Hivi mtumishi mchapakazi mwenye vyeti feki anaweza kufukuzwa kazini?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
jamani kuna mjadala mzito kuhusu uhakiki wa vyeti maofisini vya wafanyakazi hii iwe serikalini au sekta binafsi.

hivi mfano ikitokea katika uhakiki ukagundua mmoja kati ya wafanyakazi amefoji vyeti lakini mtu huyu aliyefoji vyeti akiwa ofisini ni mtendaji mzuli na ni mchapakazi mzuri akiwa kazini.

sasa swali langu jee mtu kama huyu unaweza kumsimamisha au kumfukuza kazi kwa kufanya udanganyifu na kufoji vyeti hebu tusaidiane
 
Ni wa kufukuza tu maana atakua anafanyia experience na siyo taaluma. The problem is, hawaezi kubuni kitu kingine ambacho kitaikomboa kampuni na kuiinua zaid ya kufanya Yale Yale ya kila siku kwa mazoea.

For a company to grow,it needs a new idea na ubunifu kila uchwapo.
 
Hakuna mbadala wa cheti feki.
Hizo kazi ingekuwa bora angezichapa vizuri shuleni ili zilete cheti halali.
Lakini yawezekana maisha yalikuwa magumu wazazi wakashindwa kumpeleka shule au shule zetu za vijijini ambazo zilikuwa na waalimu wawili na hata mwamko wa elimu haupo.

Sio lazima aendelee kuwa hapo kazini. Mtu mchapakazi hata umchukulie kila kitu anaweza kuanza upya na ndani ya Muda mfupi akarudia hali yake ya zamani. Mlango Ukifungwa Unapitia hata dirishani. Yawezekana dirisha likawa ni Duka,Shamba au Biashara.
 
Ni wa kufukuza tu maana atakua anafanyia experience na siyo taaluma. The problem is, hawaezi kubuni kitu kingine ambacho kitaikomboa kampuni na kuiinua zaid ya kufanya Yale Yale ya kila siku kwa mazoea.

For a company to grow,it needs a new idea na ubunifu kila uchwapo.
Jidanganye,waangalie mtaani wanavyoweza kubuni vitu na wanafanikiwa na kukuacha nyuma wewe unaesema ni msomi,cheki miradi yote inayopangwa na hao wasomi hata ktk miradi ya maendeleo ya jamii maofisini wanakesha wanaandika miradi na pesa zinatoka serikalini au kwa watoa misaada huko nje,chek hyo miradi hua inaishia wapi,wanaandika vzr sana kushawishi pesa zije na mwishowe hawawezi simamia au walichoandika walidanganya ni kitu kisichowezekana ktk jamii na kinakuja kufeli.sasa nenda kwa unaowaponda kua hawakusoma uone miradi yao wanayobuni,hii haimaanishi kua wasomi hawana maana hapana.ila najaribu kukupa uwazi kua usijalibu kudharau mtu mwenye hajasoma vzr ila pia ana akili.
 
Km huna cheti ina maana huna vigezo halina mjadala
hapa nina maana kama kuna mtu anafanya kazi lakini pia kazi za kampuni anazifanya katika ustadi wa hali ya juu na analeta unaweza ukamtoa ofisini kwa kigezo cha cheti
 
Ni wa kufukuza tu maana atakua anafanyia experience na siyo taaluma. The problem is, hawaezi kubuni kitu kingine ambacho kitaikomboa kampuni na kuiinua zaid ya kufanya Yale Yale ya kila siku kwa mazoea.

For a company to grow,it needs a new idea na ubunifu kila uchwapo.
sasa mfano mtu kama huyu mwenye cheti feki lakini production yake ndani ya ofisi ipo juu sana na anachapa kazi na kuleta faida hivi unadhani kumwondoa kazini kwa kigezo cha cheti ni sawa
 
hapa nina maana kama kuna mtu anafanya kazi lakini pia kazi za kampuni anazifanya katika ustadi wa hali ya juu na analeta unaweza ukamtoa ofisini kwa kigezo cha cheti

Kama hana cheti halali ina maana kafanya udanganyif
 
Ni wa kufukuza tu maana atakua anafanyia experience na siyo taaluma. The problem is, hawaezi kubuni kitu kingine ambacho kitaikomboa kampuni na kuiinua zaid ya kufanya Yale Yale ya kila siku kwa mazoea.

For a company to grow,it needs a new idea na ubunifu kila uchwapo.
Hivi mtu aliyefoji cheti hawezi kuwa na new ideas na ubunifu?
 
kama ingekuwa ndio wewe umeajiri mtu kama huyu na mbaya zaidi unakuta ofisi ndio inamtegemea kwa ufanisi wake katika kazi jee unadhani unaweza kumsimamisha kwa kigezo cha cheti

Kwani hamna wengine wanaoweza kufanya hiyo kazi kwa ufanisi?

Km mm nliamua kukgua vyeti basi nitmuondoabyeyote asiyekuwa na cheti bila kujali ufanisi wake
 
Kwani hamna wengine wanaoweza kufanya hiyo kazi kwa ufanisi?

Km mm nliamua kukgua vyeti basi nitmuondoabyeyote asiyekuwa na cheti bila kujali ufanisi wake
inawezekana wakawa wapo lakini ni vigumu kufanana na yeye maana unakuta huyu huyu mwenye cheti feki unakuta ana experience na kazi muda mrefu.

na kibaya zaidi unakuta hawa wenye vyeti wanaokuja kazini wamefundishwa kazi na aliefoji cheti na huyo aliyefoji cheti hawa wengine wakikwama katika kazi wanamtegemea huyu aliyefoji cheti kwa maana ana uzoefu wa muda mrefu na ukitokea umemuondoa katika kazi basi ofisi inaweza ikayumba na mwisho wa siku atayekuja kushika hii nafasi basi hatakuwa na uwezo kama huyu aliekuwa mwanzo katika kazi
 
Kama yule Doctor wa Kenya, alikuwa ndio tegemeo pale Hospital hata kama yuko nyumbani ikitokea issue kubwa kazini wanamuita kazini. Uhakiki wa vyeti ulikuja mpeleka police.
 
Mimi nampandisha cheo,,,,! Kwa sababu kama anaweza bila kusomea ina maana huyo ni "genius."
 
jamani kuna mjadala mzito kuhusu uhakiki wa vyeti maofisini vya wafanyakazi hii iwe serikalini au sekta binafsi.

hivi mfano ikitokea katika uhakiki ukagundua mmoja kati ya wafanyakazi amefoji vyeti lakini mtu huyu aliyefoji vyeti akiwa ofisini ni mtendaji mzuli na ni mchapakazi mzuri akiwa kazini.

sasa swali langu jee mtu kama huyu unaweza kumsimamisha au kumfukuza kazi kwa kufanya udanganyifu na kufoji vyeti hebu tusaidiane
Uchapakazi wake hauhalalishi ufeki wake na ufeki wake ndio chanzo cha uchapakazi wake
 
Back
Top Bottom