Hivi Musa alikuwa Myahudi au Mwarabu?

Musa alimwabudu MUNGU aliye hai ambaye alijitambulisha kama Mungu wa Baba yake Musa, Mungu wa Ibrahim, Mungu wa Osaka, Mungu wa Yakobo. Kutoka 3:6. Musa alipomuuliza Mungu kuwa akamueleze farao ametumwa na Mungu yupi, Mungu alimwambia akaseme ametumwa na MUNGU aitwae "Mimi Niko ambaye Niko".. Kutoka 3:14..
Uyo ndo mungu aliewapora wamisri baraka zao.
 
Yaani muislam au mjewish(mjuda)?

Majibu tafadhili.

Update
Musa alikuwa ni muebrania(moja ya kabira la wayaudi)
Na aliwaongoza wayaudi kwenda israel kwa imani ya wayaudi. Yaan Mungu alietenanisha bahari na aliewalisha mda wote
Na ikumbukwe hakuna myaudi muislam
Na kihistoria alienzisha au kukuza uislam ni Mohammad na uislam haukuepo enzi hizo
Kuna wengine wanafika adi hatua ya kusema Adam alikuwa muislam. Cjui maantiki yao ni wap. Na upande wa kuchoma kondoo ili kuondolewa dhambi je??
Duu,umeanzisha uzi,ukauliza swali mwishowe ukajijibu mwenyewe. Hongera sana.
 
Musa alikuwa Muisraeli tena wa uzao wa Lawi ambao ndiyo waliokuwa makuhani katika hekalu la maturubai . Uislamu umeanza miaka mia sita baada ya Ukristo kuanzia pale Antiokia. Wakati wa Musa, Uislamu haukuwepo, ila waarabu (wamidiani) walikuwepo na walikuwa wakiabudu miungu.
Swali halijauliza dini. Kama ni dini hata Ukristo haukuwepo. Swali limeuliza ni Mwarab au Myahudi? Umejibu kisichoulizwa. Uarab siyo Uislam,kwani wapo Waarab Waislam,Wakristo na wasioamini.
 
Changanya na zako. Ndo kiki zenu siku hizi? Kwa hiyo wakati Ukristo unaanza wenyewe ulikuwa wapi?
Hakuna dini ukristo umetokana na jina la cheo cha mwana wa mariam Yesu. Masiah. Umasiha =ukristo kigiriki. Ufuasi wa mteule. Mteule mwenyewe ni muislam anaye abudu mungu mmoja elohi elohi Allah allah
 
This

is 100% truth. Ni afadhali uuamini na uchukue hatua kuliko kushikilia kejeli ulizorithishwa na waamini mashetani na majini mwisho ukutane na Yesu mbele ya hukumu. Maana imeandikwa, mbele ya yesu Kila goti litapigwa. Shauri lako
Yesu mwenyewe Alipigwa. Mi niko na mungu mwenyeenzi mwenye nguvu Yesu nabii kama manabii
 
Yaani muislam au mjewish(mjuda)?

Majibu tafadhili.

Update
Musa alikuwa ni muebrania(moja ya kabira la wayaudi)
Na aliwaongoza wayaudi kwenda israel kwa imani ya wayaudi. Yaan Mungu alietenanisha bahari na aliewalisha mda wote
Na ikumbukwe hakuna myaudi muislam
Na kihistoria alienzisha au kukuza uislam ni Mohammad na uislam haukuepo enzi hizo
Kuna wengine wanafika adi hatua ya kusema Adam alikuwa muislam. Cjui maantiki yao ni wap. Na upande wa kuchoma kondoo ili kuondolewa dhambi je??
Haya umeyatoa kitabu gani, Maana Qur'an haisemi hivyo usitumie kitabu cha Chinua Achebe ukauelezew Uislamu mkuu.
 
Nilidhani waislamu wanapoambiwa elimu ilipita mgongoni nilidhani uongo Kumbe kweli. Waislamu ni Shida elimu Hakuna na ht hekima ht kdg hakna. Waislamu kila jambo ni nguvu na kila jambo kwao ni hadithi za kukaririshwa
 
wapo wayahudi wengi waislam na wakati wa mtume mohamad wengi waliingia dini ya kiislaam nabii musa ni muislam manabii wote walikuwa waislam kwanza ujue nini maana ya uislam halafu soma quran sura inaitwa alimran mungu anasema hakika dini kwangu ni islam
 
Ni vizuri kumjua huyo Musa kwanza ni nani.

Musa alikuwa kiongozi wa Wana wa Israel na Mwanzilishi kwa maelekezo ya Mungu wa utaratibu wa sheria za Ibada ya Wana wa Israel, Dini inayoitwa leo ya Kiyahudi, Judaism. Kiebrania anaitwa Moshe Rabbeinu maana yake Moshe Our Rabbi(Musa Mwalimu Wetu wa Dini).

Namba ya Musa kiyahudi, Moshe Rabbeinu ni 613 ambayo pia imelingana na idadi ya sheria/maagizo (mitzvot) ambazo Mungu kupitia Musa aliwafundisha wana wa Israel kuzitimiza.

Musa ni binadamu pekee ambaye alionana na Mungu uso kwa uso, Kumbukumbu Ya Torati 34:10, na kuongea nae moja kwa moja live, Hesabu 12:8.

Musa alizaliwa mwaka wa Kiyahudi wa 2368 baada ya uumbaji, tarehe 7 ya mwezi wa kumi na mbili (adar) kwa kalenda zetu unaangukia mwezi wa pili na wa tatu.

Musa alikuwa mtoto wa Mzee Amram na Mkewe Yokebedi, wana wa Israel wa kabila la Lawi. (Kutoka 6:16-20), (Kutoka 2:1-2). Musa alizaliwa wakati wakati Mama yake akiwa na umri wa miaka 130.

Baba yake alimpa jina la Chaver(rafiki) na Babu yake akampa jina la Gedori (Avigdor). Binti wa Farao baada ya kumfanya mwanae alimpa jina la Minios, yawezekana kutokana na mazingira aliyompata mtoto Musa, kumuokota mtoni,Kutoka 2:10, jina la Minios lina maana ya "toa nje", Moshe ni tafsiri ya kiebrania ya jina hilo la Minios ambalo kwa kiswahili ni Musa.

Musa alizaliwa katika kipindi kigumu sana, kipindi ambacho Farao alikuwa ametoa agizo kuwa watoto wote wa kiume wa Waebrania (watoto wa Israel) wauwawe, kipindi hiki Wana wa Israel walikuwepo utumwani Misri.Kutoka 1.22. Mama yake Musa alifanikiwa kumficha mtoto wake huyu kwa kipindi cha miezi 3, baada ya kipindi hiki akamtengenezea maficho mtoni, mahala ambapo binti wa Farao alimpata, Kutoka 2:6. Kwa ushauri wa dada yake Musa, Miriam, binti Farao alimuajiri Mama yake Musa, Yokebedi kuwa yaya wa mtoto Musa, Mama huyu sasa akiwa yaya wa mwanae na bila binti wa Farao kujua ndiye akamjenga Musa kujitambua yeye ni nani na ndugu zake ni akina nani, na kujenga upendo kwa ndugu zake Wana wa Israel waliokuwa utumwani Misri, yeye akiwa Ikulu ya Farao.

Machache yanajulikana juu ya maisha ya utoto ya Musa ndani ya Ikulu ya Farao, biblia haijaeleza sana juu ya hili, kwa historia ya kitamaduni za Kiyahudi, kuna habari kuwa pindi Musa alipokuwa kijana mdogo ndani ya Ikulu ya Farao, siku moja alikwenda na kuketi miguuni mwa Farao pindi Farao akiwa kwenye kiti chake cha kifalme pamoja na Washauri na Waganga wake na Musa akamvua Farao kofia yake ya Kifalme kimchezo tu kama Babu achezaye na mjukuu wake.

Kitendo kile kwa tasfiri ya waganga wa Kimisri waliokuwa pamoja na Farao ilikuwa ishara mbaya ya uasi wa Musa dhidi ya Farao. Hili kuthibitisha kiu ya utawala ya Musa mbele ya Farao kabla ya kumuangamiza, wakamuwekea Musa mbele yake bakuli kubwa ya mkaa unaowaka na bakuli kubwa ya dhahabu safi ya Farao. Kama Musa akichukua dhahabu ya angepaswa auawawe maana ingethibitika sio mwaminifu kwa Farao na ana uchu na Ufalme wa Farao. Lakini kwa msaada wa Malaika na kwa mshangao wa wote, Musa alichagua kuula mkaa wa moto mdomoni mwake badala ya kuchukua dhahabu ya Kifalme, kitendo hiki kilimuepusha na kifo siku hiyo lakini kilimpa kilema cha mdomo, toka siku hiyo Musa hakuweza tena kuongea vizuri, Kutoka 4:10.

Kufupisha, Musa alichaguliwa na Mungu kuwaongoza Israe kuelekea nchi ya ahadi, Kutoka 3-4, aliwaongoza wana wa Israel kwa miaka takribani 40 kueleka nchi ya ahadi, Kanaani, na Mungu alimpa Musa torati kwa niaba ya Wana Israel, Kumbukumbu ya Torati 12:24.Torati ambayo Musa aliwapata wana wa Isarel, torati ambayo kwa ujumla wake ina vitabu vitano, Mwanzo, Kutoka, Walawi, Hesabu na Kumbukumbu ya Torati.

Maagizo mengine ya mdomo, oral tradition, yanapatikana pia kwenye historia na tamaduni za wana Isarel, talmud. Musa hakuingia nchi ya ahadi, Kumbukumbu ya Torati 32:48-52.

Japo Mungu alimuonyesha Musa nchi hiyo ya ahadi ya Wana Israel akiwa mbali. Kumbukumbu ya Torati 34:4 " BWANA akamwambia hii ndio nchi niliyowaapia Ibrahiu, na Isaka na Yakobo nikisema, nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko" . Ni nchi hii ambayo leo Wana wa Israel, watu wa Musa, wanapigana na Waarabu kuihusu.

Musa alifariki juu ya mlima Nebo mwaka 2488 akiwa na umri wa miaka 120, Kumbukumbu ya Torati 34:7, kuepuka Wana wa Israel kuliabudu kaburi lake, Musa hakuonekana tena baada ya kwenda mlimani ambapo ndipo alipokufa na kuzikwa na Mungu mwenyewe bila wanadamu, mwili wake haukuwahi kuonekana. Kumbukumbu ya Torati 34:5-6.Yoshua Mwana wa Nuni alichukua uongozi wa Wana Israel baada ya Musa, kama Mungu alivyomuagiza Musa, Kumbukumbu ya Torati 34:9.

Maneno ya mwisho ya Musa (Moshe Rabbeinu) yalikuwa haya: Kumbukumbu ya Torati 33:29
"U heri, Israel. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na Bwana! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahala pao pa juu."

Huyu ndiye Moshe Rabbeinu, shujaa wa wakati wote wa Israel, Mtumishi Mwaminifu wa Yehova, Mungu wa Ibrahimu, Mungu wa Isaka na Mungu wa Yakobo.
Umedadavua vƴema mkuu
 
Yaani muislam au mjewish(mjuda)?

Majibu tafadhili.

Update
Musa alikuwa ni muebrania(moja ya kabira la wayaudi)
Na aliwaongoza wayaudi kwenda israel kwa imani ya wayaudi. Yaan Mungu alietenanisha bahari na aliewalisha mda wote
Na ikumbukwe hakuna myaudi muislam
Na kihistoria alienzisha au kukuza uislam ni Mohammad na uislam haukuepo enzi hizo
Kuna wengine wanafika adi hatua ya kusema Adam alikuwa muislam. Cjui maantiki yao ni wap. Na upande wa kuchoma kondoo ili kuondolewa dhambi je??


Waarab ni kizazi kilicholaaniwa kwa sababu baba yao Ishmael alikuwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Avram (Abraham) alizaa Ishmael na yaya wake (beki tatu wake) aitwaye Hagar ambaye alikuwa Mmisri. Kwa wayaudi, mtoto wa pembeni anahesabiwa kuwa ni mtoto wa laana (forbidden child) na ndiyo maana myaudi hataki hata siku moja kutawaliwa na kizazi kilicholaaniwa. Hii ipo kwenye historia, ila watakuja watu wasiojuwa historia na kutaka kuniua mimi au kujiua wao wenyewe kwa kukata ukweli. All in all, hizi dini hazituhusu...sie tuliletewa tu kwenye maboti.....tuwaachie wenyewe waarab na wayaudi wapiganie dini zao.
 
Waarab ni kizazi kilicholaaniwa kwa sababu baba yao Ishmael alikuwa mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa. Avram (Abraham) alizaa Ishmael na yaya wake (beki tatu wake) aitwaye Hagar ambaye alikuwa Mmisri. Kwa wayaudi, mtoto wa pembeni anahesabiwa kuwa ni mtoto wa laana (forbidden child) na ndiyo maana myaudi hataki hata siku moja kutawaliwa na kizazi kilicholaaniwa. Hii ipo kwenye historia, ila watakuja watu wasiojuwa historia na kutaka kuniua mimi au kujiua wao wenyewe kwa kukata ukweli. All in all, hizi dini hazituhusu...sie tuliletewa tu kwenye maboti.....tuwaachie wenyewe waarab na wayaudi wapiganie dini zao.
dhabi haizai dhambi ..
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom