Hivi mtu asipopiga nyimbo ya msanii fulani kwenye kituo chake kosa liko wapi?

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu habari zenu?,
Hivi inakuwaje hapa radio ya kwangu mimi ,nimesota nimeianzisha mimi ,nikaweka utaratimu wa kuwa na piga nyimbo tu za wasanii ambao mimi kwa mtazamo wangu naona watanisaidia kukuza radio yangu, na pia nakuwa nafanya nao biashara natembea nao mikoani wanaimba nawalipa wananiingizia pesa.

Msanii akisema nampa hela ndogo kulingana na jina lake akataka hela nyingi na wakati mimi naona kabisa hapa napata hasara na temana nae huyu sio mtu wakufanyanae biashara sasa.nikifanya biashara kwa hasara mbona nitafirisika kisa kumlizisha mtu.

Kama unataka hela nyingi basi na mimi sipigi nyimbo zako,kwa sababu naona hauna faida kwangu kwanini unichukie na useme nimekudhurumu na wakati tulikubaliana ukalizika,hakuna mtu ataye kubali kufanya biashara kwa hasara,nikifuria mnicheke nimefuria .

sema kingine mnakuwa mnataka maisha ya juu sana ulichokuwa unapata ndio ulichostahili mbona kama mnaladhimisha hivi na wakati hamna hadhi hiyo.

swala la me kutokupiga nyimbo yako kwenye radio yangu,elewa kwamba hiyo ni redio yangu na mimi na fanya biashara kama umechuja kwa nini niangaike na wewe anatafutwa mwingine anayeweza ,Naendelea kufanya nao biashara .

Sasa kwa mtazamo wa kituo nyimbo yako ni mbovu watu hawaipendi niipige sana yanini sasa watu watakuwa hawaisikilizi hiyo radio yangu kama nitakuwa napiga nyimbo nzuri watu watakuwa wanapenda kuisikiliza na kuifatilia.

Mziki ni biashara mbona wewe unanyotaka kuninyonya mbona me nakataa na wewe kwanini usikatae ukapambana kivyako kama mimi nimeamua kupambana kivyangu yaani nyimbo yako na hadhi yako unasema kubwa umekataa hatuwezi kufanya biashara mbona mimi nimekubalikupambana na hali yangu kwa kutokusika kwa nyimbo zako ambazo unasema ndio bora watu wanataka kuzisikiliza,wewe mbona autakikupambana hali yako? ,umesikia hiyo radio ni ya serikali au ni ya familia yako?

Jiongeze usijenge chuki zisizo kuwa na maana mbona hiyo hela mnayosema ndogo mbona wengine wanafanya maendeleo.

Unatakiwa uelewe kwamba mimi natafuta maisha kama wewe na sio bosi,na hela nyingi haipatikani kila hisi hivyo mnavyo fikilia.

Radio ya kwangu mwenyewe nimeiangaikia mwenyewe halafu wewe unatoka usipojulikana unanipangia hata kama nakuona umefuria kabisa eti nipige nyimbo zako, hakuna kitu kama hicho .
Hata kama nitaweka kwenye kituo changu cha radio ndugu au watu wa kabila langu ,elewa radio ni ya kwangu ikifa nitanyoshewa kidole mimi wewe autausika.

Nisipo piga nyimbo yako kwenye kituo changu cha radio kosa liko wapi? hi hayo tu wakuu
 
Alishafanya, nakumbuka kuna siku aliwahi kuagiza siku nzima isipigwe bongo fleva kwenye hiyo redio na hazikupigwa kweli. Huku vijana wake wakiteleza siku nzima na msemo wa "bosi kasema".

Anyway, pumzi zisitutie kiburi na kujikuta tunajiropokea hovyo. Hapo umesema vipi ukiamua kuweka wafanyakazi wote ambao ni kabila lako, sawa unaweza, lakini hebu jaribu kuweka tangazo la kazi na moja ya sifa ya muombaji iwe ni kabila uone utakavyofuatiliwa. Haiwezekani kila mtu ajiendeshe anavyotaka, haiwezekani. Hii ni nchi.

Kuhusu upige nyimbo ya nani na ya nani usipige, hakuna shida, unaweza ukachagua utakavyo, chamsingi tuone wasanii wetu wanabadilika kupitia mziki wao, kuna msanii wa kike aliwahi kulalamika kulipwa laki 3 na ni msanii mkubwa katika tasnia ya bongofleva. Ambae aliamua kujitenga nao na leo hii akiamu kuandaa show yake mlimani city anajaza ukumbi. Na hadi leo hutokaa usikie nyimbo zake zikipigwa redioni pale, na bado anafanya vizuri.

Tuishi kwa upendo wanadamu, tupendane, wote tunapita hapa, hutobeba chochote kwenda nacho kaburini zaidi ya malipo ya matendo yako hapa duniani.
 
sio lazima kupiga nyimbo ya msanii
1. ila kuwafanyisha wasanii shoo, jingle na matangazo bila malipo au malipo kidogo is not fair.

2. kumleta msanii wa nje na kumlipa kuliko was ndani pia sio fair

3. kuwarubuni wasanii kuhusu kulipwa mirahaba nyimbo zao zikisikika redioni kutaua mziki sio fair pia
 
1. Hapo ndio utajua akili.za msanii ni binadamu au ng'ombe unapelekwa kama kuku aliekatwa kichwa bila kureasoning
2. Msanii gani wa hapa anaweza kulipwa sawa na Davido au Wizkid achilia mbali hao wa nje
3. Malipo ya mrahaba kwa Wasanii - JamiiForums
 
Na mtu asipo mposti marehemu kwenye account zake za kijamii kosa liko wapi?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Alishafanya, nakumbuka kuna siku aliwahi kuagiza siku nzima isipigwe bongo fleva kwenye hiyo redio na hazikupigwa kweli. Huku vijana wake wakiteleza siku nzima na msemo wa "bosi kasema".

Anyway, pumzi zisitutie kiburi na kujikuta tunajiropokea hovyo. Hapo umesema vipi ukiamua kuweka wafanyakazi wote ambao ni kabila lako, sawa unaweza, lakini hebu jaribu kuweka tangazo la kazi na moja ya sifa ya muombaji iwe ni kabila uone utakavyofuatiliwa. Haiwezekani kila mtu ajiendeshe anavyotaka, haiwezekani. Hii ni nchi.

Kuhusu upige nyimbo ya nani na ya nani usipige, hakuna shida, unaweza ukachagua utakavyo, chamsingi tuone wasanii wetu wanabadilika kupitia mziki wao, kuna msanii wa kike aliwahi kulalamika kulipwa laki 3 na ni msanii mkubwa katika tasnia ya bongofleva. Ambae aliamua kujitenga nao na leo hii akiamu kuandaa show yake mlimani city anajaza ukumbi. Na hadi leo hutokaa usikie nyimbo zake zikipigwa redioni pale, na bado anafanya vizuri.

Tuishi kwa upendo wanadamu, tupendane, wote tunapita hapa, hutobeba chochote kwenda nacho kaburini zaidi ya malipo ya matendo yako hapa duniani.
Hata kama ni wewe umeanzisha redio, sio yako tena ni ya wote hatuwezi kuziba masikio tusisikie . Kwa hiyo hakuna kuchagua msanii fulani kwa sababu ya chuki zako juu yake usipige muziki wake. Ndio maana kuna vitu huwezi kutangaza hata kama wewe ndio mwenye radio stesheni. Nafikiri kuna sheria zipo lakini hazijafuatiliwa tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom