kuwachukulia hatua vigogo wa aina hii?

Je hii inathibitisha ile imani ya kuwa Pinda ni mwoga au dhaifu? Au hawa vigogo wa ATCL waliochukuliwa hatua za nidhamu na Dr ni tofauti na wale ambao Pinda anawaogopa?? Au Dr ni jasiri zaidi ya Pinda? Au ni nini?

Nawasilisha!

Ni tabia ya CCM kushughulika na sisimizi na kuwaacha vinara wa ufisadi, kama kweli Dr Mwakyembe alikuwa na ubavu ni kwanini ameiacha Bodi ya ATCL inayoongozwa na Na Mustapha Nyang'anyi mmoja wa viongozi toka enzi za Mwalimu Nyerere na mmoja wa vinara wa ufisadi hapa nchini kwa kushirika katika kashafa ya ununuzi wa kivuko kibovu cha Kigambani kilichokuwa kikijulikana kama UNIFLOTE. Hata katika kashafa ya Richmond ni huyu huyu Mwakyembe aliyamua kuficha ukweli wote na badala yake kumkomalia sisimizi Lowassa.
 
Back
Top Bottom