Elihuruma Lwinga
Member
- Jun 3, 2014
- 63
- 68
Nina maswali mengi najiuliza, lilikua uhakiki wa vyeti feki, wakawekwa hadharani, na kutimuliwa makazini, na sasa wanaingia uhakiki wa waliofoji umri, yaani waliopunguza umri, swali langu je kama mtu alipunguza au aliongeza umri si juu yake? Kumbe ni kosa kujiongezea Lwinga ila mzee anaitwa Peerre, ukaamua kutumia la Pierre badala ya Lwinga unatumbuliwa.
Huu uhakiki unawaweka njiapanda baadhi ya wananchi ambao wengi tunasubiri ajira, mfano kuna wengi waalimu wamemaliza ualimu wameamua kusomea fani nyingine ya kujilazimisha maana aliipenda ualimu na kazi bado, kuna wengi walisoma fani mbalimbali ila serikali imesitisha ajira sababu ya uhakiki wa vitu vingi, bado kuhakiki wagonjwa makazini, ugonjwa ninaousema hapa ni ule wa kuwa mvivu kazini either kufanya kazi au kuchelewa au kudoji kazini sababu mkuu unayemuogopa kasafiri au ambao wanakauli mbaya kwa wateja na hata kwa viongozi au kwa wafanyakazi wenzao, wachafu yaani anaenda kazini na nguo chafu, au wanaenda huku hawajaoga yaani pafume ya jasho inakua kero kazini.
Najiuliza huu uhakiki utaishi lini? Na je unaweza ukaisha kabisa? Na ukiisha je ajira zitaanza kutolewa? Na je huko juu hakuna aliyefoji cheti? Je mkuu akiwa amefoji kitu chochote atatangazwa kama wengine hadharani? Na je waalimu wanataka kufanyiwa uhakiki wa uwezo wao wa kufundisha, je ndo suluhisho la Elimu nchini kufanya vizuri?
Ni maswali yangu mafupi tu.
Elihuruma Lwinga wa Mbeya