maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Miaka ya nyuma kidogo niliwahikuona kikundi cha wafungwa wakienda kufanya kazi za usafi kumalizia vifungo vyao katika ofisi za mkuu wa wilaya (bomani)
Wafungwa hao ambao nao kama Mramba na Yona walipunguziwa adhabu kwa kutakiwa kufanya kazi za kijamii, sikuona wakikabidhiwa zana yoyote ya kufanyia kazi hizo mbali na fagio na majembe waliyobeba kutoka makwao.
Cha ajabu kinachofanyika hivi sasa kwa akina Mramba waliowaibia watanzania mabilioni ya kodi yao kinatia kinyaa, eti wanakabidhiwa maovaroli, gumboots, glovu na vizuia vumbi katika kile kinachoonekana kama kahafla kadogo.
Ilitakiwa wakabidhiwe vifaa hivyo na mfungwa mwenzao ndio hadhi yao si kukabidhiwa na mganga mkuu, hawa ni wezi tu na wafungwa kw nini wananyenyekewa kama wanaenda kufanya utafiti?