Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 14,176
- 25,919
Juzi hapa nilikuwa Uturuki. Ni nchi ya watu ambao dini yao inaruhusu kuwa na mke zaidi ya mmoja, lakini wanawake katakata hawakubali kuwa katika ndoa ya mke zaidi ya mmoja, na wanaume wao wanaelewa hilo. Nimewaheshimu sana wanawake wa Uturuki kwa kujitambua kwa namna hii.
Hili ni jambo ambalo siku zote nimeshindwa kuwaelewa wanawake, na wala mtu asiniambie dini yangu inaruhusu. Mwanamke anakuwa katika akili gani hadi anakubali kuolewa kama mke wa pili, au wa tatu?
Kuolewa mke wa pili bado naona kama ningekuwa mwanamke nisingekubali kamwe, sasa wa tatu? Wa nne? Kwamba unakuwa na shida sana ya kupata mwanaume wako au una hali mbaya ya kiuchumi ndio ukakubali?
Na siamini kabisa kwamba yule mwanamke unaemkuta kwa huyo mumeo anafurahia kitendo cha wewe kuja kama mke wa pili au mbaya zaidi, wa tatu au wa nne.
Kwa nini wanawake hamtaki kujikomboa katika jambo hili? Sidhani kama nitamheshimu mwanamke anaekubali kuolewa mke wa tatu au wa nne; labda kidogo wa pili nitamuelewa. Mie naona kama anaekubali kuingilia ndoa ya wengine ambayo tayari ina mke mmoja au wawili kufikiri kwake hakupo sawa.
Nadhani ni Safari Sound au Marquiz waliwahi kuimba, "kama nitakuwa mke wa pili nakubali, lakini kama ni watatu sikubali hata kidogo nasikitika"